Anga la washenzi na Joana anaona kitu usiku

ANGA LA WASHENZI ---- 02




Simulizi za series






“Vipi, kaka kuna tatizo?” Mwanamke aliuliza. Alikuwa amevalia suruali ya jeans na tisheti nyeupe ya bia ya Serengeti. Mkono wake wa kuume alikuwa ameshikilia sahani ndefu ya plastiki iliyobebelea kinywaji cha Balimi.
.
.
.
“Hamna tatizo dada,” Jona alijibu akipangusa uso. Alinyanyua kinywaji chake akapiga mafundo mawili. Mwanamke alimtazama kwa mashaka. Ni wazi alikuwa anastaajabu kutingwa kule kwa mwanaume huyo.
.
.
.
“Samahani,” akasema. “Nilitaka kujua kama utahitaji chochote toka jikoni.”
“Ooh, kuna chakula gani?” Jona akauliza akiketi vema kitini.
“Nyama ya kukaanga, rosti, ndizi, chips na ugali.”
.
.
.
Jona akatazama saa yake ya mkononi. Muda ulikuwa umeenda, na pia alihisi uchovu. Aliona ni vema akabeba chakula moja kwa moja aende nacho nyumbani, hivyo akaagizia na kungoja.
.
.
.
Baada ya muda mfupi, chakula kikaletwa, akalipia na kuondoka.
Toka hapo bar mpaka nyumbani kwake si mbali. Mwendo wa wastani ungekufikisha kwa takribani dakika kumi. Kama ukikazana unaweza kuchukua hata dakika tano tu. Ila Jona hakuwa na haraka na nyumbani. Hakuwa na cha kuwahi, labda kama kungekuwa kuna mvua ingemkimbiza. .
.
.
Mvua ilikuwa imekata, manyunyu tu ndiyo yalikuwa yanashuka. Nyumbani hakukuwa na mtu wa kumngojea, anaishi peke yake. Miguu yake ilitembea taratibu akitazama chini. Alipokaribia nyumbani kwake, akaona kuna gari limesimama kwa mbele, shaka likampata.
Alisimama upesi, akalichambua gari hilo. Alisogea kidogo apate kuliona vema. Mara akagundua ni lile lile aliloliona kule kazini likiwa limesimama, na kisha kuondoka.
.
.
.
Lilikuwa ni Range Rover Sport, pleti namba yake ya Kenya.
Jona akajikuta anapata maswali. Akiwa hapo anaendelea kutazama, akamuona mwanamke mmoja akitokea gizani, akapanda ndani ya gari hilo upesi. Mavazi ya mwanamke huyo yalimfanya Jona aamini ndiye yule mwanamke aliyemtembelea kazini akidai mzigo wa Beatrice.
.
.
.
Ina mana amenifuata nyumbani? Alijiuliza. Kumbe ndiye yeye aliyekuwa ndani ya gari hilo kule nje ya mabanda!
.
.
.
Hakutoka hapo alipokuwa amejibanza. Macho yake yaliendelea kutazama gari akingojea liondoke. Aliminya mfuko wa chakula, akasonya.
.
.
“Chakula kinapoa.”
.
.
Punde anamuona mwanaume mmoja mrefu akiwa kando na gari. Hakujua ametokea wapi. Mwanaume huyo aliegeza mikono yake dirishani mwa gari akasimama hapo kwa muda kidogo. Bila shaka alikuwa anaongea jambo na mtu ama watu waliomo ndani ya gari. .
.
.
Alitazama huku na kule, akapanda kwenye chombo wakaondoka. Jona alisindikiza hilo gari mpaka lilipoyoyoma kisha akatoka alipokuwa na kuenenda nyumbani kwake. .
.
.
Ilikuwa ni nyumba ya wastani, sebule na vyumba viwili, yenye uzio mfupi wa tofali na geti dogo jeusi. Ilikuwa kimya na tulivu sana, pia ilikuwa giza. .
.
.
Jona alikula kisha akaelekea chumbani kwake pasipo kupoteza muda. Kilikuwa ni chumba kipana kidogo, kitanda kikubwa na kabati moja kubwa la nguo lenye kioo kipana. Pembezoni mwa kabati hilo kulikuwa kuna kitu kikubwa chenye pembe nne kikiwa kimefunikwa na shuka la kijivu.
Jona alioga, kisha akafungua kabati lake na kitoa kisanduku fulani cha mbao, kidogo kwa umbo. Alikifungua, ndani yake kulikuwa kuna brashi kadhaa za kuchorea, mirija kadhaa ya rangi na penseli za mikaa, charcoal pencils.
.
.
.
Alikiweka kisanduku hicho juu ya stuli aliyosogeza karibu na kitu kilichofunikwa na shuka, kisha akalibandua shuka hilo. Kumbe hapo kulikuwa kuna makaratasi lukuki meupe marefu, mahususi kwa ajili ya kuchorea.
.
.
.
Karatasi ya kwanza kabisa ilikuwa ina picha ya mwanamke mrembo mwenye nywele za rasta. Jona aliitazama picha hiyo kwa sekunde kadhaa akifikiria jambo.
.
.
.
Mwanamke alikuwa anatabasamu, macho yake yaliangaza. Jona naye akajikuta anatabasamu, ila macho yake yakiwa mekundu.
.
.
.
Alifungua picha nyingine, picha ya mtoto wa kiume mwenye makadirio ya miaka mitatu.
.
.
.
Alitazama picha hiyo kwa sekunde kadhaa kabla hajaigeuza na kukutana na karatasi mpya isiyo na mchoro wowote. Hapo akaanza kuchora kwa kutumia penseli.
.
.
.
Hakutazamia popote pale isipokuwa alirejea kichwani mwake. Alichora picha ya mwanamke, yule aliyekuja kumtembelea ofisini akidai mzigo wa Beatrice. Alimchora mwanamke huyo hivyo hivyo kama anavyoonekana kuanzia kichwani mpaka kifuani asisahau hata vazi.
.
.
.
Alipomaliza aliketi kando, akitazama picha hiyo kwa umakini. Alijiuliza maswali kadhaa lakini hakuyapatia majibu. Alitamani Beatrice angekuwepo karibu ili amuulize, au basi angekuwa na simu ampigie.
Mwishowe anaamua kuipuuzia, anafuata jokofu sebuleni na kutoa chupa kubwa ya whisky anayoanza kuigida akielekea chumbani. Alikunywa chupa yote, kisha akalala.
.
.
.
Hawezi kulala pasipo kufanya hivi. Hujaza jokofu lake mara kwa mara kwa vileo vikali, kwa kazi moja tu, kumsaidia alale.
.
.
.
Asipokunywa, usingizi huwa mrefu kupitiliza. Ataamka na kushtuka kila mara. Hatapata amani.
Amekuwa akifanya hivi kwa takribani miaka mitatu sasa. Tangu pale alipoacha kazi yake ya uaskari, akiwa inspekta mwadilifu. .
.
.
Ni miaka hiyo ya nyuma, mwanaume huyu alikuwa na furaha akitenda kazi yake kiufanisi. Alisuluhisha kesi kedekede zilizoonekana ngumu na zisizowezekana mbele ya macho ya wengine. Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kumaliza makundi ya majambazi yaliyokuwa yameweka makazi yake ndani ya jiji la Dar es salaam.
.
.
.
Alifahamika kwa jina la Joh 'the knife', moto wa kuuotea mbali. Mwanaume mwenye mateke mazito, ngumi za kasi na matumizi mazuri ya silaha, haswa kisu. Hata kivuli chake kilikuwa kinaogopesha.
.
.
.
Simulizi hiyo ya kupendeza ilikuja kuhitimishwa muda mfupi baada ya baba yake mzazi alipofariki akiwa kazini, kituo cha polisi. Babaye alikuwa ni miongoni mwa maafisa polisi waliouawa kwenye mashambulizi ya majambazi vituoni vya polisi kwa dhumuni la kupoka silaha.
.
.
.
Ilikuwa bado miezi mitatu tu mzee huyo astaafu, adha hiyo ya kifo ikamkumba. Jambo hili lilimuuma sana Jona, akaapa kutafuta wahusika wote na kuwatia nguvuni. Ilimgharimu mwezi tu kufanikisha adhma hiyo. Alipomaliza akaamua kuacha kazi papo hapo.
Maamuzi haya hakushawishiwa na yeyote yule isipokuwa akili yake. Alirudisha kila kitu cha jeshi akiandika barua ya kushindwa kuendelea na majukumu. Barua hiyo haikueleza sababu, bali tu hitaji.
.
.
.
Kiuhalisia, Jona alisononeshwa sana na namna jeshi la polisi lilivyomhudumia na kumjali marehemu baba yake. Aliona anastahili zaidi ya kile alichopewa na jeshi hilo. Alilipigania sana, alilitendea kazi kwa uadilifu na kwa uaminifu. Heshima aliyopata, haikuwa hata theluthi ya yale aliyotenda.
.
.
"Nami nikifa nitatendwa hivi hivi," alikuwa anasema Jona.
"Kama wameshindwa kumthamini baba yangu aliyewatumikia miaka nenda rudi, vipi kwangu? Familia yangu itaachwaje?"
.
.
.
Aliona kazi hiyo haimfai. Aliamua ahamishie nguvu zake kufanya mambo mengine yatakayomletea faida zaidi, ambayo ni kujihusisha na biashara. Kuwepo ndani ya jeshi la polisi kulikuwa kunamkumbusha baba yake na kifo chake. Mara kadhaa alijikuta anajiuliza endapo angekuwa katika nafasi ya baba yake, familia yake ingebakije, ingeishije? Upuuzi.
.
.
.
Alitaka kupumzisha akili yake na purukushani. Alikuwa na ndoto za kufanya biashara, atengeneze faida kisha aende mbali kabisa, ulimwengu mwingine ambapo hakutakuwa na simu za kuitwa ofisini wala kazi za kutumikishwa. Atakuwa na familia yake tu, karibu kabisa na maji ya bahari, visiwa, samaki, moto na miti.
Ila matarajio hayo yote yanakatwa ghafla kana kwamba kibatari mbele ya kimbunga. Familia yake inauawa kwenye moto mkali ulioteketeza nyumba. Biashara yake ya kusafirisha korosho nje ya nchi inakufa, mtaji unakata. .
.
.
Mambo haya yanatukia kwa haraka sana. Yanamwacha Jona katika fikirishi kali maisha yake yakigeuka juu chini, chini juu. Ni ndani ya muda mfupi anapoteza mihimili yake ya maisha. Anageuka kuwa fukara, na ombaomba.
.
.
.
Katika kipindi hicho cha ukata mnene, jeshi la polisi likatupa ndoana kwa Jona kumtaka arejee kazini kabla hajafa kibudu.
.
.
.
Lakini, ingawa Jona hakuwa na mbele wala nyuma, akakataa kata kata, wakati huo hana hata uhakika wa chakula mezani.
Lakini je nani aliyapanga mambo haya yote kwa Jona? Yalitukia tu? .
.
.
Taarifa ya kikosi cha zimamoto na uokoaji, ilisema nyumba iliungua kwa hitilafu za umeme. Sababu ambayo haikukuna kabisa kichwa cha Jona kwani aliamini aliweka makazi yake katika usalama kwa kufunga vifaa vya kuzima umeme punde tu hitilafu inapobainika.
.
.
.
Isitoshe, kama ukimuuliza leo hii kwanini biashara yake, iliyoanza kuchanua, ilikufa hatakupa jibu la kueleweka. Hajui. Ni ndani ya juma moja tu, mtandao wake wa biashara ukakata huko Vietnam, mizigo yake ikazuiliwa bandarini na kugubikwa na urasimu mkubwa.
.
.
.
Kama haikuwa kipaji chake cha kuchora, hakujua maisha yake yangeenda wapi. Angalau alipata chakula na hata nauli za kumsogeza toka eneo moja kwenda lingine. Japokuwa pesa ilikuwa finyu!
Sasa kivipi mtu huyu atalala pasipo kilevi? Kwake, haikuwezekana. Alishuka chini kama embe lidondokavyo mtini. Alikuwa kama bado yu kwenye bumbuwazi. .
.
.
Ikiwa ni kwenye komo la usiku, majira ya saa kumi na moja, gari nyeusi Mark X, inasogea mbele kidogo ya geti la Jona na kusimama. Anashuka mwanamke mmoja mrefu aliyevalia kimini kifupi cheusi na viatu vyenye kisigino kirefu.
.
.
.
Mwanamke huyo alikuwa na nywele nyingi alizozikusanya na kuzibana kwa kamba nyekundu, uso wake mnene ulikuwa una miwani ya macho yenye fremu nzito.
.
.
.
Aliegemea gari akitazama nyumba ya Jona. Punde akamwona mwanaume huyo akifungua mlango na kutoka ndani.
Ilikuwa rahisi kwake kumuona Jona kuliko Jona kumuona kwani yeye alikuwa gizani wakati Jona akiwa kwenye mwanga.
.
.
.
Jona alifika getini ndiyo akajua kuna mtu yupo kando. Alishtuka, lakini hakumpa faida hiyo mgeni. Alisogea kwa kujiamini akasimama akimtazama mwanamke aliyekuwa hapo.
.
.
.
"Wewe nani?" Aliuliza pasipo salamu. Macho yake yalikuwa mekundu. Alikunja ndita.
"Habari yako?" Mwanamke akasalimu kwa sauti tamu.
"Nzuri," Jona akajibu.
"Samahani kwa kukusumbua, Jona. Najua huu ndio muda pekee wa kukupata maana umekuwa ukishughulika na kubanwa kwa siku nzima. Kwa jina naitwa Nade, ni mtumishi wa Mheshimiwa Eliakim Mtaja, nimekuja kukufikishia wito wake binafsi kwako. Anakuhitaji.
"Ananihitaji kivipi?" Akauliza Jona.
"Nadhani ingekuwa vizuri ukaongea naye, sina majibu ya kukuridhisha. Naweza nikakupeleka?"
"Hapana, huwezi."
"Jona, sasa mheshimiwa atakupataje?"
"Sijui."
"Una simu?"
"Hapana."
.
.
.
Mwanamke alifungua gari mlango wa nyuma akatoa Nokia xperia nyeusi akamkabidhi Jona.
.
.
.
"Ina kila kitu. Bila shaka mtawasiliana kwa kutumia hiyo."
Jona akapandisha kichwa juu.
"Sawa," alijibu kiufupi.
"Naweza nikakupeleka job?" Mwanamke aliuliza.
"Hapana," akajibu Jona. "Nashukuru."
.
.
.
.
***
***
 
JOANA ANAONA KITU USIKU – 03

Mama yake alimsihi aende huko msibani akatoe pole zake maana walikuja kupewa taarifa mapema sana na haitakuwa vema endapo asipoenda. Akakubali na kuahidi kwenda, mamaye akaondoka zake.
.
.
.
Akabakia pale kitandani akijuliza sana kuhusu mauaji hayo. Asipate majibu, akaamua kunyanyuka na kujiandaa. Akanywa chai na kujivesha nguo, gauni refu la mauamaua na kikoi, kabla hajatoka kwenda kwa jirani.
.
.
.
Hakukuwa mbali sana, alifika akawakuta ndugu wa marehemu wakiwa wameketi sebuleni, watatu kwa idadi: mmoja alikuwa mwanamama wakati wawili wakiwa wanaume.
.
.
.
Umri wao ulionekana mkubwa. Mwanaume mmoja alikuwa na kiwaraza mwingine kichwa kikijaa mvi. Mwanamke alikuwa na kifua kilichochoka, na hata uso wake ulionyesha ni mtu aliyekula chumvi.
.
.
.
Ila nywele zake zilikuwa nyeusi ti. Pengine ni kutokana na sababu za kutumia madawa.
.
.
.
Nyuso zao wote zilikuwa zinafanana, kama ungesema wametoka kwenye mfuko mmoja wa uzazi ungekuwa hujakosea kabisa. Baba na mama mmoja.
.
.
.
Wanaume walikuwa na nyuso kavu wakati mwanamke akiwa ana macho mekundu yalioashiria ametoka kulia muda si mrefu.
.
.
.
“Karibu,” akasema mwanamke, yule ndugu, kumpokea Joana.
.
.
.
“Ahsante,” akaitikia Joana kwa sauti kavu, pole na ya chini kisha akasema: “Poleni kwa msiba.”
.
.
.
Hakuitikiwa. Ndugu wote walimtazama kwa macho makali. Aliona sura zao zimebadilika na kuwa za kutisha. Akaogopa.
.
.
.
Mwanaume yule mwenye kiwaraza, haraka ya kufumba na kufumbua, akachoropoa gongo moja kubwa chini ya sofa. Akaropoka:
.
.
“Muuaji mkubwa wewe! Umemuua dada yangu, na hapa unakuja kufanya nini?”
.
.
.
Joana akapigwa na bumbuwazi, akakosa neno la kusema. Mdomo ulijing’atang’ata akihangaika apate hata neno la kujitetea.
.
.
.
Asipewe hata muda, mwanaume mwenye kiwaraza akatimua mbio kumfuata akiwa amelenga kumbamiza na gongo. Joana akakimbia upesi kufuata mlango.
.
.
.
“Nakuua mlozi mkubwa wewe!” alifoka mwanaume. Uso wake ulikuwa umebeba hasira na dhamira kweli ya kutenda.
.
.
.
Joana alifungua mlango akatoka ndani, akakimbia upesi akiwa anapiga kelele za kuomba msaada.
.
.
.
Gauni lake alilolivaa halikumpa nafasi ya kukimbia vema. Na hata hivyo mbio zake hazikuweza kumuacha mwanaume anayemkimbiza, hivyo ndani ya muda mfupi akatiwa nguvuni kwa kusukumiziwa chini.
.
.
.
Akadondoka na kubiringita mara tatu kabla hajakoma na kutulia. Mwanaume mwenye kiwaraza alikuwa tayari ameshamfikia, amesimama akimtazama.
.
.
.
“Muuaji wewe! Mlozi wewe!” akafoka mwanaume mwenye kiwaraza. “Leo nakumaliza!”
“Si mimi!” Joana akapaza sauti akilia. “Usiniue tafadhali, si mimi!”
“Si wewe! Ni nani? Unadhani hatujui yaliyotukia huko chuo ulipotokea?”
“Sijaua mtu yeyote chuo. Sijaua yeyote!”
“Nani anayeua kama si wewe?! Sasa umerudi nyumbani unataka kutumaliza na sisi?”
.
.
.
Kabla Joana hajasema jambo, mwanaume mwenye kiwaraza akanyanyua gongo lake juu na kumtwanga Joana kichwa.
.
.
.
Mara giza likatwaa!
.
.
.
Mara Joana akashtuka akivuta hewa kwanguvu na kutoa macho kana kwamba mtu anayezama majini.
.
.
.
Alitazama, akajiona yupo kando kidogo ya mlango wa jirani. Watu walioketi sebuleni walikuwa wanamtazama kwa mshangao.
.
.
.
“Binti, upo sawa?” akauliza mwanamke pekee aliyekuwa ameketi sebuleni.
.
.
.
Joana akajitazama na kujikagua. Uso wake ulikuwa na bumbuwazi. Alimtazama mwanaume yule mwenye kiwaraza, hakuona shida yoyote, alikuwa ameketi akimtazama kwa mshangao.
.
.
.
Ina maana alikuwa ndotoni?
.
.
.
Hapana, ndoto gani mtu akiwa macho? Sasa ilikuwa ni nini? Joana akateswa na maswali.
.
.
.
“Karibu binti, karibu!” Akakaribishwa tena na sauti ya mwanaume, alikuwa ni ya yule mwenye mvi lukuki kichwani. Akapiga moyo konde na kusogea mpaka kwenye kiti alipoketi na kujitambulisha.
.
.
“Oooh Joana! Umekua kweli,” akashangaa mwanamama. “Unajua nilikuja huku muda mrefu sana uliopita. Nilikuona ukiwa mdogo sana. Hata kukutambua nimepata shida, nusura nitafute miwani.”
.
.
.
Joana akatabasamu kwa mbali. Tabasamu la uongo. Alitoa pole zake na kuelekeza kwa namna alivyoshangazwa na kifo hicho cha ghafula.
.
.
“Hata sisi tumeshangazwa mno,” akasema mwanaume mwenye kiwaraza. “Usiku wetu huu haukuwa mzuri kabisa. Katikati ya usiku wa manane tunapigiwa simu na jirani wa karibu, anatueleza amesikia kelele kali za kuomba msaada toka humu ndani.
.
.
.
Alitoa taarifa polisi ila haikusaidia kwani polisi walimkuta akiwa tayari ameuawa.”
.
.
.
Ndugu yule mwanamke akatoa machozi. Alichomoa leso akajifuta huku akikabwa na kwikwi.
.
.
.
“Polisi wamesema watafuatilia, ila mpaka sasa hawajui wala kumhisi yeyote,” alisema mwanaume mwenye mvi, mwenye kiwaraza akadakia.
.
.
.
“Ajabu sana! ni wazembe kiasi gani.”
“Hapana!” Mwanamke naye akatia neno. “Wamesema hawajapata kiashiria wala ushahidi wowote. Si milango wala madirisha yamevunjwa. Ni chumba tu cha dada ndicho kilikuwa kimevurugika.
.
.
.
Muuaji atakuwa ni mtaalamu wa hali ya juu. Kinachonishangaza ni muuaji wa kaliba hiyo kumuua mtu kama dada yangu. Ina staajabisha. Kwa kipi?”
.
.
.
Maneno mengi yaliongelewa. Mengine hata Joana hakuyasikia. Akili yake ilikuwa inahama. Hakuwa ametulia.
.
.
.
Hakukaa sana akaaga na kurudi nyumbani.
.
.
.
Alienda moja kwa moja chumbani kwake akampigia mpenzi wake, Moa. Alimweleza kila kitu kilichomkumba. Moa akastaajabu, akamuahidi kuja kumtembelea keshokutwa.
.
.
.
“Usijali, mpenzi. Nitatafuta namna,” alisema Moa kisha simu ikakatwa.
.
.
.
Joana akatoka ndani na kujipaki kwenye gari, akaelekea hospitali. Akaonana na daktari na kumuelezea yanayomsumbua, kuona damu mwilini pasi na taarifa wala kuona mushkeli.
.
.
.
Akafanyiwa vipimo kisionekane kitu. Akaondoka zake kwenda kutembea angalau apumzishe akili yake.
.
.
.
Alienda beach, akatembea ufukweni akichezea maji. Alivua nguoze akaogelea, alipochoka akatoka na kujilaza juu ya mchanga akijianika juani.
.
.
.
Kwasababu haikuwa siku na muda wa mapumziko, watu hawakuwa wengi fukweni wala ndani ya maji. Ila hilo halikuwa kwazo kwa Joana, alifurahia maana hapendi bughdha wala mahali penye mkusanyiko wa watu.
.
.
.
Ilipofika jioni, akajirudisha nyumbani.
.
.
.
Kweli ilipofika keshokutwa, Moa akaja Ubelgiji wakakutana mahala tulivu. Ndani ya hoteli moja ya nyota tatu walipojilaza kwenye ukumbi wa bwawa la kuogelea.
.
.

Walikuwa wamevalia nguo za kuogelea wakijianika kwenye jua baada ya kuogelea na kujipaka mafuta ya jua.
.
.
.
“Joana, nimekusikia hayo yote uliyosema. Kweli yanatisha na yananyima amani. Ila kuna kitu ningekuomba. Naomba uwe mvumilivu. Najua yatapita.”
“Yatapitaje, Moa?” akastaajabu Joana. “Sijui nini shida, siwezi kulitatua. Kila siku natingwa na mawazo. Napata mashaka sana, Moa. Sana! Maisha yangu hayana furaha kwakweli. Kuna kitu hapa. Kuna kitu!”
.
.
.
Moa alijitahidi sana kumtuliza Joana. Ila mwisho wa siku kabla hawajaachana, akamwambia:
“Naomba hiyo bangilii aliyokupa mama.”
“Kwanini?” Joana akadadisi.
“Naona haijakupendeza. Unahitaji zawadi nyingine tofauti na hiyo.”
“Ila mama yako hatajisikia vizuri.” Joana alipata shaka.
“Usijali, yule ni mama yangu, najua namna ya kuendana naye.”
.
.
.
Kishingo upande, Joana akavua bangili na kumkabidhi Moa. Wakaagana na kuachana.
.
.
.
Baada ya siku tatu, Moa akawa yupo kwao, Brazil, akipata chakula cha pamoja na wanafamilia.
.
.
.
Walikula kwa ukimya kila mmoja akifurahia chakula hicho kitamu. Mpaka wanakaribia kumaliza, hakuna mtu aliyekuwa anaongea. Ila kabla hawajatoka na kusafisha meza, mama akaita:

“Moa!”
“Naam,” Moa akaitikia na kumtazama mama yake.
.
.
.
Uso wa mama ulikuwa umefumwa kwa hasira. Alimtazama Moa kana kwamba chui anamtazama swala mawindoni.
.
.
.
“Nimekuta bangili chumbani kwako nikifanya usafi. Umeitoa wapi bangili ile na wakati nilimpa Joana?”
“Amenikabidhi,” Moa akajibu kifupi.
.
.
.
Mama hakusema tena jambo. Wakasafisha meza na shughuli zingine zikaendelea.
.
.
.
Baadae majira ya usiku, saa tano, Mama akaenda kumgongea mlango Moa. Akaketi pembeni ya kitanda na kumueleza:
“Rudisha bangili hiyo kwa Joana. Umenielewa?”
“Mama ame…”
“Sitaki maneno, Moa. Nimekwambia rudisha hiyo bangili, sawa?” Mama alisema akitumbua macho yake meupe nje. Moa akaogopa.









****
 
unazingua tupia mojamoja mpk iishe anga la washenzi kwanza,hiyo nyengine mpk iishe hii si vizuri kuchanganya ugari na wali
 
Back
Top Bottom