Sioni hoja ya kujenga hapa zaidi ya simulizi za kale zenye maslahi kwa watu fulani fulani,sijui hoja hii kama inasaidia ujenzi wa madarasa na umasikini wa watoto wa kitanzania au ndo dirisha la kupotezea muda.
Wasioona hoja ya kujenga kikwelikweli wameiruka hii thread, hata hawajachangia.
Wewe kwa kuchangia tu, ushaipa relevance, ushaipa muda wako, ushaipa mawazo yako.
Ujenzi wa madarasa usingewezekana bila ya simulizi za kale, maana hata kabla ya maandishi, ujuzi wa ujenzi ulipitishwa kwa simulizi za kale, kizazi kwa kizazi, ma griot walihifadhi habari za falme, wahunzi walifundisha wana wao kazi na kadhalika.
Tatizo si kwamba simulizi ni za kale au mpya, kwa maana hamna kipya duniani, unachoona "simulizi za kale" kinaendelea mpaka leo, na kama ushakiri ni za "maslahi ya watu fulani" basi haziwezi kuwa za kale hivyo. Badala ya kuyaanika hayo maslahi ueleweke, unakimbia.
Umaskini wa watoto wa Kitanzania unaweza kuwa unaendana na tabia ya Kitanzania ya kuogopa authority.
Tabia ya Kitanzania ya kuogopa authority inachanua sana kwa mbolea ya dini.
Thread hii inatoa nafasi ya kuanika hili, na kwa wewe kukataa kuchangia kuonyesha hayo, umechangia moja kwa moja kuendeleza umaskini wa Tanzania, japo kwa kiasi kidogo.
Maneno yanaumba, na usidharau thread kwa sababu haijajikita moja kwa moja katika ujenzi wa barabara.
Kwani ujenzi wa barabara huanza kichwani na kwa kubadilishana mawazo kama katika thread hii.
Sema jingine, uliyosema juu yameonekana kukosa uzito.