msemakweli2
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 1,627
- 1,880
Ni hivi juzi tu simu imeita, napokea anajitambulisha mimi shemeji yako mke wa rafiki yako A, mimi namwambia aaah sawa shem,vipi kwema, anasema sio kwema rafiki yako kutwa na wanawake anahonga pesa nyumbani haachi hela ya matumizi watoto hawajali na mimi hela yake siioni nataka nimuache shem, namshauri hapana usifanye hivyo shem mna watoto wanawaangalia tena wakubwa, naomba niongee naye labda ameghafilika. akajibu nitashukuru shem, anasema haiwezekani anapenda wanawake wa nje wakati mkewe nipo shem au ana laana ya wazazi wake huyo, namjibu hapana shem usiseme hivyo nitazungumza naye. anajibu sawa shem nashukuru.
Siku ya kwanza yapili anapiga tena shem na mimi nimeona nitafute mtu anitimizie shida zangu, namjibu usifanye hivyo sio vizuri shem ubaya haulipizwi kwa ubaya kaeni muyamalize, namwambia halafu utakayempata huko nje huwezi kujua kama naye tabia yake itaendana na unayoyataka unaweza kupata akawa zaidi ya uliyenaye, anajibu ni kweli shemeji, then anasema ahsante then anakata simu.
Baada ya dk 5 inaingia msg anasema SHEM NIMEKUCHAGUA WEWE,NAJUA UTANIPA NINACHOKIKOSA KWA RAFIKI YAKO. Daaah mwili unanisisimka kwakuwa sikutegemea mwanamke huyu tena wa rafiki yangu aniambie maneno haya, mpaka sasa hivi sijamjibu hii msg bado nawaza.