Anayoyafanya mumewe anataka nimfanyie yeye

msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,627
1,879
Ni hivi juzi tu simu imeita, napokea anajitambulisha mimi shemeji yako mke wa rafiki yako A, mimi namwambia aaah sawa shem,vipi kwema, anasema sio kwema rafiki yako kutwa na wanawake anahonga pesa nyumbani haachi hela ya matumizi watoto hawajali na mimi hela yake siioni nataka nimuache shem, namshauri hapana usifanye hivyo shem mna watoto wanawaangalia tena wakubwa, naomba niongee naye labda ameghafilika. akajibu nitashukuru shem, anasema haiwezekani anapenda wanawake wa nje wakati mkewe nipo shem au ana laana ya wazazi wake huyo, namjibu hapana shem usiseme hivyo nitazungumza naye. anajibu sawa shem nashukuru.

Siku ya kwanza yapili anapiga tena shem na mimi nimeona nitafute mtu anitimizie shida zangu, namjibu usifanye hivyo sio vizuri shem ubaya haulipizwi kwa ubaya kaeni muyamalize, namwambia halafu utakayempata huko nje huwezi kujua kama naye tabia yake itaendana na unayoyataka unaweza kupata akawa zaidi ya uliyenaye, anajibu ni kweli shemeji, then anasema ahsante then anakata simu.

Baada ya dk 5 inaingia msg anasema SHEM NIMEKUCHAGUA WEWE,NAJUA UTANIPA NINACHOKIKOSA KWA RAFIKI YAKO. Daaah mwili unanisisimka kwakuwa sikutegemea mwanamke huyu tena wa rafiki yangu aniambie maneno haya, mpaka sasa hivi sijamjibu hii msg bado nawaza.
 
Bro usimwamini mwanamke kila anacho kueleza,

Wanawake huwa hawatongozi kwa maneno kama sisi tufanyavyo, ila wao huja na sababu na visa.

Huyo unaweza kukuta hana ugomvi na mumewe na kila kitu anapewa, ila katumia njia hiyo ili uingie kirahisi baada ya kushindwa baadhi ya njia.

Hii imetukuta wanaume wengi,Nikushauri ukae mbali na Huyo mwanamke bro,Wake za watu siku hizi ndo walivyo,wakitaka kuchepuka huleta sababu za hovyo ili usimwone ni Malaya.
 
Dem anataka kujisafisha kwa mumewe kupitia Shem wake
 
Bro usimwamini mwanamke kila anacho kueleza,

Wanawake huwa hawatongozi kwa maneno kama sisi tufanyavyo, ila wao huja na sababu na visa.

Huyo unaweza kukuta hana ugomvi na mumewe na kila kitu anapewa, ila katumia njia hiyo ili uingie kirahisi baada ya kushindwa baadhi ya njia.

Hii imetukuta wanaume wengi,Nikushauri ukae mbali na Huyo mwanamke bro,Wake za watu siku hizi ndo walivyo,wakitaka kuchepuka huleta sababu za hovyo ili usimwone ni Malaya.
Naunga mkono hoja. Huyo mwanamke malaya tu huenda anadanganya ila anamtaka shemeji yake.
 
Bro usimwamini mwanamke kila anacho kueleza,

Wanawake huwa hawatongozi kwa maneno kama sisi tufanyavyo, ila wao huja na sababu na visa.

Huyo unaweza kukuta hana ugomvi na mumewe na kila kitu anapewa, ila katumia njia hiyo ili uingie kirahisi baada ya kushindwa baadhi ya njia.

Hii imetukuta wanaume wengi,Nikushauri ukae mbali na Huyo mwanamke bro,Wake za watu siku hizi ndo walivyo,wakitaka kuchepuka huleta sababu za hovyo ili usimwone ni Malaya.
Asipokuelewa basi kashindikana
 
Basi huyo atakuwa malaya tu. Unaweza kukuta mumewe ni mtulivu na hajishugulishi na michepuko ila yeye anakutafuta kwa tamaa zake za ngono. Temana nae mkuu.
mumewe namjua ni mskaji wangu ni malaya balaa,nimeshamshauri lakini hashauriki
 
si ndio inaitwa kimasiara hiyo na imeanzishiwa uzi kabisa na wadau wanatiririka walivyokula kimasiara.
 
mumewe namjua ni mskaji wangu ni malaya balaa,nimeshamshauri lakini hashauriki
Mke atakuwa kiukweli anaumia, hasira na mihemko ya malipizi ndo inayomwendesha, inaweza kuwa kweli kaamua alipize akijua atatuliza machungu, na zaidi kaona akifanya na mtu wa karibu na mumewe atakuwa amemkomoa zaidi, mwambie hiyo sio busara, atafute kitu cha kufanya ata km ni juice au uji atafute genge auze, awe bize apoteze mawazo juu ya usaliti wa mumewe, kila akirudi jioni amechoka, anawaza atakuzaje mtaji, analala kesho anaamka na hekaheka za utafutaji, asimuulize tena mumewe kuhusu umalaya wake, ajikaze asioneshe hasira wala asiwe mgomvi kwa mumewe, aachane na mawazo ya kuchepuka maana hatokaa awe na amani. Kama ni mumewe ni mtu mwenye akili ataanza kubadilika mwenyewe
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom