Anayoyafanya mumewe anataka nimfanyie yeye

Wale ambao hatujaoa tusikate tamaa sababu ya huyu samaki aliyeoza, siku hizi samaki mmoja akioza unamchomoa na kutupa jalalani wanabaki wazima pekee.
 
Unaweza kuta huo ni mtego wamepanga na jamaa yako wanakupima kama unaurafiki naye wa kweli au wa kinafki.
 
Mke atakuwa kiukweli anaumia, hasira na mihemko ya malipizi ndo inayomwendesha, inaweza kuwa kweli kaamua alipize akijua atatuliza machungu, na zaidi kaona akifanya na mtu wa karibu na mumewe atakuwa amemkomoa zaidi, mwambie hiyo sio busara, atafute kitu cha kufanya ata km ni juice au uji atafute genge auze, awe bize apoteze mawazo juu ya usaliti wa mumewe, kila akirudi jioni amechoka, anawaza atakuzaje mtaji, analala kesho anaamka na hekaheka za utafutaji, asimuulize tena mumewe kuhusu umalaya wake, ajikaze asioneshe hasira wala asiwe mgomvi kwa mumewe, aachane na mawazo ya kuchepuka maana hatokaa awe na amani. Kama ni mumewe ni mtu mwenye akili ataanza kubadilika mwenyewe
akili kubwa,umeongea maneno ya busara mno
 
Wewe jamaa achana na huyo mwanamke kwani anataka kutengeneza uadui wa hatari kati yako na rafiki yako!!!! Kuna kifo hapo Ohoooooooh!!!!!!! Epuka mke wa mtu ni sumu ya hatari sana.
 
Aisee

Huyo mwanamke atulize akili anayotaka kuyafanya yatakuwa majuto ya baadae..nawe jitahidi umuepuke shetani..
 
Huyu anataka kumkomoa mumewe hivyo ukigusa tu hesabu urafiki wenu utaisha mwezi mrefu, maana atafajya kila njia mumewe ajue umemla
 
Huo ni mtego wa panya mtu.unapimwa akili mzee. Iyo idea itakuwa ya rafiki yako. Be warned.
 
Binadamu ni kiumbe complex sana, nadhani kuliko viumbe wote duniani. Nitajitahidi kusoma viumbe baadhi kujua complexities walizonazo, ila kwa sasa binadamu anaweza kuwa the most complex creature on planet earth.
 
Ni hivi juzi tu simu imeita, napokea anajitambulisha mimi shemeji yako mke wa rafiki yako A, mimi namwambia aaah sawa shem,vipi kwema, anasema sio kwema rafiki yako kutwa na wanawake anahonga pesa nyumbani haachi hela ya matumizi watoto hawajali na mimi hela yake siioni nataka nimuache shem, namshauri hapana usifanye hivyo shem mna watoto wanawaangalia tena wakubwa, naomba niongee naye labda ameghafilika. akajibu nitashukuru shem, anasema haiwezekani anapenda wanawake wa nje wakati mkewe nipo shem au ana laana ya wazazi wake huyo, namjibu hapana shem usiseme hivyo nitazungumza naye. anajibu sawa shem nashukuru.

Siku ya kwanza yapili anapiga tena shem na mimi nimeona nitafute mtu anitimizie shida zangu, namjibu usifanye hivyo sio vizuri shem ubaya haulipizwi kwa ubaya kaeni muyamalize, namwambia halafu utakayempata huko nje huwezi kujua kama naye tabia yake itaendana na unayoyataka unaweza kupata akawa zaidi ya uliyenaye, anajibu ni kweli shemeji, then anasema ahsante then anakata simu.

Baada ya dk 5 inaingia msg anasema SHEM NIMEKUCHAGUA WEWE,NAJUA UTANIPA NINACHOKIKOSA KWA RAFIKI YAKO. Daaah mwili unanisisimka kwakuwa sikutegemea mwanamke huyu tena wa rafiki yangu aniambie maneno haya, mpaka sasa hivi sijamjibu hii msg bado nawaza.
huo ni mtego wa kufanywa uwe fukara mtu kapanga mipango na mkewe that us ( POVERTY TRAP)
 
Back
Top Bottom