Anayewania kumrithi Fatma Karume TLS aikosoa Katiba

Anayewania kumrithi Fatma Karume TLS aikosoa Katiba

Mkuu,nakuhakikishia kuwa Wakili Msomi Wasonga hawezi kuwa Rais wa TLS. Historia yake, wakati ule Lissu akigombea,inamkwamisha na kumwangusha. Aprili tunakwenda Arusha kumkataa tena. Hawezi kutuzuga kwa kukosoa Katiba!
Mkuu hizi siyo kampeni kweli hizi? Au zimeanza? Ila hata mimi ngekuwa Mwanasheria huyo jamaa ningemla kichwa, alichemka sana wakati ule Lissu anagombea! Huyu yuko upande wa chama hatawafaa!!
 
Mkuu,nakuhakikishia kuwa Wakili Msomi Wasonga hawezi kuwa Rais wa TLS. Historia yake, wakati ule Lissu akigombea,inamkwamisha na kumwangusha. Aprili tunakwenda Arusha kumkataa tena. Hawezi kutuzuga kwa kukosoa Katiba!
Tukumbushana Mkuu
Ilikuwaje kwani?
Nimesahauuuu
 
Wengine tulikuwa tunajuwa TLS ni chama cha wanasheria kisichojali candidate ana mwongozo gani wa chama wala itikadi ya vyama vya siasa?!
Kumbe kigezo muhimu na kwanza ni lazima uwe shabiki wa CDM?!
Mbona haiweleki...
 
Hatuwezi kuzungumzia demokrasia kama Katiba ina upungufu ndani yake, lazima sisi wanasheria tuzungumze na kukubaliana na wasomi, wanazuoni na jamii kwa nia njema ya kupata kitu kizuri,” amesema Wasonga.
Imekaa vizuri sana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu,nakuhakikishia kuwa Wakili Msomi Wasonga hawezi kuwa Rais wa TLS. Historia yake, wakati ule Lissu akigombea,inamkwamisha na kumwangusha. Aprili tunakwenda Arusha kumkataa tena. Hawezi kutuzuga kwa kukosoa Katiba!
Historia yake ikoje? Hebu weka muhtasari hapa!
 
Hahaha huyu kibaraka, yale aliyokuwa akiyapendekeza Mwakyembe, na Kabudi huyu akishinda ndiye ataya implement.
 
Anayewania kumrithi Fatma Karume TLS aikosoa Katiba

Dodoma. Uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unatarajia kufanyika Aprili 6, 2019 Jijini Arusha, lakini mgombea wa nafasi ya urais, Godfrey Wasonga ameitaja Katiba ya Tanzania kuwa bado ina upungufu

pic+wasonga.jpg

BY Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
  • Wakili Godfrey Wasonga amejitosa kugombea nafasi ya urais wa TLS lakini ameutaja uongozi wa Tundu Lissu kwamba ulikuwa wa muda mfupi lakini ulikuwa na manufaa sana. Ameitaja Katiba ya Tanzania kuwa ina upungufu

Dodoma. Uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unatarajia kufanyika Aprili 6, 2019 Jijini Arusha, lakini mgombea wa nafasi ya urais, Godfrey Wasonga ameitaja Katiba ya Tanzania kuwa bado ina upungufu
Soma zaidi: Mambo matatu anayojivunia Fatma TLS
Wasonga ambaye anagombea kwa mara ya tatu sasa akiwania kumrithi Wakili Fatma Karume, amesema akipata nafasi ya kuongoza mawakili, ajenda yake kubwa itakuwa ni kufanya ushawishi kwa viongozi ili Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ifanyiwe mabadiliko.
“Hatuwezi kuzungumzia demokrasia kama Katiba ina upungufu ndani yake, lazima sisi wanasheria tuzungumze na kukubaliana na wasomi, wanazuoni na jamii kwa nia njema ya kupata kitu kizuri,” amesema Wasonga.
Mgombea huyo pia amemmwagia sifa Tundu Lissu akisema kuwa aliongoza na kuifanyia marekebisho makubwa TLS na kuongeza kuwa kama Lissu angepewa nafasi hiyo kwa muda zaidi huenda wangekuwa mbali zaidi.
Wakili huyo amesema kuwa uongozi wa Lissu aliyeshika nafasi hiyo kabla ya Fatma, unatakiwa kufuatwa na viongozi wanaoingia ndani ya TLS na kuboresha zaidi ndipo watafikia mafanikio.
Soma zaidi: Sita wawania kumrithi Fatma Karume TLS
“Lissu alituongoza vizuri sana, mimi nakubali uongozi wake isipokuwa tunatofautiana kwenye matusi na kejeli zake ndani ya Serikali, lakini lazima tukubali kuwa jamaa alifanya kazi nzuri sana yenye mfano wa kuigwa,” amesema.
Wasonga pia amesema kwamba akishinda na kuwa Rais wa TLS atakifanya chama hicho kuwa cha uwekezaji kwenye ardhi na atahamisha mikutano ambayo kila wakati inafanyikia Arusha ili kupeleka mikoani ambako gharama zitakuwa ndogo.
Soma zaidi: Lissu atumikia urais TLS kwa miezi sita tu, kuondoka Aprili

BAK unamjua huyu jamaa vizuri. Huyu ni CCM damu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo nafasi nadhani haina umuhimu kwa hicho chama, kwa nini mnabadirisha viongozi ndani ya muda mfupi nanmna hii?
 
Kakosea hakuwa na sababu ya Ku m associate Lisu kwenye kampeni zake.Every leader is unique kusema sijui nitaiga Lisu upuuzi mtupu.Tell your uniqueness basi.Uongozi sio copy cat
 
Back
Top Bottom