Anayewania kumrithi Fatma Karume TLS aikosoa Katiba

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,045
Anayewania kumrithi Fatma Karume TLS aikosoa Katiba

pic+wasonga.jpg


BY Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Wakili Godfrey Wasonga amejitosa kugombea nafasi ya urais wa TLS lakini ameutaja uongozi wa Tundu Lissu kwamba ulikuwa wa muda mfupi lakini ulikuwa na manufaa sana. Ameitaja Katiba ya Tanzania kuwa ina upungufu


Dodoma. Uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unatarajia kufanyika Aprili 6, 2019 Jijini Arusha, lakini mgombea wa nafasi ya urais, Godfrey Wasonga ameitaja Katiba ya Tanzania kuwa bado ina upungufu

Wasonga ambaye anagombea kwa mara ya tatu sasa akiwania kumrithi Wakili Fatma Karume, amesema akipata nafasi ya kuongoza mawakili, ajenda yake kubwa itakuwa ni kufanya ushawishi kwa viongozi ili Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ifanyiwe mabadiliko.

“Hatuwezi kuzungumzia demokrasia kama Katiba ina upungufu ndani yake, lazima sisi wanasheria tuzungumze na kukubaliana na wasomi, wanazuoni na jamii kwa nia njema ya kupata kitu kizuri,” amesema Wasonga.

Mgombea huyo pia amemmwagia sifa Tundu Lissu akisema kuwa aliongoza na kuifanyia marekebisho makubwa TLS na kuongeza kuwa kama Lissu angepewa nafasi hiyo kwa muda zaidi huenda wangekuwa mbali zaidi.

Wakili huyo amesema kuwa uongozi wa Lissu aliyeshika nafasi hiyo kabla ya Fatma, unatakiwa kufuatwa na viongozi wanaoingia ndani ya TLS na kuboresha zaidi ndipo watafikia mafanikio.

“Lissu alituongoza vizuri sana, mimi nakubali uongozi wake isipokuwa tunatofautiana kwenye matusi na kejeli zake ndani ya Serikali, lakini lazima tukubali kuwa jamaa alifanya kazi nzuri sana yenye mfano wa kuigwa,” amesema.

Wasonga pia amesema kwamba akishinda na kuwa Rais wa TLS atakifanya chama hicho kuwa cha uwekezaji kwenye ardhi na atahamisha mikutano ambayo kila wakati inafanyikia Arusha ili kupeleka mikoani ambako gharama zitakuwa ndogo.

Soma zaidi: Lissu atumikia urais TLS kwa miezi sita tu, kuondoka Aprili
 
Anajaribu sana kujisogeza kwa lissu na kumpaka mafuta ya mgongo ili anufaike. Wanasheria si WAPUMBAVU!

Mkuu,nakuhakikishia kuwa Wakili Msomi Wasonga hawezi kuwa Rais wa TLS. Historia yake, wakati ule Lissu akigombea,inamkwamisha na kumwangusha. Aprili tunakwenda Arusha kumkataa tena. Huwezi kutuzuga kwa kukosoa Katiba!
 
Back
Top Bottom