Anayekutawala amekuzidi Akili

Anayekutawala amekuzidi Akili

Superpower hawawezi kuwa Wawili katika ulí mmoja na zama moja. USA sasa hivi ndio Superpower ndiye anayetawala Dunia ikiwemo hao wachina.
Sidhani kama siasa za kimataifa na historia yake unazielewa vizuri hapa tutakesha.

Ila nikukumbushe civilization duniani haijaanzia ulaya na suala la kutawala watu kimabavu sio level of intelligence.
 
Umeandika mwngi yenye uelekeo wa ukweli Ila sio lazima iwe kweli..ni uelekeo tu .
Ni sawa' na bati ambalo halijapigiliwa vizuri upepo ukivuma nilipiga kelele Sana kama linang'oka kumbe lipo tu na upepo ukitulia nalo linatulia.
Hiyo Ni kichwa yako' huo' unatumia ndumu au bangi ..ukivuta unachangamka kweli..utandika wee Ila Moshi ukitulia na ww una tulia.
I know what I'm saying
 
ANAYEKUTAWALA AMEKUZIDI AKILI

Anaandika, Robert Heriel.
Mtibeli.

Ukiona mtu amekuzidi na kukutawala kisiasa, kiuchumi, kijamii au kiteknolojia basi fahamu kabisa mtu au jamii hiyo imekuzidi Akili.

Akili ndio inayotawala mambo yote duniani. Ili upewe Mamlaka na nguvu basi lazima uwe na akili kuwashinda wengine hasa hao unaowatawala.

Kijinsia, Mwanaume anaakili kuliko Mwanamke ndio maana anamtawala. Ingawaje zipo siasa na porojo za kuwafariji wanawake kuwa wanaakili kuwashinda wanaume lakini kiuhalisia Mwanaume anaakili zaidi kuliko Mwanamke. Ndio maana Mwanaume anamtawala Mwanamke.

Kijamii, Wazungu na jamii zao wanaakili kushinda Waafrika, na Waarabu na wachina na jamii zingine. Ndio maana wazungu miaka nenda rudi wanatawala huu ulimwengu.

Kuna ile kujidanganya kuwa utawala ni majaliwa lakini hata hiyo akili yenyewe ni Majaliwa. Kila kitu kwenye maisha ni Majaliwa.

Wanyama wa porini tunawatawala kwa sababu ya sisi kuwashinda kiakili.
Huwezi tawala kitu ambacho kimekuzidi Akili hiyo haiwezekani na haitakuja kutokea.

Elewa kuwa wewe unaakili nyembamba au ndogo ndio maana unatawaliwa, na ndio maana wewe sio mtawala. Ingawaje unaweza na unaruhusiwa kujifariji kuwa umewazidi waliokutawala akili hiyo haibadilishi chochote kuwa wewe kiakili upo Chini.

Kama nitaulizwa ni kwa nini CCM mpaka leo inatawala mpaka leo basi moja kwa moja nitakuambia kuwa CCM inaakili kuliko vyama vingine. Yaani Watu wa ccm(inawezakuwa isiwe wote) wanaakili kuliko vyama vingine.
Haiwezekani kila mpambano na kila uchaguzi CCM ishinde tuu. Hiyo ni kuonyesha kuwa wanaakili kuwashinda wapinzani wao.

Watu wajinga hupenda kutoa visingizio katika kushindwa au pale wanaposhindwa na wenye Akili.
Sijui polisi, sijui wanatumia vyombo vya Dola, sasa kwa nini ninyi msitafute akili ya kupata ushawishi kwenye hivyo vyombo vya Dola kama mnajua kuwa kuna wakati ili mpate ushindi basi vyombo vya dola vinaweza kuwasaidia. AKILI.

Unakuta mtu anajiona anaakili kuliko Boss wake. Mpaka unamshangaa. Hiyo ni dalili ya kuchanganyikiwa. Huwezi kuwa na akili zaidi ya mtu ambaye amekuzidi na amekutawala katika uchumi alafu useme unamzidi akili za uchumi.

Kwenye Vita baina ya Israel na Palestina, watu wajinga na wenye upeo mdogo wanakataa kuwa Israel haina Akili na utawala wake unatokana na Kusaidiwa na Marekani. Yaani kama sio Marekani basi Israel haiiwezi Palestina na Waarabu. Unakuja kugundua kuwa wanaosema hivyo upeo wao upo chini katika kuyachambua mambo.

Hawajiulizi mbona Ukraine inasaidiwa na Marekani, na nchi za Nato lakini Inashindwa mbele ya Urusi. Hawajiulizi hivyo kwa sababu hawajui kuwa Akili ndogo haiwezi kuishinda akili kubwa.
Urusi ni akili kubwa hivyo inapokutana na Ukraine hapo ni lazima Ukraine ashindwe tuu bila kujali huyo Ukraine atasaidiwa na Marekani au Nato.

Wewe kama unajua ili ushinde unatakiwa ufanye moja mbili tatu. Kwa nini usifanye hizo moja mbili tatu.
Mshindani wako akikushinda unaleta visingizio.
Ooooh! Fulani kaenda kwa waganga wa kienyeji, sijui anauza madawa ya kulevya, ndio maana anapesa, pesa za wizi zile.
Hivi kwa ujinga wako unafikiri hata huo Wizi au kuuza madawa ya kulevya hakuhitaji AKILI?

Nenda nawe ukauze au kaibe ili ujue huyo mwenzako amekuzidi Akili na atakutawala kwa ufinyu wa akili yako.

Elewa kuwa Akili ni akili tuu. Bila kujali ni Akili ya uadilifu au akili ya uhalifu. Kutawaliwa ni kutawaliwa tuu iwe unatawaliwa kwa Haki au kwa haramu.

Jambo moja nalotaka kusema ni kuwa, ukishindwa kubali umeshindwa, kukubali kushindwa ni mwanzo wa kujitambua na unaweza kujua wapi pakuanzia.
Lakini kujifanya unauwezo wakati uwezo huo huna na kama ungekuwa nao usingeshindwa ni dalili ya kutojitambua.

Mimi nimemaliza,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Upo sahih

Mbowe ametuzid akili
 
L
Sidhani kama siasa za kimataifa na historia yake unazielewa vizuri hapa tutakesha.

Ila nikukumbushe civilization duniani haijaanzia ulaya na suala la kutawala watu kimabavu sio level of intelligence.

Wapi nimesema Civilization imeanzia Ulaya?

Hiyo Historia ya mataifa ni ileile tuu. Huwezi kuwa na Superpower Wawili Kwa wakati mmoja. Hiyo haipo na haitakuja kutokea.

Akili inaweza kufanya kazi kwa njia rahisi au njia ya mabavu. Kitakachoangaliwa zaidi ni matokeo kuwa yataleta tija tuu.
 
Huwezi tenganisha Akili na utawala.
Uwezo wa kujitawala unaenda sambamba na uwezo wa akili.
Uwezo wa kutawala Watu na kutawala mazingira unaenda sambamba na Akili.

Ukiona unashindwa kujitawala an kutawala mazingira yake hiyo ndio tafsiri ya kuambiwa unaupeo mdogo sana wa Akili.
CCM vs CHADEMA
 
Umeandika mwngi yenye uelekeo wa ukweli Ila sio lazima iwe kweli..ni uelekeo tu .
Ni sawa' na bati ambalo halijapigiliwa vizuri upepo ukivuma nilipiga kelele Sana kama linang'oka kumbe lipo tu na upepo ukitulia nalo linatulia.
Hiyo Ni kichwa yako' huo' unatumia ndumu au bangi ..ukivuta unachangamka kweli..utandika wee Ila Moshi ukitulia na ww una tulia.
I know what I'm saying

Wewe ndio umeandika haya lazima ujue ulichoandika, unajaribu kueleza unajielewa zaidi lakini unashindwa kuelewesha wasomaji wako.
Karibu Sana Mkuu
 
Wacha nikukumbushe kitu hiki kitakusaidia.

Ancient China ndio wagunduzi wa gunpowder lakini hawakutumia kuunda bunduki nyingi na kuanza kupora maeneo ya watu hovyo duniani ila baada ya wazungu kuipata hiyo teknolojia toka China angalia walivyo anza mabavu ya utumwa na kupora maeneo ya watu hovyo na kuwakoloni.

Hii itakusaidia kujua mabavu, kutawaliana na akili nyingi havina mahusiano
 
Akili ndio sifa namba moja na nguzo ya kutawala chochote kile.
Hata kwenye ndoa unaambiwa ishi kwa akili na mkeo kwani bila hivyo huwezi kumtawala.

Vigezo vingine ni Minors

Mimi binafsi naona hekima ndiyo kitu cha kwanza, akili ni ujuzi ambao karibu kila mtu anao, lakini hekima ni namna bora ya kutumia maarifa au akili. Kwa hiyo unaweza kuwa na akili (maarifa) lakini usiwe na hekima, hilo likapelekea kuwa na majanga. Hata mfalme Sulemani mwenye hekima, alivyoambiwa na Mwenyezi Mungu achague kitu kitakachomsaidia kutawala Israeli aliomba hekima. Hekima ndiyo kila kitu.
 
Wacha nikukumbushe kitu hiki kitakusaidia.

Ancient China ndio wagunduzi wa gunpowder lakini hawakutumia kuunda bunduki nyingi na kuanza kupora maeneo ya watu hovyo duniani ila baada ya wazungu kuipata hiyo teknolojia toka China angalia walivyo anza mabavu ya utumwa na kupora maeneo ya watu hovyo na kuwakoloni.

Hii itakusaidia kujua mabavu, kutawaliana na akili nyingi havina mahusiano

Waligundua mwaka gani?
Nani aliyegundua?
Nini kilipelekea ugunduzi huo?
 
Mimi binafsi naona hekima ndiyo kitu cha kwanza, akili ni ujuzi ambao karibu kila mtu anao, lakini hekima ni namna bora ya kutumia maarifa au akili. Kwa hiyo unaweza kuwa na akili (maarifa) lakini usiwe na hekima, hilo likapelekea kuwa na majanga. Hata mfalme Sulemani mwenye hekima, alivyoambiwa na Mwenyezi Mungu achague kitu kitakachomsaidia kutawala Israeli aliomba hekima. Hekima ndiyo kila kitu.

Hekima ni level ya juu ya Akili.
 
Wacha nikukumbushe kitu hiki kitakusaidia.

Ancient China ndio wagunduzi wa gunpowder lakini hawakutumia kuunda bunduki nyingi na kuanza kupora maeneo ya watu hovyo duniani ila baada ya wazungu kuipata hiyo teknolojia toka China angalia walivyo anza mabavu ya utumwa na kupora maeneo ya watu hovyo na kuwakoloni.

Hii itakusaidia kujua mabavu, kutawaliana na akili nyingi havina mahusiano

Kati ya hao wawili, Wachina walikuwa na akili (ujuzi) wa kutengeneza gunpowder, lakini pia walikuwa na hekima (namna bora ya kutumia ujuzi/akili) katika matumizi ya huo ujuzi wao.
Wazungu kwa upande wao, walikuwa na ujuzi (ambao waliutoa kwa waChina) wa kutengeneza bunduki, lakini hawakuwa na hekima ya kutumia, ndiyo maana wakatumia ujuzi huo katika robbery and plundering.
 
Utawala unahusisha akili kubwa zaidi ya kudili na watu, kuwadhibiti na kuwaongoza wafanye yale unayotaka.
 
Back
Top Bottom