Anayekutawala amekuzidi Akili

Anayekutawala amekuzidi Akili

Hata wewe unawezakuwa na akili kwa level ya familia yenu. Halikadhalika na Mimi.
Huyo China anaweza kuwa na akili kwa level ya jamii zao(Wachina, Wajapan, Wakorea) na ukanda wa Mashariki ya mbali . Lakini tukizungumzia Ulimwenguni hapo tunazungumzia habari nyingine kabisa.

Ni sawa useme Chadema inanguvu kisa umeenda Moshi au Arusha. Kitaifa Watu watakushangaa.

Hao Wachina hawana Rekodi yoyote ya maana katika mambo ya Akili na utawala ulimwenguni.
Labda kama unazungumzia habari za Future ambazo kwa sasa hazina maana yoyote.
Na hapa ndipo tatizo lilipo unadhani dunia imeanza baada ya western Civilization.

Unafahamu kuhusu misri ?
Unafahamu kuhusu uajemi ?
Unafahamu kuhusu waarabu ?
Unafahamu kuhusu wahindi ?
Unafahamu kuhusu wachina ?

Hayo maswali yakatakusaidia
 
Na hapa ndipo tatizo lilipo unadhani dunia imeanza baada ya western Civilization.

Unafahamu kuhusu misri ?
Unafahamu kuhusu uajemi ?
Unafahamu kuhusu waarabu ?
Unafahamu kuhusu wahindi ?
Unafahamu kuhusu wachina ?

Hayo maswali yakatakusaidia

Nafahamu kuhusu Misri, uajemi, umedi(kurdi), Ashuru (Syria) , Uyunani (Ugiriki), Warumi, Dola la Ottoman, kisha na hawa Wazungu.
Wahindi na wachina sijawahi kusikia popote waliwahi kutawala Dunia.

Labda utoe elimu mpya hapa
 
Nafahamu kuhusu Misri, uajemi, umedi(kurudi), Ashuru (Syria) , Uyunani (Ushiriki), Warumi, Dola la Ottoman, kisha na hawa Wazungu.
Wahindi na wachina sijawahi kusikia popote waliwahi kutawala Dunia.

Labda utoe elimu mpya hapa
Umeona sasa kwako wewe akili nyingi unaitanabaisha kwa kupora maeneo na kubana watu vifungoni.

Wacha nikuulize tena linalo endana na hali ya sasa.

Toka U.S.A imekuwa super power wa duniani ni vita ngapi na maeneo mangapi imepora na kukalia kimabavu ? Na toka China imekuwa super power ni vita ngapi imewahi iona ikiwapiga watu na kuwavamia kimabavu kama marekani ?
 
Umeona sasa kwako wewe akili nyingi unaitanabaisha kwa kupora maeneo na kubana watu vifungoni.

Wacha nikuulize tena linalo endana na hali ya sasa.

Toka U.S.A imekuwa super power wa duniani ni vita ngapi na maeneo mangapi imepora na kukalia kimabavu ? Na toka China imekuwa super power ni vita ngapi imewahi iona ikiwapiga watu na kuwavamia kimabavu kama marekani ?

USA inatawala mpaka China.
Ndio maana ya kuitwa Superpower.
China haijawahi kuwa Superpower, ndio maana hata eneo la Taiwan ambalo ni eneo lake inahangaika nalo.
Hivi unajua maana ya Superpower?
 
ANAYEKUTAWALA AMEKUZIDI AKILI

Anaandika, Robert Heriel.
Mtibeli.

Ukiona mtu amekuzidi na kukutawala kisiasa, kiuchumi, kijamii au kiteknolojia basi fahamu kabisa mtu au jamii hiyo imekuzidi Akili.

Akili ndio inayotawala mambo yote duniani. Ili upewe Mamlaka na nguvu basi lazima uwe na akili kuwashinda wengine hasa hao unaowatawala.

Kijinsia, Mwanaume anaakili kuliko Mwanamke ndio maana anamtawala. Ingawaje zipo siasa na porojo za kuwafariji wanawake kuwa wanaakili kuwashinda wanaume lakini kiuhalisia Mwanaume anaakili zaidi kuliko Mwanamke. Ndio maana Mwanaume anamtawala Mwanamke.

Kijamii, Wazungu na jamii zao wanaakili kushinda Waafrika, na Waarabu na wachina na jamii zingine. Ndio maana wazungu miaka nenda rudi wanatawala huu ulimwengu.

Kuna ile kujidanganya kuwa utawala ni majaliwa lakini hata hiyo akili yenyewe ni Majaliwa. Kila kitu kwenye maisha ni Majaliwa.

Wanyama wa porini tunawatawala kwa sababu ya sisi kuwashinda kiakili.
Huwezi tawala kitu ambacho kimekuzidi Akili hiyo haiwezekani na haitakuja kutokea.

Elewa kuwa wewe unaakili nyembamba au ndogo ndio maana unatawaliwa, na ndio maana wewe sio mtawala. Ingawaje unaweza na unaruhusiwa kujifariji kuwa umewazidi waliokutawala akili hiyo haibadilishi chochote kuwa wewe kiakili upo Chini.

Kama nitaulizwa ni kwa nini CCM mpaka leo inatawala mpaka leo basi moja kwa moja nitakuambia kuwa CCM inaakili kuliko vyama vingine. Yaani Watu wa ccm(inawezakuwa isiwe wote) wanaakili kuliko vyama vingine.
Haiwezekani kila mpambano na kila uchaguzi CCM ishinde tuu. Hiyo ni kuonyesha kuwa wanaakili kuwashinda wapinzani wao.

Watu wajinga hupenda kutoa visingizio katika kushindwa au pale wanaposhindwa na wenye Akili.
Sijui polisi, sijui wanatumia vyombo vya Dola, sasa kwa nini ninyi msitafute akili ya kupata ushawishi kwenye hivyo vyombo vya Dola kama mnajua kuwa kuna wakati ili mpate ushindi basi vyombo vya dola vinaweza kuwasaidia. AKILI.

Unakuta mtu anajiona anaakili kuliko Boss wake. Mpaka unamshangaa. Hiyo ni dalili ya kuchanganyikiwa. Huwezi kuwa na akili zaidi ya mtu ambaye amekuzidi na amekutawala katika uchumi alafu useme unamzidi akili za uchumi.

Kwenye Vita baina ya Israel na Palestina, watu wajinga na wenye upeo mdogo wanakataa kuwa Israel haina Akili na utawala wake unatokana na Kusaidiwa na Marekani. Yaani kama sio Marekani basi Israel haiiwezi Palestina na Waarabu. Unakuja kugundua kuwa wanaosema hivyo upeo wao upo chini katika kuyachambua mambo.

Hawajiulizi mbona Ukraine inasaidiwa na Marekani, na nchi za Nato lakini Inashindwa mbele ya Urusi. Hawajiulizi hivyo kwa sababu hawajui kuwa Akili ndogo haiwezi kuishinda akili kubwa.
Urusi ni akili kubwa hivyo inapokutana na Ukraine hapo ni lazima Ukraine ashindwe tuu bila kujali huyo Ukraine atasaidiwa na Marekani au Nato.

Wewe kama unajua ili ushinde unatakiwa ufanye moja mbili tatu. Kwa nini usifanye hizo moja mbili tatu.
Mshindani wako akikushinda unaleta visingizio.
Ooooh! Fulani kaenda kwa waganga wa kienyeji, sijui anauza madawa ya kulevya, ndio maana anapesa, pesa za wizi zile.
Hivi kwa ujinga wako unafikiri hata huo Wizi au kuuza madawa ya kulevya hakuhitaji AKILI?

Nenda nawe ukauze au kaibe ili ujue huyo mwenzako amekuzidi Akili na atakutawala kwa ufinyu wa akili yako.

Elewa kuwa Akili ni akili tuu. Bila kujali ni Akili ya uadilifu au akili ya uhalifu. Kutawaliwa ni kutawaliwa tuu iwe unatawaliwa kwa Haki au kwa haramu.

Jambo moja nalotaka kusema ni kuwa, ukishindwa kubali umeshindwa, kukubali kushindwa ni mwanzo wa kujitambua na unaweza kujua wapi pakuanzia.
Lakini kujifanya unauwezo wakati uwezo huo huna na kama ungekuwa nao usingeshindwa ni dalili ya kutojitambua.

Mimi nimemaliza,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kutawala ni utashi, akilini ni tunu.
Wanazuoni wengi ulimwenguni hawakauwa watawala, lakini watawala wengi waliwatumia wanazuoni katika kutawala.
 
USA inatawala mpaka China.
Ndio maana ya kuitwa Superpower.
China haijawahi kuwa Superpower, ndio maana hata eneo la Taiwan ambalo ni eneo lake inahangaika nalo.
Hivi unajua maana ya Superpower?
Sasa unazidi kuchanganya mambo U.S.A anaitawala China ki vipi ?

Suala la Taiwan sifikiri kama unalielewa.

Wewe nisaidie maana ya superpower nisiyo elewa mimi karibu ?

Pia nikukumbushe swali langu la vita kati ya U.S.A na China hujajibu bado
 
Sasa unazidi kuchanganya mambo U.S.A anaitawala China ki vipi ?

Suala la Taiwan sifikiri kama unalielewa.

Wewe nisaidie maana ya superpower nisiyo elewa mimi karibu ?

Pia nikukumbushe swali langu la vita kati ya U.S.A na China hujajibu bado

Superpower hawawezi kuwa Wawili katika ulí mmoja na zama moja. USA sasa hivi ndio Superpower ndiye anayetawala Dunia ikiwemo hao wachina.
 
Back
Top Bottom