Anayejua makweme na makilaume aje hapa

Anayejua makweme na makilaume aje hapa

makilaume nimekula sana na hadi leo yapo mengi kuzunguka nyumba yetu kijijini. makwembe yapo rundo, yanaota kwa kutambaa juu ya mti afu bonge la boga kubwa linazaa, ukipasua ndio hizo kwembe, nimekula san akwa kuzichoma unapasua. udogoni tulikuwa tunazitwanga kwembe na kuweka kwenye mboga, na hata nikienda leo kijijini napenda mboga ya majani ikiwekwa kweme. hayo makilaume yakiwa machanga, ukayamenya na kuunga kwa karanga au kweme au na mafuta kama mboga tu, ilikuwa ni alternative ya mboga kama haujapata msosi na unataka msosi wa haraka.
Good for health, wapi kwenu nitembelee, npo lake zone sasa
 
Ase mkuu tutumie picha ya mimea ukiweza. Asante
images.jpeg
 
Nayajua yote hayo nshafika, picha zake naweza leta baadae.

Hizo hapo picha nishazipata. ......

View attachment 669102
Hizo ni kweme.

View attachment 669103
Hayo ni matunda damu.

Ever Smiling Kasie.
Ahsante kwa picha la sivyo nisingeyajua. Nilpokuwa Moshi yote hayo niliyaona ila kweme sikujua kazi yake nilihisi ni chakula cha kuku kuwa kinasagwa na kuwa kama mashudu ya alzeti kisha wanapewa kuku.
 
hata mimi sijui yanazaliwaje, ila mkuu mshana jr na KikulachoChako nahisi wanajua
Hata mimi sijui huwa yanazaliwaje kwa kuwa sijawahi kuyaona mtini wala ardhini

Aisee nimekumbuka mbali maana hayo makweme bibi alikuwa anayaunguza na moto alafu anatoa kiini cha ndani na kukitwanga alafu ule unga wake anauweka kwenye maziwa ya mtindi na kachumvi kwa mbali......yaani unaweza ukajikuta unamaliza kilo moja peke yako......huku pembeni upo na kibakuli cha msele( mthele).......

Nimekumbuka mbali sana......
 
Makila - yanaleta ladha fulani kwenye mboga hasa za majani.
Mchuzi hata ukiwa mwepesi na kilaume unakata 'sima' ya ugali. Sometimes ukila wali/ makande na unahisi hakuna ladha basi unaling'ata kidogo kila ukiweka kijiko cha chakula mdomoni unanyonya ' kakila'

Makweme/makungu- unaweka kwenye mboga kama karanga, unayachoma unasaga then unachanganya na maziwa mgando unakula ugali (nzuri hii kwa afya)
Makweme- huwekwa pia kwenye ndizi kama nazi,
MZAZI ALIYEJIFUNGUA - Mboga zake baada ya kutenga supu huchemshwa muda mrefu na makweme hakika hurekebisha tumbo, mafuta ya asili, ni mboga tamu na nzito n.k
Umenitamanishaaaz ugal wa msele home
 
Ahsante kwa picha la sivyo nisingeyajua. Nilpokuwa Moshi yote hayo niliyaona ila kweme sikujua kazi yake nilihisi ni chakula cha kuku kuwa kinasagwa na kuwa kama mashudu ya alzeti kisha wanapewa kuku.
Ni msosi mkuu
 
Hata mimi sijui huwa yanazaliwaje kwa kuwa sijawahi kuyaona mtini wala ardhini

Aisee nimekumbuka mbali maana hayo makweme bibi alikuwa anayaunguza na moto alafu anatoa kiini cha ndani na kukitwanga alafu ule unga wake anauweka kwenye maziwa ya mtindi na kachumvi kwa mbali......yaani unaweza ukajikuta unamaliza kilo moja peke yako......huku pembeni upo na kibakuli cha msele( mthele).......

Nimekumbuka mbali sana......
[emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39]
 
Oh yes, makweme hayo umepatia ila makilaume bado, hata hayo wanaita matunda damu.
Makweme nayajua....

Na hayo mengine Ninayafahamu yanaitwa matungusha... Unaweza kula hivyohivyo ila ni machachu sana!

Huku njombe pia nimeyaona.... Nahisi yanastawi sana sehemu za baridi....

Ningekuwa naweza kuyachora ningeyachora ila siwezi na sina picha.
 
Nayajua yote hayo nshafika, picha zake naweza leta baadae.

Hizo hapo picha nishazipata. ......

View attachment 669102
Hizo ni kweme.

Ever Smiling Kasie.
Kweme sijaziona Kwa Miaka Mingi sana ni Tamu ukizitupia Motoni haswa ule wa Kuni na mafiga kisha unaziipua unazipasua unakula ya kiradha furani kama karanga safi sana Sijui naweza zipataje nipo huku Kwedukwazu
 
Agiza Lushoto mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom