Anayedaiwa kwamba cheti chake ndio anatumia Makonda afunguka

Anayedaiwa kwamba cheti chake ndio anatumia Makonda afunguka

kwani huyo pier christian kagenzi kwani c apige picha gamba zake za secondar tu panapolalamikiwa avimwage jamvini tuvione vyake kwanza harafu vya makonda baadae

Maana hapa kuna tatizo asije kuwa katengenezwa kumtetea mheshimiwa
 
hahaha mmeshikwa pabaya. utetezi mufirsi kabisa aweke attachments hapa
 
CHETI siku hizi ni NAMBA tu. HATUTAKI MANENO YA KWENYE KANGA. Hatuna haja na Majina yenu.
Ww no yako tutaipata na ya BASHITE tutaipata. Baada ya hapo tutakuweka CELLO na HUYO BASHITE wako. Huu ni uhujumu uchumi. UMEKULA mishahara isiyo halali YAKO!! UMEDANGANYA TAIFA.

Mm nimeumwa na MBU kibao pale ADVANCE afu ww mwenye ZIRO uje uniongoze??
 
kagenzi aweke vyeti vyake kwanza tuvione au naye ni kilaza? Maana mko wengi sana utawala huu mtakimbia na kuisha wote
 
Halafu tutaagalia uraia wako, japo jina pierre ni peter ila kwa tanzania haitumiki ukizingatia ni jina la kifaransa . Hilo jina linatumika kwa nchi za zinazoongea kifaransa na ubelgiji ,wewe utakuwa mhamiaji haramu.
 
Makonda kaza hapo hapo bado kidogo wakimbie nchi. Umewashika babaya mno kila mtu Amalia hajui afanye nini. Kumbe nchi ilikuwa imeshikwa hivi na wauza unga. Ndiyo mana pinda aliwahi kusema ukiwagusa nchi itayumba. Makonda big up nchi nzima imepagawa kwani wote wanahamia upinzani sasa nakushauri uwafate hukohuko ulisema hakuna jiwe litakalosalia huu ya jiwe.

Usitishwe na kelele hizi za akina mbowe na henge lake soon watapotea.
Mutu ya Congo
 
SAKATA LA VYETI.

Yule Bwana nayedaiwa kwamba cheti chake ndio anatumia Makonda anaeleza.

“Paul Makonda nimemfahamu kupitia habari, na hata jina wanavyolitaja waliotunga taarifa ya mtandaoni wanakosea.... kwani mimi naitwa PAUL PIERRE CHRISTIAN KAGEZI, hatuna uhusiano na makonda, mimi Muhaya na yeye ni Msukuma.”

Kuna watu wanaoanisha majina pasipo kufanya utafiti wa kutosha, hawa wangeuliza kwanza kabla ya kutoa na kusambaza taarifa kwenye mitandao.

“Taarifa hizo (za kumpa cheti Makonda) si za kweli kwa sababu huwezi kutoa cheti wakati umepata daraja la kwanza kidato cha sita, utakwenda vipi chuo kikuu? Sasa niliwezaje mimi kwenda chuo kikuu halafu kwa wakati huo nimpe naye aende chuo kikuu kwa cheti hicho hicho?

katika kidato cha tano na sita nilichukua mchepuo wa sayansi masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), hivyo si rahisi kutoa cheti hicho kwani ningeshindwa kumudu huko nilikokwenda.

Hivi kama Makonda hakufanya vema kidato cha nne au hakusoma kidato cha sita, akatumia cheti cha mtu mwingine, angeweza vipi kufanya vema katika mitihani yake ya chuo kikuu?

Watu wamekuwa wakipika na kuoanisha majina,....Kama wanataka kumpata huyo bwanamdogo (Makonda) kwa njia hiyo wamemkosa kwani kutumia cheti kimoja kwa vyuo viwili vya Serikali ni jambo lisilowezekana.... Makonda asingeweza kutumia cheti nilichokuwa nakitumia mimi.

“Sera ya Serikali ni kwamba unapata asilimia 100 ya mkopo, inakuwaje mtu huyo nimpe cheti changu wakati huo naye anakwenda chuo kikuu ambacho nacho ni cha Serikali?”

“Huyo bwana anajitegemea yeye kama yeye, na walichokifanya wao (waliosambaza taarifa mtandaoni) kwa makusudi yao bila shaka wana lengo lao, wao wametaka kuingiza hoja ambazo hazina mashiko.

“Cheti cha daraja la kwanza unauza kwa gharama gani? Nimesoma shule ya msingi na sekondari, (Makonda) alikuwa na fedha kiasi gani za kunipa ili nimuachie cheti? Inaweza kukuingia akilini kweli?.. hata hiyo namba ya Makonda sina".
Nyie ndo wale wote mnaotumwa na kutumika..poor u
 
Hii habari inakoelekea ni kubaya zaidi. hadithi itakuwa sio kwamba Daudi Bashite kauziwa cheti na Paulo Makonda bali ni kuwa Daudi Bashite kaiba cheti cha Paulo Makonda na kukitumia bila ya Paulo (original) kutambua kuwa cheti chake kinatumika eneo jingine.
Paulo (original) anaicheza picha hii kwa ufanisi ili Daudi Bashite aucheze muziki huu mwenyewe.
 
SAKATA LA VYETI.

Yule Bwana nayedaiwa kwamba cheti chake ndio anatumia Makonda anaeleza.

“Paul Makonda nimemfahamu kupitia habari, na hata jina wanavyolitaja waliotunga taarifa ya mtandaoni wanakosea.... kwani mimi naitwa PAUL PIERRE CHRISTIAN KAGEZI, hatuna uhusiano na makonda, mimi Muhaya na yeye ni Msukuma.”

Kuna watu wanaoanisha majina pasipo kufanya utafiti wa kutosha, hawa wangeuliza kwanza kabla ya kutoa na kusambaza taarifa kwenye mitandao.

“Taarifa hizo (za kumpa cheti Makonda) si za kweli kwa sababu huwezi kutoa cheti wakati umepata daraja la kwanza kidato cha sita, utakwenda vipi chuo kikuu? Sasa niliwezaje mimi kwenda chuo kikuu halafu kwa wakati huo nimpe naye aende chuo kikuu kwa cheti hicho hicho?

katika kidato cha tano na sita nilichukua mchepuo wa sayansi masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), hivyo si rahisi kutoa cheti hicho kwani ningeshindwa kumudu huko nilikokwenda.

Hivi kama Makonda hakufanya vema kidato cha nne au hakusoma kidato cha sita, akatumia cheti cha mtu mwingine, angeweza vipi kufanya vema katika mitihani yake ya chuo kikuu?

Watu wamekuwa wakipika na kuoanisha majina,....Kama wanataka kumpata huyo bwanamdogo (Makonda) kwa njia hiyo wamemkosa kwani kutumia cheti kimoja kwa vyuo viwili vya Serikali ni jambo lisilowezekana.... Makonda asingeweza kutumia cheti nilichokuwa nakitumia mimi.

“Sera ya Serikali ni kwamba unapata asilimia 100 ya mkopo, inakuwaje mtu huyo nimpe cheti changu wakati huo naye anakwenda chuo kikuu ambacho nacho ni cha Serikali?”

“Huyo bwana anajitegemea yeye kama yeye, na walichokifanya wao (waliosambaza taarifa mtandaoni) kwa makusudi yao bila shaka wana lengo lao, wao wametaka kuingiza hoja ambazo hazina mashiko.

“Cheti cha daraja la kwanza unauza kwa gharama gani? Nimesoma shule ya msingi na sekondari, (Makonda) alikuwa na fedha kiasi gani za kunipa ili nimuachie cheti? Inaweza kukuingia akilini kweli?.. hata hiyo namba ya Makonda sina".


Hahaha atakuwa aligawa marinda sio lazima atoe hela....
 
Ukimya wa Makonda katika suala la cheti akifungua kinywa chake litaumbua watu wengi sana.

Bahati mbaya hakuna mtu aliyejisumbua kufanya utafiti kubaini ukweli. Hakuna waandishi wa habari za uchunguzi waliojitokeza kufanya utafiti wao.

Makonda ni kijana wa juzi tu hapa inawashinda nini kwenda Nyamagana alipozaliwa na kufanya upelelezi wenu kuanzia shule aliposoma shule ya msingi na sekondari mtapata ukweli.

Kwani Makonda kasomea mbingu nyingine? Si hapahapa duniani? Iweje mshindwe kwenda huko kuhoji walimu wake? Wanafunzi aliosoma nao na kuja na uthibitisho uliojawa na tafiti?

Hili suala linakuzwa na wauza dawa za kulevya na vibaraka wao...bahati mbaya ktk kipindi ambacho vita ya dawa za kulevya imeshika kasi.

Watanzania tumekuwa watu wa kujadili mapokeo ambayo hatuyatathmini na kubaini ukweli....leo JF imekuwa jukwaa la mapokeo na kujadili bila hata kufanya utafiti. Ni aibu.

Ukiona watu wazima wanajadili jambo dogo ambalo wanaweza kupata majibu kirahisi jua nia ni nyingine ama kumchafua mtu au kuzuia vita dhidi ya dawa za kulevya isiendelee.

Nimwambie kijana mwenzangu Makonda awaache waonge weeee halafu badae kabisa ambapo watu wabaya dhidi yake wameishajipambanua awajibu. Najua majibu anayo ila hataki kuingia kwenye njadala huo sasa kwakuwa nia yake ya mjadala huu sio njema na haina tija kwa taifa. Chadema na vibaraka wenu mtaumbuka sana....kuweni na akiba ya maneno

Mchungaji Gwajima kasema anazo mpaka nakala za vyeti na anaelewa mpaka shule ya msingi aliyosoma.
 
Kwanini Makonda mwenyewe asijitokeze kukanusha, pia Makonda waTbr na Makonda wa Dar, wote muambatanishe vyeti vyenu tuvione? mbona kesi ndogo sana hii, kuliko kutokwa na povu jingi.
 
Propaganda at work, atoe vyeti vyake tuvione na si kuna watu walianza nae shule anaogopa nini ? Mmh shule ya msingi Daudi ghafla Paul, wonders shall never end
Hili sakata linamfanya mtu akose usingizi, ingawa ana ulinzi wa kufa mtu
 
Mbona rahisi tu, Acheni maneno mingi, leta vyeti baaaasi., hapo utawaziba mdomo wote the so called haters.
 
Back
Top Bottom