Nilufer
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 9,566
- 13,541
SAKATA LA VYETI.
Yule Bwana nayedaiwa kwamba cheti chake ndio anatumia Makonda anaeleza.
“Paul Makonda nimemfahamu kupitia habari, na hata jina wanavyolitaja waliotunga taarifa ya mtandaoni wanakosea.... kwani mimi naitwa PAUL PIERRE CHRISTIAN KAGEZI, hatuna uhusiano na makonda, mimi Muhaya na yeye ni Msukuma.”
Kuna watu wanaoanisha majina pasipo kufanya utafiti wa kutosha, hawa wangeuliza kwanza kabla ya kutoa na kusambaza taarifa kwenye mitandao.
“Taarifa hizo (za kumpa cheti Makonda) si za kweli kwa sababu huwezi kutoa cheti wakati umepata daraja la kwanza kidato cha sita, utakwenda vipi chuo kikuu? Sasa niliwezaje mimi kwenda chuo kikuu halafu kwa wakati huo nimpe naye aende chuo kikuu kwa cheti hicho hicho?
katika kidato cha tano na sita nilichukua mchepuo wa sayansi masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), hivyo si rahisi kutoa cheti hicho kwani ningeshindwa kumudu huko nilikokwenda.
Hivi kama Makonda hakufanya vema kidato cha nne au hakusoma kidato cha sita, akatumia cheti cha mtu mwingine, angeweza vipi kufanya vema katika mitihani yake ya chuo kikuu?
Watu wamekuwa wakipika na kuoanisha majina,....Kama wanataka kumpata huyo bwanamdogo (Makonda) kwa njia hiyo wamemkosa kwani kutumia cheti kimoja kwa vyuo viwili vya Serikali ni jambo lisilowezekana.... Makonda asingeweza kutumia cheti nilichokuwa nakitumia mimi.
“Sera ya Serikali ni kwamba unapata asilimia 100 ya mkopo, inakuwaje mtu huyo nimpe cheti changu wakati huo naye anakwenda chuo kikuu ambacho nacho ni cha Serikali?”
“Huyo bwana anajitegemea yeye kama yeye, na walichokifanya wao (waliosambaza taarifa mtandaoni) kwa makusudi yao bila shaka wana lengo lao, wao wametaka kuingiza hoja ambazo hazina mashiko.
“Cheti cha daraja la kwanza unauza kwa gharama gani? Nimesoma shule ya msingi na sekondari, (Makonda) alikuwa na fedha kiasi gani za kunipa ili nimuachie cheti? Inaweza kukuingia akilini kweli?.. hata hiyo namba ya Makonda sina".