Anataka to-do, But No Love Relationship!!

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,423
29,084
Hello Wanabodi,

Kuna mdada mmoja ambae amekua rafiki yangu kwa muda mrefu sana. Huyu dada tumekua tukifanya biashara mbalimbali za hapohapo (deals) pamoja kwa muda mrefu tu.

Ni kawaida nikiwa na deal namuita chemba labda guest, bar, hotel, kwake, kwangu, beach n.k tunaongea, nae hivyohivyo, tuko kifedha tu. Pia anaweza akawa ama shida ya Tshs kadhaa nikamkopa, nami pia hivyo. Anamjua Gf wangu, nami namjua Mumewe. Sijawahi kum-feel kimapenzi (sijui upande wake)

Sasa jana akaniita chemba (hotelini) tuongee kwani kuna issue/biashara anataka anipe. Kukutana nae zikaanza story za hapa na pale, huku tukijaribu kukumbushiana biashara zilizopita zilivyofanikiwa na nyingine zilivyofeli.

Story zilikua nyingi sana huku akikawia kwenda kwenye point (sio kawaida).

Baadae ndio akadai eti mumewe kasafiri mwezi wa pili sasa hivyo haja-do muda mrefu na anaskia SANA hamu. Alidai yuko serious na nichukulie kama namsaidia tu kama rafiki. Nilimuuliza kama ana feelings zozote za Mapenzi kwangu akadai ananichukulia kama kaka tu ma mshirika wake wa karibu. Aliniambia nisimuangushe, na ananipa Jana mpaka leo kujiandaa, but leo jioni KUSAIDIANA TIME!!

Nimemuuliza hatanogewa akataka tena, na mumewe akijua itakuaje akajibu nichukulie kama ni ombi la kawaida tu kama mengine ya kusaidiana kifedha. Hivyo ya mumewe nimuachie mwenyewe.

Wanabodi,
Leo jioni ndio time, mdada ni best yangu sana, tuseme tunawekana mjini kwa Biashara tufanyazo,

Ushauri wenu.
1) Nikamsaidie shida yake??
2) Ku-do bila kua kwenye mahusiano kuna ladha gani??
3) Any other ushauri!!
 
inaonekana u mtu mzima lkn gf wako umefikiria unamtendea haki??coz ngono c kitu km fedha mnazopeana unaweza kufanya nae na ikakuathiri na ht kuathiri dili zenu kabisa;mfikirie ulienae na thamani yake na ww co chombo cha starehe ova n out
 
Ushauri wangu, mwambie awe mvumilivu mpaka mumewe arudi tu kwani sio lazima kila anayekuvutia kimapenzi ufanye naye lazima kujitawala (self control). Mbanie kwenye point aliyesema anakuchukulia kama kaka yake na wewe sisitiza kwamba huna hisia zozote isipokuwa za dada tu na unafeel gilty hata kuwazia hilo tendo kulifanya naye. Atakuelewa tu. Kama unamwamini Mungu aliyehai omba Roho Mtakatifu akusaidia kumlanisha ili aachane na mpango wake wa uzinzi na wewe.
 
Mke wa mtu????Achana nae ndugu yangu,mtaona ni siri lakini hata ipite miaka kumi, lazima mme wake atajua tu.Asikulainishe kwamba suala la mme wake umuachie,lazima akuambie hivyo ili uingie king kutokana na kuzidiwa kwake na tamaa.Asingeweza kukuambia kwamba mme wake atajua maana angezidi kuondoa "uhalali" wa anachokifikiria.Lakini uamuzi wa mwisho unao wewe maana ndo uko eneo la tukio.Kazi kwako
 
Hapa kuna maswali meni ya kujiuliza,
1. Iweje vikao vingine vya kibiashara mkutanie guest badala ya maeneo mengine kama hotelini?
2. Umesahau kuwa huyo ni mke wa mtu na attempt yeyote ya kumsaidia maana yake itakuwa unatembea na mke wa mtu?
3. Huoni kwa kumsadia huyo dada utakuwa umemsaliti GF kirahisi?
4. Huoni kuwa kumkubalia huyo dada ni kujidhalilisha (kuwa cheap), anyone anaweza akakutaka tu pale anapojisikia hamu-kwa kifupi huna thamani na huoni thamani juu ya mwili wako?
5. Unayajua madhara ya kufumaniwa?
6. Na mwisho nyie mmekuwa kuku au paka au panya kushiriki tendo la ndoa bila mapenzi?

Na log off!
 
huhitaji ushauri wetu katika hili unless you are seriously considering doing this.otherwise make the right decisions,dont do it.
 
Wewe unaonaje?
Maswali mengine bwana, ni kutaka kujua hisia za watu tu. Uko naye kwa hotel, kakwambia hayo mpaka unaachana haujajua cha kufanya au kutofanya siamini. Be frank sema you did it and you feel bad, bado tutakuelewa tu!

Kuna g/f wangu wa zamani tulipoteana, tulipoonana akanambia wameachana na mume wake na kwa sababu na mimi nilikuwa single wakati huo tukakumbuashia.

Kibaya zaidi baada ya wiki akaniambia wametengana tu kwa muda kwa sababu ya kuingilwa kwenye mahusianao yao na familia ya mume wake.............duh! nilichoka ..............Kifupi bado hawajaachana na wamerudiana. Hapo ndipo alarm yangu juu ya viumbe hawa ikarudi kuwa active!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom