Ukishaamua kuwa mzazi, welfare ya mtoto wako ndo inakuja kwanza kabla ya yako. Mtoto hakukuomba umzae, ni wewe ndo uliamua kumleta; so give your all to that child. Kama mzazi lazima usacrifice
Sio kila ndoto kwenye maisha yetu, tulifanikiwa kuzitimiza, asipoolewa ni sawa tu, maisha yataendelea. Wapo wengi hawajaolewa na hawana hata mtoto na wanaishi na kuenjoy maisha, sembuse yeye atakayekuwa na watoto wake watakaomtia nguvu na kumpa tabasamu anapolia? Na wapo ambao wameolewa na hawana watoto, you can imagine what they are going through.
Nimeshakutana na single parents wengi tu ambao wameamua kuwa hawaoi/kuolewa, watabaki kulea tu watoto wao, kwa sababu hawana uhakika na welfare za watoto wao once wakiingia ndoani. Hata hawa naamini walikuwa na ndoto za ndoa, ila ndo hivyo. Kwenye maisha it's not all about kupata kila unachokitaka, ila ni kuenjoy kile ulichonacho. Afu kuna watu wana kibali cha ndoa, wanaolewa tu hata kama wamezaa watoto ishirini.