Hapa naona kama tayari mimba ishatolewa hivyo nafsi zinawasuta hivyo mnataka angalau mpate huruma ya watu wakiwaambia kilichofanyika ni sahihi.
Kushika mimba nje ya ndoa kiimani(kwa waamini) na hata kwa jamii si sahihi hivyo hivyo kuitoa mimba hiyo haitosahihisha kosa la kwanza la uzinzi. Hiyo mimba ni matokeo ya mchakato mrefu sanaaa, sio ajali. Hivyo kama aliumia kihisia alipaswa kuchukua tahadhari kweli kweli ili hilo lisitokee tena.
(Kama bado ipo) Kwakuwa lishatokea basi awe tu responsible kwa makosa yake na sio kugharimu maisha ya kiumbe kisicho na hatia.
Amwambie muhusika then wao ni watu wazima watajua jinsi ya kuendelea kutokea hapo ila asithubutu kutoa mimba, damu ni nzito itamuandama na anaweza pitia maumivu makali ya kihisia kuliko hayo aloyapata awali.