Anakua? Uaminifu unapungua?

Anakua? Uaminifu unapungua?

hata baba na mama wanaweza raise a grown boy, all parents wishes to raise men.

sisi tulilelewa na mama na baba
watoto wa siku hizi wanalelewa na mom and dad.....big difference if you ask me....
 
Kijana wangu mdogo simwelewi kwa kweli, sijui ni kwamba anakua au haniamini tena. Hayuko muwazi kwangu kama zamani tena, mambo mengine haniambii tena.

Kuna siku alikuwa na kisanga na baba, sikuwepo home. Basi akagombezwa na wakamalizana. Nlivyorudi nikamuuliza ilikuwaje, akanijibu 'mambo mengine yanatakiwa kubaki hapa(huku akijishika kifuani)'. Ndo akamaliza.

Kuna wakati alienda kwa ndugu, nikamwagiza afanye jambo fulani, hakufanya. Nilipo muuliza kasema amesahau, nikamgombeza akaomba samahani yakaisha. Juzi juzi hapa katika maongezi akawa ananiambia asivyopenda kuwa sehemu ya ugomvi. Akanikumbusha hiki kisa na aliyoyakuta ugenini, akaamua kupotezea nilichomtuma. Akaniambia hakusema sababu hakutaka ugomvi.

Usiku huu dada kamuumiza bahati mbaya, nimemuuliza umefanyaje, kanijibu nimejiumiza huko jikoni.

Am troubled kwa kweli, ni nini hiki? Ndio watoto wa kiume mnakuwaga hivyo kwa mama zenu. Ndio mie ni mama mtata, ila ni rafiki wa wanangu. Sijui nakosea wapi, nataka aniambie kila kitu kama zamani. Hajafika hata 10yrs.

He is trying to become 'independent'...thats how men are...you should be proud, you are rising a man!
 
Back
Top Bottom