Anakotupeleka Rais Magufuli ni kuzuri; Serikali itakuwa na uwezo wa kumlipa hela kila asiye na kazi

Wengi hushangaa wakisikia mtu asiye na kazi nchi zilizoendelea kuwa hulipwa posho kila mwezi na serikali

Siri yake ndogo tu ni kuwa miradi mikubwa ya maendeleo mila pesa nyingi kama mabarabara, hospitali, Shule, njia za reli, umeme, maji nk yote ilishaisha kujengwa. Hivyo serikali zingine zikija hazina cha kufanya hivyo kuwa na pesa nyingi zisizo na kazi, hivyo kufanya hicho kiasi cha ziada kitumike kuongeza mishahara na marupurupu ya wafanyakazi na kuwalipa wasio na kazi.

Rais Magufuli anachofanya mbeleni kitakuwa na faida kubwa kwani bajeti ya maendeleo yaweza kupewa pesa kidogo sababu hakuna cha kufanya hivyo excess kwenda kwa wafanyakazi na wasio na ajira.

Kama Taifa kama kila Raisi angejikita miradi ya maendeleo kama Magufuli tungekuwa na pesa sasa hivi nyingi zisizo na kazi.
Inawezekana upo ndotoni
 
Siri ni moja tu . 1 .muachane na ulafi wizi huku hiyo habari ya kuona bila kunawa ishasahailika.
2. Watu wajitume kufanya KAZI nchi zilizoendelea kazi ni kipimo cha Utu

3. Hicho kichwa cha JPM hamkipati in years to come .Kwa sasa hatukioni Ila in reality watu wengi ni vichwa boga
Ni kweli hatukipati kwa sababu hakuna Mtanzania mwingine ambaye Ni mwingi, muuaji, mbaguzi, mropokaji na mwizi Kama JPM
 
Umesahau kuongelea inflow ya pesa zitakazotokana na hiyo miradi kama SGR , Umeme ,Stendi mpya,meli mpya nk analyisis yako iko based to kwenye Outflow haijakaa kisomi imekaa ki layman!!! Infmgekuwa umeandika thesis ya ku graduate degree ningekupa zero

Chuo ulichosoma wajinga walikupaje digrii mjinga kama wewe? walikufundisha kuwa kufanya analyisis unatakiwa u cincentrate kwenye outflo tu bila kuweka inflow ? hopeless kabisa
Kwa iyo buku buku ndio unaita inflow ya pesa ya kulipia trilions zilizokopwa, subiri wachina waje wachukue nchi yao deni halilipiki.
 
Wengi hushangaa wakisikia mtu asiye na kazi nchi zilizoendelea kuwa hulipwa posho kila mwezi na serikali

Siri yake ndogo tu ni kuwa miradi mikubwa ya maendeleo mila pesa nyingi kama mabarabara, hospitali, Shule, njia za reli, umeme, maji nk yote ilishaisha kujengwa. Hivyo serikali zingine zikija hazina cha kufanya hivyo kuwa na pesa nyingi zisizo na kazi, hivyo kufanya hicho kiasi cha ziada kitumike kuongeza mishahara na marupurupu ya wafanyakazi na kuwalipa wasio na kazi.

Rais Magufuli anachofanya mbeleni kitakuwa na faida kubwa kwani bajeti ya maendeleo yaweza kupewa pesa kidogo sababu hakuna cha kufanya hivyo excess kwenda kwa wafanyakazi na wasio na ajira.

Kama Taifa kama kila Raisi angejikita miradi ya maendeleo kama Magufuli tungekuwa na pesa sasa hivi nyingi zisizo na kazi.
Ndoto za vikojozi hizi, unaota umekutana na choo kizuri kina muhudumu wa kukuvuta zip.
......Amka kumekucha utakojoa kwenye godoro na unaona hali ya mvua, godoro halitakauka. Amkaaaaaaa
 
Back
Top Bottom