Heshima mbele wanaMMU
Ninayoiweka hapa ni mada ya ukweli ambayo rafiki yangu aliniletea
tuidisscus..sasa katika kuidiscuss kuna mawazo ambayo nilimpa na of
course kuna mengine ambayo tulishindwa kuafikiana. Lakini kwa sababu
kisima cha JF hakikaukiwi maji nimeona kabla hajafikia uamuzi rasmi basi
niwashirikishe nanyinyi hapa ili nione kama mnaweza kuchangia kitu gani
katika huu mpango mzima!
Iko hivi..Jamaa yangu huyu alishawahi kuwa na rafiki wa kike kama miaka
kumi iliyopita maeneo ya huko Mwanza. Na kama mnavyojua raha ya maisha
kuhangaika, baada ya muda mrefu kila mtu kuwa kwenye mihanjo yake
mawasiliano yalikatika na kila mtu kupata uhusiano mpya. Jamaa yangu
alioa na kwenye ndoa yake kajaaliwa kupata mtoto mmoja, halikadhalika
bibie naye aliolewa na kubahatika kupata mtoto mmoja pia. Kwa kipindi
cha miaka ya karibuni kama miaka mitatu iliyopita marafiki hawa wa
zamani walijikuta wameonana na wakawa wamebadilishana mawasiliano na
wakaanza kuwa wanajuliana hali na vitu kama hivyo. Kwa mujibu wa huyu
jamaa yangu, ilionekana kama mwanamke alikuwa anapenda wakumbushiane na
jamaa yangu kwa mujibu wa alivyoniambia alimwambia waheshimu ndoa zao na
wabaki kuwa 'friends'. Kwa mujibu wa mshkaji, mwanamke aliliafiki kwa
shingo upande tu.
Sasa, tatizo limekuja,Mume wa jamaa alifariki..na mshkaji wangu hajui
kilichomuua japo inasemekana ni 'pressure' na ofcourse ni kama mwaka
mmoja uliopita na jamaa kwa mila na desturi baada ya siku nyingi za
kutokwenda Mwanza alienda kwao na akaamua kwenda kumpa pole huyu mama.
Cha ajabu huyu mama aliipokea pole yake lakini pia akamwambia angependa
azae naye kwa sbb anahisi anahitaji mtoto na hayuko tayari kuolewa tena
coz umri umeenda. Mshkaji wangu anadai alimchomolea, lakini yule mama
alimwambia..'wewe nipe mimba tu hayo ya ulezi niachie mimi'!.
Sasa ili kufupisha habari hapo ndio kesi ilipo..Jamaa alifanikiwa
kuchomoa kwa mara ya kwanza lakini huyu mama kaja hapa Dar na kampata
jamaa na madai yake yamesimama vilevile!!..Naomba ushauri hapa 'Je? ampe
tu hiyo mimba au asepe mazima!!..
NB: Matusi na Kejeli sio kitu cha maana hapa, na kama huna la
kuchangia please ukimbie huu uzi!!