Anachokitafuta RC wa Kagera atakipata

Anachokitafuta RC wa Kagera atakipata

Vita ya Kagera (1978) Ila Kagera bado maskini Vs Rwanda Genocide (1994) Ila Rwanda Leo inapiga hatua kubwa za maendeleo, **punguza visingizio! Wana-Kagera wabinafsi na sifa za kijinga
Umefikiri vizuri ndugu. Serikali ya Rwanda iliamua kuwekeza kutoka hapo ilipokuwa tena kwa jasho na dame. Je serikali ya Tanzania iliamua kuwekeza Kagera? Sana sana walipora hela za tetemeko.

Halafu tofautisha nchi na Mkoa.
Ningekuwa mkazi wa huko hata kukutukana ningekutukana.
 
CHANZO CHA UMASIKINI KAGERA KWA MAWAZO YANGU NI TOFAUTI NA WATAWALA WANAOWAZA KISIASA.

Kinachonisikitisha ni kwamba kila anayepanda jukwaa kuelezea kinachoitwa umaskini wa Mkoa wa Kagera anakuja na ngonjera za wingi wa maprofesa na Ma-PhD holders kutoka mkoani mwetu.

Lawama zote zinarundikwa kwa watu hao na Wanakagera kwa jumla. Huo ndio utawala wetu ambao tumezoea kwa miaka mingi sasa. Watawala wanajifanya kama hawajui chanzo halisi cha kile wanachokiita umasikini uliokithiri mkoani humo.

Bila tafakuri yoyote ya "tafiti" zinazodaiwa kufanywa na Serikali, wanakuja tu na porojo za jumlajumla kuhusu "umasikini" huo. Tafiti hizo za kimangumashi hazielezei chanzo cha tatizo la Mkoa wa Kagera. Haziangalii matokeo ya Vita vya Kagera na uharibifu wa usalama na miundombinu uliosababishwa na ugomvi wa Serikali na Iddi Amin.

Kwamba shughuli za uzalishaji na kiuchumi zilikufa kabisa kutokana na vita hiyo. Hawaoni kwamba Serikali ilikosea (kwa makusudi) kutotangazwa kwa hali ya hatari mkoani humo, kwa maana ya kujenga miundombinu upya na kuwasaidia Wanakagera kurudia maisha yao ya kabla ya vita. Hawasemi Serikali ilifunga mpaka na Uganda, hivyo kusitisha shughuli zote za kiuchumi, ambapo soko kuu la mkoa wa Kagera lilikuwa Uganda.

Baada ya vita Ukimwi uliotokea Uganda ulimaliza nguvukazi kubwa ya mkoa huo kwa kupuputisha maisha ya maelfu ya nguvukazi wa Kagera. Wanajifanya hawajui kwamba MV.

Bukoba ilizama na kuua mamia ya watu, wengi wao wakiwa Wanakagera. Hapohapo, MV. Victoria "iliharibika" na kufanya Wanakagera kukosa kabisa usafiri wa kuwaunganisha na nchi yao, huku mazao yao ya kiuchumi yakishindwa kusafirishwa kwenda kwenye masoko makubwa ya kibiashara ya hapa nchini kama Mwanza na Dar es Salaam.

Serikali haikuona umuhimu wa kuwapa Wanakagera vyombo vingine vya usafiri ili wajimudu kiuchumi. Ndipo pia ulipoingia "Ugonjwa wa Mnyauko" wa migomba uliopigilia msumari wa mateso na umasikini wa Wanakagera. Yapata sasa zaidi ya miaka 15. Je, Serikali ilichukua hatua gani kuwasaidia wakulima wa kilimo cha migomba mkoani Kagera? HAKUNA.

Wakati huohuo Wanakagera walikatazwa kuuza kahawa yao nchini Uganda ambako walikuwa wanapata bei nzuri kulingana na gharama za uzalishaji.

Waliopatikana na uvushaji wa zao hilo waliadhibiwa, ikiwemo vifungo au kufilisiwa, huko kahawa ikilimbikiziwa "TOZO" lukuki bila kutilia maanani gharama za wakulima za uzalishaji.

Wanasahau tetemeko la ardhi ambapo serikali haikusaidia chochote badala yake serikali ilisema nyumba wamezisukuma wenyewe wafe maana majanga makubwa yote uanzia Kagera kama UKIMWI na majanga mwngine makubwa hakuana msaada uliotolewa mbali na kunyang'anywa kidogo kilichopatika na kuzuia waliokuwa tayari kusaidia ndugu zao kuzuiwa kwa kile serikali ilichosema kuwa vitu vyote vikusanywe kwenye mfuko wa mkoa pale Boari lakini vile vitu viliyeyuka na wananchi kuambulia biskuti mpaka sasa watu wengi wanaishi kwenye turubai.

Kwa kagera kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa baadhi ya mikoa ambayo iliwahi kupata majanga kama mafuriko, njaa nk.

Leo hii tunashuhudia jitihada za serikali kuhamisha watu kutoka kwenye hifadhi nakupelekwa kwenye kijiji ambacho imewaadalia wanakuta kila kitu sembuse wanakagera ambao walipata janga la tetemeko na serikali haikujali wala haikujiusisha kabisa na jambo hilo bali ilikuwa ni kuwazuia hata waliokuwa tayari kusaidia.

Hiyo ni mifano michache tu ya hujuma ya Serikali dhidi ya Mkoa wa Kagera kwa miongo mingi sasa. Matokeo yake ni nini? Wananchi wa Mkoa wa wa Kagera waliona Serikali ilikuwa haiwataki, haiwapendi. Wakasema isiwe taabu, wakaamua kuhamia mikoa nyingine nchini na kuwekeza huko.

Je Serikali inajifanya haioni uwekezaji wao mkubwa na uliotukuka katika mikoa mingine nchini, ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na kwingineko?

Serikali imekuwa ikipiga kelele nyingi eti Wahaya wameshindwa kujenga soko na kituo cha mabasi mjini Bukoba, ikijifanya haijui kwamba jukumu hilo ni lake na vyombo vyake, ikiwemo TAMISEMI.

Kwani vituo vya mabasi na masoko ya Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam, Mwanza na kwingineko vimejengwa na nani kama sio Serikali?

Nimalizie kwa kuishauri Serikali kwamba iwekeze mkoani Kagera kama ambavyo imekuwa ikiwekeza sehemu nyingine nchini. Ikiwekeza Kagera, kama ambavyo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kufanya kwa kujenga kitengo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), mkoani humo, basi itarajie kwamba maprofesa na PhD holders kutoka mkoani Kagera watarudi nyumbani kufaidi fursa za uwekezaji wa Serikali.

Ni matumaini ya wengi mkoani Kagera kwamba Mkuu mpya wa Mkoa wa kagera, Mhe. Chalamila ataelewa chanzo cha "UMASIKINI WA MKOA WA KAGERA".

Kwani ni mnataka wanakagera tujenge stendi na soko?

Kwani WASOMI mnaosema ni watumishi wa serikali? Wanakusanya kodi gani? Maeneo mnakopeleka miradi ya maendeleo kama stendi, soko na vyuo vikuu hakuna wasomi? Kigezo icho nichakikatiba?

Mwanza imejengwa viwanda kwakuwa hakuna wasomi? Arusha, Dodoma, Mbeya, Dar Es Salaam nk. Hakuna wasomi?

Mwambie Mkuu wa mkoa awaeleze ukweli wanaKagera kuwa umasikini na utapia mlo wanaousema Kagera ni mradi wa CCM ili waendelee kutawala.

Najua hamna majibu inawezekana mkanifungulia kesi nyingine kwakuwa nimesema ukweli mimi ni Muhaya na mzalendo wa Kagera nachukia unafiki na Majungu

Serikali timiza wajibu wenu acha kurukaruka kama maharage sufuriani.

mujuni Katikabakama.
View attachment 2344869
Tatizo la Watu wa Mkoa wa Kagera hawataki kukosolewa kwenye madhaifu yao na Ukikazia maendeleo ya kuwabadilishia wanatengeneza Majungu yaani wamejaa Ukabahila/Unyarubanja .
Jamaa yangu alinunua Eneo moja ya Kijiji ili ajenge kilichomkuta aliyeuza ni Maneno na kusingiziwa anaharibu Kijiji Chao kwa kuleta Wageni wakamshawishi aliyeuza wamridishe Pesa kwa aliyemuuzia ardhi ili kiwanja kibaki kwa wazawa. Sasa kwa Mtindo huo Mkoa utaendelea vipi yaani hata tenda za Manispaa ili upate uwe Mzawa .
Wakazi wa Mkoa huo wajua kupika Majungu hatari yaani akija kiongozi mwenye nia ya kweli kuubadili Mkoa watampiga Majungu hatari.

Acha kumention sababu dhaifu eti ukimwi mbona ukimwi umeitafuna mikoa Mingi tu Ila bado unaendelea kwa Kasi. Kodi za Manispaa hamtaki kidogo tu high court , kikao Cha Kijiji mnakwenda na katiba yaani mwendo wa kumkomoa Mwenyekiti kwa maswali.
Kumbuka maendeleo hayaji kwenye Sheria Bali Sheria itungwe kusimamia maendeleo Sasa Kagera wao wapo bize na Sheria tu wanasahau usimamizi Mkali wa Sheria unakimbiza Wafanyabiashara ambao ndiyo maendeleo yenyewe.
 
Aliyesoma hiyo habari anifanyie summarization... All in all Kagera imejaa uchawi uvivu na ubaguzi vyote hivi husababisha Umasikini mkubwa ktk mkoa huo... Ndio maana huwez kukutana na Muhaya tajiri...
Mbona unawadhalilisha majirani zangu.uchawi bukoba?.sehem za kichawi Tanzania zinajulikana.simiyu,kigoma,sumbawanga,Tanga,bagamoyo,tabora na mwanza,na mbeya.ubaguzi sawa na uvivu pia sawa.
 
Hivi Kagera kuna makabila mangapi? au mkoa mzima ni wahaya tu?
Hapana siyo wote ni Wahaya.

Kuna makabila mengine kama Wanyambo wa Karagwe na Kyerwa, Waangaza wa Ngara, Wasubi wa Biharamulo.

Wahaya wanapatikana Misenyi, Muleba na Bukoba yote mjini na Vijijini.

Wanyambo na Wasubi wanasikilizana sana na Wahaya ila kwa Waangaza ni ngumu kusikilizana.
 
Hapana siyo wote ni Wahaya.

Kuna makabila mengine kama Wanyambo wa Karagwe na Kyerwa, Waangaza wa Ngara, Wasubi wa Biharamulo.

Wahaya wanapatikana Misenyi, Muleba na Bukoba yote mjini na Vijijini.

Wanyambo na Wasubi wanasikilizana sana na Wahaya ila kwa Waangaza ni ngumu kusikilizana.
Ok uwa naona mada za Kagera wanaongelea kabila la wahaya tu. Haya makabila mengine ni madogo sana?
 
Ok uwa naona mada za Kagera wanaongelea kabila la wahaya tu. Haya makabila mengine ni madogo sana?
Hapana siyo madogo kivile... Ila wahaya wamemeza wenzao kwa kigezo Cha kwenda shule.. Wahaya wanajiona Superior sana. Mfano mnyambo kumuoa Mhaya ni nadra kidogo ila mambo yanabadirika..... Ila wote ni WANAFIKI SANA, USHAMBA na UJUAJI usio na maana, ambao upelekea mivutano isiyo na tija kwenye mambo ya maendeleo
 
NATOKEA KILIMANJARO MKUU
Kumbe unatokea kwenye njaa ndo maana
Screenshot_20220716-180230.jpg
 
Pamoja na kwamba kuna changamoto za wana kagera wao kama wao ila serikali ya CCM pia inahujumu baadhi ya mikoa makusudi kabisa pengine kwa kuwakomoa watu wa eneo husika maana haiwezekani mkoa uwe una makusanyo makubwa lakini hakuna cha maama kinachofanyika ndani ya mkoa husika, hiii inanzia wilaya mpaka ngazi ya mkoa
 
Ok uwa naona mada za Kagera wanaongelea kabila la wahaya tu. Haya makabila mengine ni madogo sana?
Siyo madogo kivile sema wakiulizwa kwenu wapi wote huwa wanataja Bukoba na kabila ni Wahaya ndio inapelekea kufifia na kufunikwa wasijulikane sana.

Ukikutana mtu anasema kwao Bukoba muulize sehemu gani usishangae anakutajia Ngara au Karagwe.

Kabla haijagawiwa eneo lote la Muleba na Bukoba na Misenyi ilikuwa Wilaya moja ikiitwa Bukoba, sasa hivi kila moja ni Wilaya, ila kabila ni moja la Wahaya tofauti yake ni maneno na misamiati michache tu.
 
Pamoja na kwamba kuna changamoto za wana kagera wao kama wao ila serikali ya CCM pia inahujumu baadhi ya mikoa makusudi kabisa pengine kwa kuwakomoa watu wa eneo husika maana haiwezekani mkoa uwe una makusanyo makubwa lakini hakuna cha maama kinachofanyika ndani ya mkoa husika, hiii inanzia wilaya mpaka ngazi ya mkoa
Bora umesema ukweli, mimi niliuliza ni lini wahaya wamezuia serikali kujenga barabara, hospital, vyuo n.k??
 
Kilichoua na kinachoendelea kuua Tanzania ni Ujamaa na sera zake. Kila kitu serikali hiki, serikali kile, Pembeni ya nyumba yako umetupa taka mpaka kumeweka dampo unaulizwa nini kifanyike, jibu ni serikali ije kusafisha. Ujamaa umeua independent thinking.

Vita si sababu ya kufanya miaka 45 mbele balo sehemu ipo vile vile. Hiroshima ilidondoshewa atomic bomb ilioua maelfu na aftermath ilikuwa ya kutisha kuliko vita vyovyote vilivyowahi kutokea na kuifanya Japan kuwa masikini kushinda Tanzania kipindi hiko. Lakini leo hii hakuna jiji la Tanzania linalofikia Hiroshima, leo hii unataka kutuambia vita vya Kagera ndo kumefanya mkoa uwe masikini mpaka leo?

Tuache kulalamika, tujue maendeleo hayaji kwa mdomo, bila kazi kufanyika na kupunguza vizingiti vya biashara watu wafanye kazi kuinua maisha yao

View attachment 2345872
Hiroshima before and after; Unaniambia Kagera imepitia crisis kubwa kuliko hii?
Ambacho haujaelewa alichosema ni nini? Baada ya WW2, Marekani aliwekeza mabilioni ya dola kuijenga upya Ulaya na Japan katika juhudi za makusudi kabisa. Utalinganishaje na Kagera ambayo nasikia hata pesa za fidia walizolipa Uganda na Gaddafi haikufika hata shilingi Kagera?
 
Back
Top Bottom