WE PASCO KAMA LOWASA NDO ANAKUTUMA....KAMWAMBIE TOO LATE TO CATCH THE TRAIN....INFACT AMEBUGI...:lock1:
Kabisa unamaanisha unachokiongea? Anyway
1.Ulikuwa unajua kuna makontena 300 yamepotea,najua hujui hadi PM alipotimba bandari
2.Najua ulishakariri makontena yaliyopotea bandari ni 300,yet again PM akarudi akagundua mengine 2000 yamepotea,ulilijua hili
Unajua bado siamini kama unasema hujui nini kifanyike.
Hapa kazi tu, acha wafanyiwe kazi. Watu km wanajua wanachofanya n kibaya basi n waache mapema. Wasitarajie watafanya ujinga alafu eti wataitwa chemba. Chemba kuongea nn!? utawala wa Maguful n utawala wa wazi hamna kuficha ficha mambo. Unachanwa live ili na wengne wajifunze kupitia kwako kilichokukuta. Watu hii nchi kuna vitengo walishavifanya km mali zao.. Hii nchi bila udikteta haiendi, maana ilikuwa imeshaoza na kunuka.. Fanya kazi inavyostahili, Magufuli utamckia tu
NImeangali maoni ya wengi kati ya wale wanaopinga hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano, nimegundua kuwa watu hawa aidha wao wenyewe wameathirika na matukio hayo moja kwa moja, au ndugu/rafiki zao wa karibu ni wahanga wa matukio hayo. Mahali ambapo taasisi imeruhusu makontena 349 yatolewe bila kulipa ushuru, lugha nzuri ya kuto kudhalilishana hapo ilikuwa ni ipi. Mahali ambapo makontena zidi ya elfu mbili yametolewa bandalini bila kulipa ushuru, lugha tamu ya kuwafurahisha waliofanya hayo ilikuwa ni ipi. Tuache unafiki, hapa kuna upotevu wa kodi ya serikali, hakuna kuchekeana maana ukicheka na nyani utavuna mabua. Mtumishi wa serikali bila aibu anamiliki nyumba zaidi ya ishirini, ni kitu gani hicho, acha wafu wawazike wafu wao.
Na wewe Shark hivi unavyofanya siyo vizuri kabisa, huu siyo utawala bora kabisa yaani unanigombeza hadharani namna hiyo kiongozi wangu? Si ungenifuata chemba tukayamaliza huko huko? Ha ha ha haaaaaa hii sasa ni hatari!