Anachofanya Kibonde wa Clouds FM ni hatari kwa redio hiyo

Bahimba

JF-Expert Member
May 8, 2013
510
346
Nasikiliza Clouds FM hapa kipindi cha jahazi, Kibonde anajaribu kusafisha mto ulochafuka. Lakini mtazamo wangu ni kwamba anajaribu kutia sukari baharini, huku akimponda mtumishi wa mungu Baba Askofu kwamba anatumia ganja.

Anasema kuwa Mungu haangalii majina ya mtu, anasema Mungu anaangalia utendaji wa mtu.
 
Mh!! Nae anataka kutajwa na mtaalamu wa kushushua ili nyota ing'ae au!!!!?
 
Mi nafikiri wanajisahaulisha tatizo hasa ni nini? Tatizo sio kwamba flani ana cheo gani wala sio kwa sababu alitumia cheo chake kupambana na kina flani.
Tatizo la msingi hapa ni kujisafisha kutoka kwenye tuhuma za kutumia vyeti na majina yasiyo halali kujinufaisha kielimu na kuudanganya umma ambalo hili ni kosa la jinai kama yalivyo makosa mengine.
Ili tuendelee wanaotetea kosa hili wanatakiwa watambue kwamba hakuna haki bila wajibu, ili kupata haki lazima utimize wajibu na kamwe usijaribu kupata haki usiyoistahili.
 
Sogea pale mbele kidogo kama unaenda kawe sikiliza wale achana hiyo radio ya ccm unategemea itaongea nn kama ilikuwa nae kwenye towaz aliyokuwa anatembelea dah
 
Ukiwa na tabia ya kumsikiliza Kibo, January hadi December, baada ya mwaka nawe unaishia kuwa mtu wa hovyo, hovyo tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom