Anaandika Jemedari Said kuhusu sakata la Simba

Anaandika Jemedari Said kuhusu sakata la Simba

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,448
Reaction score
46,216
Kuna tafsiri ambayo wana Simba SC Tanzania wanayo kwa Mwenyekiti wa Klabu yao MURTAZA MANGUNGU na kuna tafsiri wana Simba wanayo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CRESENTIUS MAGORI.

Bahati mbaya sana nadiriki kusema wengi wanawatafsiri hawa watu TOFAUTI (Vice Versa) na ukweli ulivyo. Mmoja anaonekana kama mtu hohe hahe na asiejielewa wala kujua kitu na mwingine anaonekana kama mjuzi wa mambo ambaye hakuna anayemshinda kwenye mpira wa nchi hii na masuala ya klabu ya Simba.

Nimefuatilia jambo lao tangu jana na leo nimefanya mahojiano nao wote wawili, nimejifunza mambo mengi sana.

Mmoja ni msikivu, anafuata taratibu, anatumia busara, hajakivaa cheo cha Mwenyekiti, mtu muangwana ambaye hataki ugomvi wala kuparurana na watu kısa cheo, ameweka manufaa ya klabu mbele bila kujisifu wala kumtangazia mtu, ana iona klabu ni mali ya wana Simba wote walio na thamani sawa.

Mwingine ni mjuaji ambaye bila yeye Simba si lolote, mjuzi wa mambo ya soka na mbobezi ambaye anastahili vyeo vyote na heshima, anaijua Simba kuliko yoyote, yeye ni Simba ‘A’ na wengine wanafata nyuma yake, ameipigania Simba na kuichangia pengine kuliko yoyote bila kujali aliowakuta klabuni, neno lake ni amri klabuni hapo.

Kwa mujibu ya maelezo yao ya leo sikuona shida ya Mangungu kwa kilichotokea jana na mpaka sasa sikuona UBATILI wa jambo zima, kama ambavyo sijaona uhalali wa chapisho la Magori tena likawekwa kwenye page ya klabu likimnannga Mwenyekiti wa Simba SC.

Mangungu anasema Bodi ilipoteza uhai wake baada ya katiba mpya kupitishwa na BMT, kilichokuwa kinafanyika ni busara ya kiuongozi tu kuiweka hai kuepusha migogoro isiyo ya lazima. Lakini amelazimishwa na Serikali kuteua wajumbe wa baraza la wadhamini na akipewa deadline, hawa ni wasimamizi wa mali za Simba SC na yeye ndo Mwenyekiti wake, shida iko wapi? Kama jambo hili lisingefanywa sasa lingefanywa lini?. "
 
jemedari huwa n nyau, kutwa kuiponda yanga kwa koti la uchambuzi ila ukweli anaumia mwaka wa 5 yanga mabingwa

mangungu yuko sawa sana, ila kwa nini asiachie cheo hicho kuepusha hizi kelele zote
 
"Vise versa" haina maana ya "TOFAUTI", bali maana yake ni "VIVYO HIVYO KINYUME CHAKE"

Mfano "Lions hate hyenas, and vice versa." maana yake ni sImba wanawachukia fisi, na vivyo hivyo kinyume chake: yaani fisi pia wanachukia simba.

Nilisikiliza mahojiano ya baina Crown Media na wote wawili, Mangungu na Magori. nikaona wote wana mapungufu makubwa ya sifa za uongozi japo Magori ni sifuri kabisa

(a) Wote Mangungu na Magori hawajui kujenga hoja; ni wepesi wa kuwashambulia watu wanaowahoji kwa kuwarudishia maswali badala ya kujibu hoja walizoulizwa.

(b) Magori hajui mipaka ya madaraka yake wakati Mangungu anaijua vizuri.

(c) Magori hajui katiba ya taasisi yake inasemaje wakati Mangungu anaijua.

(d) Wote ni wana majigambo, japo Magori anajigamba kwenye kila jambo wakati Mangungu anajigamba kuwa anajua kusoma Katiba ya Simba kuliko wengine wote. Magori ana majigambo zaidi ya Mangungu
 
Tutamlinda Mwenyekiti wetu Mangungu kwa wivu mkubwa. Akitaka waganga konki wa kienyeji au walinzi shirikishi (Mabaunsa tuliopitia mafunzo ya mgambo aka Jeshi la Akiba) tupo! Yeye aseme tu ili ulinzi uanze mara moja.
 
Hiyo sijui, lakini angalia hata kwenye uzi huu watu wa Yanga wanavyomuunga mkono Mangungu
Sasa Mjomba, kwa sera hizi bora kabisa za Mwenyekiti Mangungu za kuirejesha Simba mikononi mwa wanachama unataka tusimuunge mkono? Unataka simba iendelee kuwa chini ya Kanjibhai mjanja mjanja kupitia vibaraka wake akina Magori!

Mitano 🖐️ mingine kwa Mwenyekiti Mangungu.
 
Back
Top Bottom