Anaandika Jemedari Said kuhusu sakata la Simba

Anaandika Jemedari Said kuhusu sakata la Simba

Wasiomjua magori ndio watapingana na mangungu,magori mpigaji,mwizi,mjuaji na mtu wa majungu vibaya mno,anachofanya kwa mangungu ndicho alichokua anakifanya pale nssf kwa mohamed dau,simba inamnufaisha mno magori nyakati hizi kuliko mangungu
 
Bin Kazumari ni mwehu...

Angemsikiliza vizuri Mangungu angejua kosa liko wapi...

Katiba iko wazi, mkutano utaitishwa na mwenyekiti baada ya kushauriana na bodi ya wakurugenzi...

Unapoishirikisha bodi ni lazima kuwe na majadiliano baadaye maafikiano...

Kwa kilichotokea jana, Kazumari anaamini bodi ilishirikishwa na wakaafikiana?

Hoja ya pili ni timing ya hii agenda, unajua jambo litaleta mgogoro ndani ya club halafu unakulupuka kulileta siku chache kabla ya mechi ngumu (Derby), hapa hata kama una nia njema lazima tuhoji dhamiri yako...

Nahitimisha kwakusema kama Kazumari anampenda sana Magungu amchukue akanywe nae chai, sisi Simba hatumtaki.
 
Shida mwekezaji kila kipindi cha usajili lazima kutokea songombingo na kukumbushana madeni yaliopita!!

kwani wanasimba walienda kwake kukopa shilingi yoyote!!!!

Yeye mwanaSimba nasisi wanasimba
yeye atoe ela kwa kuchungulia ivyoivyo!!!

nasisi wengine tunachangia maumivu makali na
makasiriko
pamoja na kutii maelekezo ya kwenda kunya kwa watu 🤔
 
Yeye anatizama ela tu!!
unadhani kwenda kunya kwa watu ni jambo dogo!!!!

yeye angeweza kweli kwenda kunya sehemu ya wazi km vile angepewa ilo jukumu kwa faida ya Simba❗️
 
Magori ndiye anapewa pesa za usajili na mo halafu anapeleka invoice kwa viongozi wasaini kama deni hapo ndiobtatizo linapoanza.
Magori mpira haujui ile mechi Simba ilipofungwa goli moja baada ya Camara kufata mpira uliokuwa unatoka nje Magori alikurupuka mtandaoni kumwita Camara mara tatu hapo alikuwa anatengeneza dhana Camara ameuza mechi.
Siwezi kushangaa sababu ya Camara kuachwa ikawa Magori sasa hivi amegeuka chawa wa mo ila yeye ndio kirusi.
 
Magori ndiye anapewa pesa za usajili na mo halafu anapeleka invoice kwa viongozi wasaini kama deni hapo ndiobtatizo linapoanza.
Magori mpira haujui ile mechi Simba ilipofungwa goli moja baada ya Camara kufata mpira uliokuwa unatoka nje Magori alikurupuka mtandaoni kumwita Camara mara tatu hapo alikuwa anatengeneza dhana Camara ameuza mechi.
Siwezi kushangaa sababu ya Camara kuachwa ikawa Magori sasa hivi amegeuka chawa wa mo ila yeye ndio kirusi.
magori alikua anatembelea nyota ya pope,ila kiukweli si mtu wa mpira
 
Kuweni makini sana na mapoli yaliyomo jirani wakipita tu hao jamaa wameyashusha
 
Kuna tafsiri ambayo wana Simba SC Tanzania wanayo kwa Mwenyekiti wa Klabu yao MURTAZA MANGUNGU na kuna tafsiri wana Simba wanayo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CRESENTIUS MAGORI.

Bahati mbaya sana nadiriki kusema wengi wanawatafsiri hawa watu TOFAUTI (Vice Versa) na ukweli ulivyo. Mmoja anaonekana kama mtu hohe hahe na asiejielewa wala kujua kitu na mwingine anaonekana kama mjuzi wa mambo ambaye hakuna anayemshinda kwenye mpira wa nchi hii na masuala ya klabu ya Simba.

Nimefuatilia jambo lao tangu jana na leo nimefanya mahojiano nao wote wawili, nimejifunza mambo mengi sana.

Mmoja ni msikivu, anafuata taratibu, anatumia busara, hajakivaa cheo cha Mwenyekiti, mtu muangwana ambaye hataki ugomvi wala kuparurana na watu kısa cheo, ameweka manufaa ya klabu mbele bila kujisifu wala kumtangazia mtu, ana iona klabu ni mali ya wana Simba wote walio na thamani sawa.

Mwingine ni mjuaji ambaye bila yeye Simba si lolote, mjuzi wa mambo ya soka na mbobezi ambaye anastahili vyeo vyote na heshima, anaijua Simba kuliko yoyote, yeye ni Simba ‘A’ na wengine wanafata nyuma yake, ameipigania Simba na kuichangia pengine kuliko yoyote bila kujali aliowakuta klabuni, neno lake ni amri klabuni hapo.

Kwa mujibu ya maelezo yao ya leo sikuona shida ya Mangungu kwa kilichotokea jana na mpaka sasa sikuona UBATILI wa jambo zima, kama ambavyo sijaona uhalali wa chapisho la Magori tena likawekwa kwenye page ya klabu likimnannga Mwenyekiti wa Simba SC.

Mangungu anasema Bodi ilipoteza uhai wake baada ya katiba mpya kupitishwa na BMT, kilichokuwa kinafanyika ni busara ya kiuongozi tu kuiweka hai kuepusha migogoro isiyo ya lazima. Lakini amelazimishwa na Serikali kuteua wajumbe wa baraza la wadhamini na akipewa deadline, hawa ni wasimamizi wa mali za Simba SC na yeye ndo Mwenyekiti wake, shida iko wapi? Kama jambo hili lisingefanywa sasa lingefanywa lini?. "
Jemedari akasome katiba ya Simba ni vipi wadhamini wanaweza kukoma.
 
Back
Top Bottom