Ana ujauzito wa mwingine na anataka tuoane

Ana ujauzito wa mwingine na anataka tuoane

Ulipokutana naye hukutuomba ushauri, alipojificha miezi minne hukutuambia, leo kaja na gea kuubwa kuwa likwenda toa ikakataa.
Yote sawa, tu, mwambie akutonye mwenye mtoto. Mwuulize jamaa kama kweli hataki mtoto, weye chukua boga na ua lake. Weka ndani, atakuja kuwa kifaa baadaye. Nimeona walioliwa wakiwa ndani ya chumba cha ndoa. Wakachepuka kwa ma X wao. Mtoto kaja sura tofauti na wazazi. Bado kaitwa mwanaye. Kitanda hakizai haram. Chukua kimya kimya ka wampenda mwanamke huyo.
 
Hili nalo la kuomba ushauri?

Mapenzi yaki kuendesha hakika maisha yako yatayumba. Tumia akili kufikiria sio moyo.
 
yaani kaliwa ndani ya uhusiano wenu halafu unakuja kutuomba ushauri???.....kwa jweli we differ.mi ningemtimua fasta sana
 
Jiulize maswali haya alafu majibu yake ndo yatakupatia maamuzi.....

je wewe bado unampenda?

Vp mwanaume wake akianza kusumbua baada ya kuzaliwa mtoto,utajiskiaje?

Kama ameweza kuchepuka kabla ya wewe kuwa naye kwa muda kwenye ndoa atashundwa kuchepuka mkishaingia?

Ameshatoa mimba ngapi kabla ya hiyo bila ww kujua?

Una uhakika na umejiridhisha kwamba hatorudia?

Nafkiri ukipata majibu utachukua uamuzi mzuri.
 
Daaah hiyo ishu sijui niseme imenikuta mimi ila tofauti ni kidogo sana huyo muhusika mwenye mimba ni mchepuko wangu sasa sijui kama hiyo story iko relate na ya kwangu
 
Jamani wadau, naheshimu sana mawazo yenu.

Mchumba wangu nje na kuwa nae miaka takribani mitatu sasa, amepata ujauzito kwa jamaa mwingine.

Kanidanganya tusionana karibu miezi miinne ili atoe mimba ikashindikana na sasa kaamua kusema ukweli. " Nilifanya bila ridhaa kwenye birthday ya rafiki yangu nikapata ujauzito, nisamehe nakupenda sana usiniache" . Maneno yake akijitetea.

Nimepwatwa hasira sina maamuzi mazuri.

Nisaidieni wadau.

Jamaa kaikataa mimba

Huna sababu ya kutafuta ushauli ndugu..ishi nae siku moja utaona mengine na yatakupa majonzi zaidi ya hayo,nyani ukimkuta shambani na akakuona na bunduki hua analia,msamehe na kumuacha kisha kesho urudi shambani utakuta amekula mahindi yote
 
Huna sababu ya kutafuta ushauli ndugu..ishi nae siku moja utaona mengine na yatakupa majonzi zaidi ya hayo,nyani ukimkuta shambani na akakuona na bunduki hua analia,msamehe na kumuacha kisha kesho urudi shambani utakuta amekula mahindi yote

sio mahindi tu atakuta amefukua hadi MAGIMBI TEH TEH TEH..........
 
Oa, oa kijana usiogope hapo utakuwa umenunua ng'ombe halafu una uhakika wa kupata ndama soon,,,,
 
Kama unampenda, utamlinda, inauma sana, ila kama unampenda, unaweza kuendelea nae japokuwa kuna mawili ( kama hajitambui basi atakuona mjinga na kama anajitambua atakuheshimu sana maana umemtoa aibu).
 
Kaka kama kusoma basi tazama picha...kama vyote kwako taabu,basi ulizaliwa upate taabu mpaka kwenye mambo yanayofurahishaaa na kufurahiwa...
 
Kaka kama kusoma basi tazama picha...kama vyote kwako taabu,basi ulizaliwa upate taabu mpaka kwenye mambo yanayofurahishaaa na kufurahiwa...
 
huyo kazini nje tena bila kinga....nenda kapime ukimwi kwanza....ukikuta mzima...shukuru...na ukitaka kufa endelea nae...sio mbaya pia.
 
Kuna wadada wengi wanalilia ndoa na they are




Kuna wadada wengi wanalilia ndoa na wana tabia njema tu lakn hawajapata huyo anachrzea mahusiano eeh nyambafu mkubwa sana et katembea nae peku katakuwa ndo kamchezo wake Mungu kaamua kumuadhibu sikushauri uendelee nae ingawa kwa upande mwingine uamzi ni wako haya ni maisha yako Fanya maamzi sahihi na Mungu akusaidie katika hili usije kuiona ndoa chungu ni hayo tu…
 
Back
Top Bottom