Ana Penzi La Moyoni??

eRRy

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
1,125
204
Marafiki zangu, hakuna jambo baya katika uhusiano kama kutokuitambua nafasi yako. Hapa namaanisha kwamba, upo na mwenzi wako ambaye ana dalili zote za nje zinazoonyesha kwamba anakupenda, lakini kilichopo ndani yake unakuwa haukifahamu!

Wengi huwa hawana muda wa kufikiria juu ya hilo, lakini napenda kukufahamisha kwamba, lipo penzi la nje, ambalo mwenzi wako anaweza kutumia kila anachoweza kukufanya uamini kama anakupenda sana lakini ndani ya moyo wake kukawa na vitu vingine tofauti.

Hii ni mada ambayo itakuwezesha wewe kijana (mvulana/msichana) kufahamu nia ya ndani ya mwenzi wako. Kabla sijaanza kuwapa vipengele muhimu zaidi, tuanze kwa kuangalia tofauti kati ya penzi la ndani na lile la nje.

PENZI LA MACHONI
Hili halipo moyoni, kwasaabu hiyo basi linakuwa la usanii kupitiliza. Anakuwa mtu wa ahadi sana, anaweza kukufanyia mambo makubwa sana kwa nyakati tofauti, kuhakikisha unamuona kama mtu muhimu ambaye maisha anayaweza!
Anaweza kukupiga mabusu mfululizo mkiwa faragha tu, hawezi kufanya hivyo mbele za watu. Mwoga hata wa kukushika mkono. Hawezi kukufanyia mambo ya kimahaba mnapokuwa mmetoka pamoja. Mwingi wa visingizio hata kama mmepanga kutoka kwa ajili ya jambo muhimu sana.

Kimsingi kwakuwa penzi lake ni la mashaka, siyo la kudumu na halipo moyoni, huwa kama anakutega, akisubiri ukosee kidogo ili muachane. Hana penzi la kweli kwako.

PENZI LA MOYONI
Hili ni penzi la dhati, ni rahisi kulijua, lakini pia ni vigumu sana kulifahamu! Unatakiwa kuwa makini sana na mwenzi wa aina hii ili uweze kujua msimamo wake.

Kwanza kabisa anazungumzia anavyokupenda, siyo mkali wa stori za ngono na mara nyingi amekuwa akizungumzia zaidi maisha na wewe kuliko kuwaza mambo yasiyofaa.

Penzi lake ni uwazi na hujisikia furaha kukushika mkono na hata kukuzawadia busu mwanana mbele za watu. Anafanya haya kwasababu anatetea kile kilicho moyoni mwake. Anatetea penzi lake la kweli.

Zipo dalili 10 muhimu zaidi, ambazo akiwa nazo mwenzi wako ujue hana penzi la moyoni, badala yake penzi lake ni la machoni. Dalili hizo ni kwa upande wa wanaume na wanawake. Leo tunaanza na upande wa wanaume kwanza, kabla ya kugeukia upande wa wanawake.Hebu zisome dalili hizo uingize kitu kipya kichwani mwako.

(1) Msemaji tu...
Mwanaume ambaye ana nia ya kukutumia na kukuacha, unaweza kupima hata maneno yake, mara zote amekuwa mtu wa maneno mengi ambayo hayatekelezeki! Ahadi zake zimekuwa nyingi ambazo baadaye unagundua kwamba ni hewa.
Huyu hana mapenzi ya kweli na nia yake ni kukuchezea na kukuacha na ndiyo maana anaweza kuropoka hata mambo ambayo anajua wazi kwamba hana uwezo wa kuyatekeleza. Mchunguze zaidi mwanaume wa aina hii, kwani ni moja kati ya dalili 10 za msingi za mwanaume ambaye hafikirii sana kuwa na wewe hapo baadaye.

(2) Hazungumzii maisha ya baadaye!
Hataki kabisa kuzungumzia juu ya mustabali wa maisha yenu ya baadaye. Hataki mijadala ya mambo ya ndoa, ukianzisha anakukatisha. Hata mijadala hiyo inapotokea kwenye runinga au redio mkiwa naye, atabadilisha channel ili asisikilize au kuona.
Huyu bado yupo yupo, anapendezwa na uzuri na mwonekano wako ambao kwake ni pambo la muda tu, na siyo la kudumu kama ambavyo wewe unawaza. Hana mpango na wewe.

(3) Anapenda penzi la siri
Hataki uhusiano wenu ujulikane na ndugu zake/zako wa karibu. Hata inapotokea akalazimika kufanya hivyo, hutoa visingizio vingi sana. Anaogopa kukutambulisha kwasababu anafahamu wazi kwamba hana nia ya kuishi na wewe hapo baadaye badala yake anakutumia tu!

(4) Mtu wa kujirusha sana
Hafikirii kabisa kuhusu maisha, muda wote anawaza starehe. Wengi wa aina hii ni wale ambao bado wanaishi na wazazi au ndugu, wakiwategemea kwa kila kitu. Lakini pia kuna wengine ambao wanafanya kazi, lakini hawana malengo na kazi zao, muda wote ni starehe sana.

Ni rahisi kukutana naye akiwa na pesa, lakini anapoishiwa kidogo hukukwepa. Anaogopa kwasababu wewe kwake ni wa kujistarehesha tu.

(5) Msiri...
Hataki mambo yake yawe wazi sana, ukimwuliza anakuwa mkali. Hapendi umchunguze kuhusu mambo yake ya kazi, mbaya zaidi ni msiri hata kwa mambo ambayo una haki ya kuyafahamu.
Mathalani, simu yake inaweza kuingiza ujumbe mfupi wa maneno ambao utautilia mashaka au akapigiwa simu na kwenda kuzungumzia nje, akirudi ukimwuliza kwanini alitoka nje, anakuwa mkali. Huyu hana nia na wewe na ndiyo maana haoni thamani yako.

Hataki ujue mambo yake, kwasababu hajiamini.
Kutokana na ufinyu wa nafasi, kwa leo naishia hapa. Usikose wiki ijayo kwa mwendelezo wake ambapo tutamalizia vipengele vitano vilivyosalia kabla ya kugeukia upande wa wanawake ambao hawana mapenzi ya kweli kwa wenzi wao. Nashukuru sana kwa kunisoma, nawatakieni mapumziko mema ya mwisho wa wiki.

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi ambaye anaandikia magazeti ya Global Publishers, pia ni Mwandishi wa Vitabu vya True Love na Secret Love vilivyopo mitaani. Unaweza kumtembelea katika www.shaluwanew.blogspot.com


source:http://www.globalpublisherstz.com/2009/10/23/ana_penzi_la_moyoni_au_machoni.html

showing_some_love_comment_graphic_01.jpg
 
Hivi you chaps have ever been in real ndoa?...au mnadesa tu hii mambo!

Sometimes tunalazimika kufanya zaidi ya nusu ya mambo hayo uliyoyataja ...ili tu kulilinda penzi lisiharibike!

We acha tu bana...sio kwamba tunapenda saana kufanya hivyo,...bali kua uyaone!
 
eeee kumbuka nimeitowa kwenye chanzo flani! sijaitunga mkuu!
 
Back
Top Bottom