ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,141
- 951
Mke ana nga'ng'ania aongezewe mtaji ili aende Dubai, Hong Kong, Jakat na Taipei akaanze biashara ya nguo. Hivi karibu ameonyesha kutokea kuipenda hela sana tofauti na mwanzoni. Yeye ni mfanyakazi ana mshahara wa kati na nyumbani maisha si mabaya, Mume nae ni mfanyakazi ila mwanzoni mwa mwaka huu alianza hili wazo la kutaka kuacha kazi ili aanze biashara akidai inalipa sana kwa kuwa marafiki zake wote wana maduka makubwa Kariakoo, anataka kuacha kazi. Anadai kisha kopa kiasi fulani cha fedha toka kwa mwanaume mmoja anaefanya nae kazi anasema wameshibana, anataka kuongezewa tu mtaji aanze!