Ana mapenzi kweli huyu au anataka kulelewa tu!

Ana mapenzi kweli huyu au anataka kulelewa tu!

Hata mimi nikipata mteremko kama wako nashika kweli.
Mvumilie si unampenda.
 
he he he he kuna mmoja hapa analea kama wewe tena mjamaa ana govi kila cku bibie magonjwa ya chini na bwana hatoi hata jero nauli
 
Kila siku nasoma post zinazowaongelea wadada wa mjini nashangaa vijana hawaongelewi. Alitokea kijana mmoja tunapanda wote gari tukitoka kazini (hatufanyi ofisi moja) aliniomba namba za simu nikampa akaanza kuniimbisha sikua mgumu sana kwa vile sikua kwenye mahusiano baada ya siku chache akaomba anisindikize nyumbani nikamkubalia alipofika akakuta ndugu yangu ninayeishi naye amepika tukapakua tukala, since that day akitoka kazini tunaongozana hadi nyumbani kwangu ninapika tunakula tatizo sasa hatoi hata senti tano sometimez anachagua chakula ooh mi sipeni ugali usiku mara leo nimechoka wali kila siku, mwanzo nilijua kwa vile ndo tumekutana katikati ya mwezi labda kamaliza mshahara huu mwezi wa tatu sasa kila siku katika wiki anakuja kula kwangu jioni hatoi hela ukienda dukani utaona meseji nletee na soda beib. Nampenda sana tu ila mmh ananichosha kwakweli kwanza nashindwa kuelewa ana mapenzi ya kweli au ni huduma tu ndo zinazomuweka kwangu.

Baada ya kuanza uhusiano akaniambia kua ana demu wake, demu anamfanyia mshikaji vituko anataka kumuacha ila anadai anashindwa kwavile demu anakazi nzuri na kwao wanahela kuna vitu amepanga kumfanyia kwahiyo mimi nivumile tu soon akimaliza hivyo alivyomuahidi wataachana maana ananipenda zaidi nna heshima najua kulea mwanaume, nna sifa za kua mke.

huyo ulimwendekeza tu toka mwanzo..... haya mambo ukiyakosea mwanzo kidogo tu ni shida......... sawasawa na na sisi wa kiumeni ukianzisha uhusiano na mtoto wa kike kwa kumhonga na kujifanya baaabkubwa lazima mbeleni huo uhusiano uwe shubiri.... hujachelewa lakini kurekebisha mambo
 
he he he he kuna mmoja hapa analea kama wewe tena mjamaa ana govi kila cku bibie magonjwa ya chini na bwana hatoi hata jero nauli

ukute bibie naye kuna kitu anakipata kutoka kwa hiyo kitu...........
 
Hahaha what a desperate girl! Dah pole sana, ila kama ni kumlea kunakupa raha zaidi ya ukimwacha endelea bi dada! Who r we to judge!
 
Ngoja na mm nijisogeze! mjini hapa bila mipango utaishia kupiga miayo tu!
 
Kijana mtaji wake kiuno. Angekuwa hawajibiki kwenye bed ungekuja kulalamika anakupa pesa lakini hakuridhishi.
BTW si unajua kulea 'mume' why afraid.

Ila aisee kuna vidume vina 'guts' Yaani kula kila siku kwa dem!! Mimi hata nilogwe sifanyi hiyo biashara.
 
dada usijitoe ufahau hapo hakuna upendo kwanza ana gf wake asikudanganye kuna mambo ya kurekebesha labda ndoa utalia na kusaga meno bora lianzishe mapema usipoteze muda wako kulea pasipostahili
 
Ukitoka kazini piga zako kiepe ye akija mwambie no food, siku tatu mfululizo akiendelea kuja basi either ni mario mzoefu au hua hafati hiyo menu yako akistop shukuru Mungu na namba yake futa kabisaaaaaaa
 
Back
Top Bottom