Kila siku nasoma post zinazowaongelea wadada wa mjini nashangaa vijana hawaongelewi. Alitokea kijana mmoja tunapanda wote gari tukitoka kazini (hatufanyi ofisi moja) aliniomba namba za simu nikampa akaanza kuniimbisha sikua mgumu sana kwa vile sikua kwenye mahusiano baada ya siku chache akaomba anisindikize nyumbani nikamkubalia alipofika akakuta ndugu yangu ninayeishi naye amepika tukapakua tukala, since that day akitoka kazini tunaongozana hadi nyumbani kwangu ninapika tunakula tatizo sasa hatoi hata senti tano sometimez anachagua chakula ooh mi sipeni ugali usiku mara leo nimechoka wali kila siku, mwanzo nilijua kwa vile ndo tumekutana katikati ya mwezi labda kamaliza mshahara huu mwezi wa tatu sasa kila siku katika wiki anakuja kula kwangu jioni hatoi hela ukienda dukani utaona meseji nletee na soda beib. Nampenda sana tu ila mmh ananichosha kwakweli kwanza nashindwa kuelewa ana mapenzi ya kweli au ni huduma tu ndo zinazomuweka kwangu.
Baada ya kuanza uhusiano akaniambia kua ana demu wake, demu anamfanyia mshikaji vituko anataka kumuacha ila anadai anashindwa kwavile demu anakazi nzuri na kwao wanahela kuna vitu amepanga kumfanyia kwahiyo mimi nivumile tu soon akimaliza hivyo alivyomuahidi wataachana maana ananipenda zaidi nna heshima najua kulea mwanaume, nna sifa za kua mke.