Ana mapenzi kweli huyu au anataka kulelewa tu!

Ana mapenzi kweli huyu au anataka kulelewa tu!

Kila siku nasoma post zinazowaongelea wadada wa mjini nashangaa vijana hawaongelewi. Alitokea kijana mmoja tunapanda wote gari tukitoka kazini (hatufanyi ofisi moja) aliniomba namba za simu nikampa akaanza kuniimbisha sikua mgumu sana kwa vile sikua kwenye mahusiano baada ya siku chache akaomba anisindikize nyumbani nikamkubalia alipofika akakuta ndugu yangu ninayeishi naye amepika tukapakua tukala, since that day akitoka kazini tunaongozana hadi nyumbani kwangu ninapika tunakula tatizo sasa hatoi hata senti tano sometimez anachagua chakula ooh mi sipeni ugali usiku mara leo nimechoka wali kila siku, mwanzo nilijua kwa vile ndo tumekutana katikati ya mwezi labda kamaliza mshahara huu mwezi wa tatu sasa kila siku katika wiki anakuja kula kwangu jioni hatoi hela ukienda dukani utaona meseji nletee na soda beib. Nampenda sana tu ila mmh ananichosha kwakweli kwanza nashindwa kuelewa ana mapenzi ya kweli au ni huduma tu ndo zinazomuweka kwangu.

Baada ya kuanza uhusiano akaniambia kua ana demu wake, demu anamfanyia mshikaji vituko anataka kumuacha ila anadai anashindwa kwavile demu anakazi nzuri na kwao wanahela kuna vitu amepanga kumfanyia kwahiyo mimi nivumile tu soon akimaliza hivyo alivyomuahidi wataachana maana ananipenda zaidi nna heshima najua kulea mwanaume, nna sifa za kua mke.

mmmh una uvumilivu mdada mie hayo sifanyi ila inaonekana hana mpango na wewe bado yuko safarini hajatua bado, sipendi vya mtu ila pia sipendi pasiwepo na usawa ktk suala la kiuchumi
 
Nyie ndio mnaotuharibia vijana wetu mpaka wanakuwa marioo!!!!
Inatakiwa yeye akutunze wewe sio wewe umtunze yeye,siku akikosa kwa wanawake ataenda kwa wanaume Mpige na mwiko machoni ili asirudie tena alaa!!!!.
 
We wa kuonewa huruma si bure...

........Baada ya kuanza uhusiano akaniambia kua ana demu wake, demu anamfanyia mshikaji vituko anataka kumuacha ila anadai anashindwa kwavile demu anakazi nzuri na kwao wanahela kuna vitu amepanga kumfanyia kwahiyo mimi nivumile tu soon akimaliza hivyo alivyomuahidi wataachana maana ananipenda zaidi nna heshima najua kulea mwanaume, nna sifa za kua mke.
 
Dada timuaaa mbiooo unaliwaaa...khahh mwanaume gan uyo anam'describe girl wake kwa status ya kimaisha tu badala ya urembo wake,IMAGINE AKIWA MUME HUYO,SI UMEUMIAA??
 
Dada timuaaa mbiooo unaliwaaa...khahh mwanaume gan uyo anam'describe girl wake kwa status ya kimaisha tu badala ya urembo wake,IMAGINE AKIWA MUME HUYO,SI UMEUMIAA??

mapenzi ni kusaidiana yani kumnunulia soda mwanaume unaons vibaya we umezoea kuchuna tu wacha na wewe uchunwe kidogo ha ha ha
 
Hatari huyo. Na tapeli la mujini. Na muongo, anakuchezea picha.

Kwanza jua dem hana, anakudanganya ili ushindande na dem ambae hayupo maishani mwake. Anafikiri utamuambia wewe utamfanyia hayo atakayo akiachana na huyo dem.
Chezea watoto wa mujini kwa kutunga mkanda wa uongo ili atapeli mtu.
Pengine hata kazi hana, ila kajua wewe unakazi ndio anataka akulie pesa zako
 
Daa, Uzi huu umenikumbusha bi dada Fulani , Kuna wakati maisha yalimnyookea lakini baadae upepo ukabadilika hadi kodi ya nyumba ikawa tabu.Sasa alikuwa na jamaa yake ambaye alifanya Kwa shosti kama kwake akifika atapewa huduma zote Na hachangii hata senti.Mdada hata ajisemeshe vip jamaa anajifanya hajaskia kabisa.Ikabidi Dada aingie Na mbinu yakujifanya anamtisha jamaa kwamba anarudi kwawazazi kwani maisha ya Dar yamemshinda. Jamaa akaitikia fasta Kweli unaondoka! Daa itabidi unishtue mapema niwahi hii nyumba halafu utaniuzia redio Na TV yako.Ikawa jamaa kila Siku anamuuliza unaondoka lini mie nihamie hapa? Bi dada alichoka .Ndio Haya ya Huyu mwenzetu fukuzia mbali hilo zigo.
 
Vumilia tu ili mradi anakugegeda vzr basi.
Mwenzako ana uwezo wa kugegeda lkn uwezo wa kununua chakula hana.
Wewe una uwezo wa kununua chakula lkn uwezo wa kujigegeda huna na mtu wa kukugegeda huna so u have be patient! Just give him food na ye akusuuze roho yako.
 
Kila siku nasoma post zinazowaongelea wadada wa mjini nashangaa vijana hawaongelewi. Alitokea kijana mmoja tunapanda wote gari tukitoka kazini (hatufanyi ofisi moja) aliniomba namba za simu nikampa akaanza kuniimbisha sikua mgumu sana kwa vile sikua kwenye mahusiano baada ya siku chache akaomba anisindikize nyumbani nikamkubalia alipofika akakuta ndugu yangu ninayeishi naye amepika tukapakua tukala, since that day akitoka kazini tunaongozana hadi nyumbani kwangu ninapika tunakula tatizo sasa hatoi hata senti tano sometimez anachagua chakula ooh mi sipeni ugali usiku mara leo nimechoka wali kila siku, mwanzo nilijua kwa vile ndo tumekutana katikati ya mwezi labda kamaliza mshahara huu mwezi wa tatu sasa kila siku katika wiki anakuja kula kwangu jioni hatoi hela ukienda dukani utaona meseji nletee na soda beib. Nampenda sana tu ila mmh ananichosha kwakweli kwanza nashindwa kuelewa ana mapenzi ya kweli au ni huduma tu ndo zinazomuweka kwangu.

Baada ya kuanza uhusiano akaniambia kua ana demu wake, demu anamfanyia mshikaji vituko anataka kumuacha ila anadai anashindwa kwavile demu anakazi nzuri na kwao wanahela kuna vitu amepanga kumfanyia kwahiyo mimi nivumile tu soon akimaliza hivyo alivyomuahidi wataachana maana ananipenda zaidi nna heshima najua kulea mwanaume, nna sifa za kua mke.

Kama umeshindwa kujua huyo ni mtu wa aina gani,hata wewe ni tatizo ....!!!!!!
 
Embu jaribu kukaa chini kidogo halafu urudishe ufahamu wako. Naona kama ufahamu wako si ule ninaoujua. Mwambie uliyemwazima ufahamu wako akurudishie
 
Back
Top Bottom