Ana kwa ana na Dr.Ulimboka

Ana kwa ana na Dr.Ulimboka

Wewe humtakii mema, mwenzio kaenda jichimbia mbali na waliotaka kumtoa roho,sasa wabaya wake watajua yuko makelele .lol!
 
Mwishoni mwa juma hili,nilikuwa nchini Uganda kumsindikiza kigogo mmoja wa CCM na Serikali aliyekwenda kutoa mkono wa pole kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni ambaye hivi karibuni alifiwa na mama yake mzazi. Baada ya kuhani,tukarejea Kampala na miji ya pembezoni kutembeatembea na kupunga upepo.

Mimi niliamua kwenda kumtembelea 'classmate' wangu wa UDSM ambaye anahadhiri Makerere University. Ni Profesa wa Sheria pale. Tukazungumza vya kutosha na mwenyeji wangu ambaye alikuwa kwenye viunga vya chuo hicho. Baadaye nikamuaga kurejea nilipomuacha kigogo niliyemsindikiza aliyekuwa ananisumbua mno kwenye simu kama mtu asiyejiamini.

Wakati natoka viunga vya Makerere,nikamuona Dr.Stephen Ulimboka. Mimi hanijui kama akina Abed na Ighondu. Nikajipendekeza kumsalimu kwa kiswahili fasaha. Akaniitikia.Anasoma pale. Ana siha njema na mwenye furaha. Tukaongea na kufahamiana.

Anawashukuru watanzania wote kwa ujumla wao kwa kila sala,swala na nia njema kwake. Hana mengi zaidi ya shukrani.Amesema tukio lake limemsogeza karibu na Mungu na watanzania. Ilifika wakati alilia kwa furaha kwa stori zangu za huku Bongo na maisha kwa ujumla.

Dr.Ulimboka yu imara na anasonga mbele!

VUTA-NKUVUTE wa Lumumba Dar es Salaam

Hapo kwenye red kama story yako ni kweli na huyo kigogo ni mwajiri wako, basi wewe utakuwa ni mwajiriwa "mpumbavu". Inakuwaje unashindwa kuheshimu kazi yako? Boss wako akisoma hapa lazima akutimue kazi sijuhi utamlaumu nani?
Jifunzeni kuheshimu kazi zenu jamani!! Ndoo maana watu wanaamua kuajiri wageni kuliko midomo mirefu kama wewe.
 
Huyo aliyefiwa na mama yake ndio maandalizi ya uraisi manake huko ni kumaliza fedha za nchi tuu ,sasa mumemuona na si ajabu munataka kummaliza lakini dunia inaona
 
Kakuruhusu utoe habari zake au ni private umbea???
hujafanya vizuri katika hili....
 
topic_closed.png

tume elewana jamani
 
Hadithi za kufikirika,nenda kawasimulie wanao.
 
Mwishoni mwa juma hili,nilikuwa nchini Uganda kumsindikiza kigogo mmoja wa CCM na Serikali aliyekwenda kutoa mkono wa pole kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni ambaye hivi karibuni alifiwa na mama yake mzazi.
Jamani Mama yake Mseveni kafariki miaka 10 iliyopita (Source). Ni vyema tukawa na uhakika tunayoyaandika humu.
Esteri Kokundeka, President Museveni's mother died 14th November 2001 and yesterday, a memorial service marking 10 years since she died was held.
 
Hivi ni sahihi kumwaga jamvini taarifa binafsi za mtu? Halafu mtu mwenyewe ni Uli, ambaye ni muhanga wa watu wenye nia mbaya...
 
Umekwishawapa taarifa wenzako wakamalize ile kazi waliyotumwa na kushindwa kuimaliza?
 
VUTA-NKUVUTE said:
Mwishoni mwa juma hili,nilikuwa nchini Uganda kumsindikiza kigogo mmoja wa CCM na Serikali aliyekwenda kutoa mkono wa pole kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni ambaye hivi karibuni alifiwa na mama yake mzazi.

Jamani Mama yake Mseveni kafariki miaka 10 iliyopita (Source). Ni vyema tukawa na uhakika tunayoyaandika humu.
Esteri Kokundeka, President Museveni's mother died 14th November 2001 and yesterday, a memorial service marking 10 years since she died was held.

Pengine ilikuwa ni kumbukumbu ya kuadhimisha kifo cha mama yake baada ya miaka 10

Sosi: Kumbukumbu ya Kifo:Mama mzazi wa Yoweri Museveni

Au ilikuwa ni kwenye msiba wa Baba wa Yoweri, mzee Amos Kaguta

Sosi: Msiba wa Mzee Amos Kaguta, baba wa Yoweri Museveni
 
hivi kesi yake imefikia wapi? au ndio ameshazimwa na kontena la midola?

U never know bhana, hii hii sirikali ya kina Riz 1 yote yawezekana, lkn bora dk. angejivika tu tairi shingoni ili watakaobaki wawe huru baada ya kujua ukweli
 
Usikute na wewe mleta mada ulienda pale kumpatia kale kakitu unachoweka kwenye taulo kinakumaliza kabisa!!! Ha ha ha!! Nchi hii bwana!!!
 
Mwishoni mwa juma hili,nilikuwa nchini Uganda kumsindikiza kigogo mmoja wa CCM na Serikali aliyekwenda kutoa mkono wa pole kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni ambaye hivi karibuni alifiwa na mama yake mzazi. Baada ya kuhani,tukarejea Kampala na miji ya pembezoni kutembeatembea na kupunga upepo.

Mimi niliamua kwenda kumtembelea 'classmate' wangu wa UDSM ambaye anahadhiri Makerere University. Ni Profesa wa Sheria pale. Tukazungumza vya kutosha na mwenyeji wangu ambaye alikuwa kwenye viunga vya chuo hicho. Baadaye nikamuaga kurejea nilipomuacha kigogo niliyemsindikiza aliyekuwa ananisumbua mno kwenye simu kama mtu asiyejiamini.

Wakati natoka viunga vya Makerere,nikamuona Dr.Stephen Ulimboka. Mimi hanijui kama akina Abed na Ighondu. Nikajipendekeza kumsalimu kwa kiswahili fasaha. Akaniitikia.Anasoma pale. Ana siha njema na mwenye furaha. Tukaongea na kufahamiana.

Anawashukuru watanzania wote kwa ujumla wao kwa kila sala,swala na nia njema kwake. Hana mengi zaidi ya shukrani.Amesema tukio lake limemsogeza karibu na Mungu na watanzania. Ilifika wakati alilia kwa furaha kwa stori zangu za huku Bongo na maisha kwa ujumla.

Dr.Ulimboka yu imara na anasonga mbele!

VUTA-NKUVUTE wa Lumumba Dar es Salaam
Yoweri Kaguta Museveni alifiwa na baba yake na sio mama yake!
 
Back
Top Bottom