Keen
JF-Expert Member
- Sep 27, 2007
- 617
- 172
Mwishoni mwa juma hili,nilikuwa nchini Uganda kumsindikiza kigogo mmoja wa CCM na Serikali aliyekwenda kutoa mkono wa pole kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni ambaye hivi karibuni alifiwa na mama yake mzazi. Baada ya kuhani,tukarejea Kampala na miji ya pembezoni kutembeatembea na kupunga upepo.
Mimi niliamua kwenda kumtembelea 'classmate' wangu wa UDSM ambaye anahadhiri Makerere University. Ni Profesa wa Sheria pale. Tukazungumza vya kutosha na mwenyeji wangu ambaye alikuwa kwenye viunga vya chuo hicho. Baadaye nikamuaga kurejea nilipomuacha kigogo niliyemsindikiza aliyekuwa ananisumbua mno kwenye simu kama mtu asiyejiamini.
Wakati natoka viunga vya Makerere,nikamuona Dr.Stephen Ulimboka. Mimi hanijui kama akina Abed na Ighondu. Nikajipendekeza kumsalimu kwa kiswahili fasaha. Akaniitikia.Anasoma pale. Ana siha njema na mwenye furaha. Tukaongea na kufahamiana.
Anawashukuru watanzania wote kwa ujumla wao kwa kila sala,swala na nia njema kwake. Hana mengi zaidi ya shukrani.Amesema tukio lake limemsogeza karibu na Mungu na watanzania. Ilifika wakati alilia kwa furaha kwa stori zangu za huku Bongo na maisha kwa ujumla.
Dr.Ulimboka yu imara na anasonga mbele!
VUTA-NKUVUTE wa Lumumba Dar es Salaam
Conjured story but with purpose!!