Ana kwa ana na Dr.Ulimboka

Ana kwa ana na Dr.Ulimboka

Mwishoni mwa juma hili,nilikuwa nchini Uganda kumsindikiza kigogo mmoja wa CCM na Serikali aliyekwenda kutoa mkono wa pole kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni ambaye hivi karibuni alifiwa na mama yake mzazi. Baada ya kuhani,tukarejea Kampala na miji ya pembezoni kutembeatembea na kupunga upepo.

Mimi niliamua kwenda kumtembelea 'classmate' wangu wa UDSM ambaye anahadhiri Makerere University. Ni Profesa wa Sheria pale. Tukazungumza vya kutosha na mwenyeji wangu ambaye alikuwa kwenye viunga vya chuo hicho. Baadaye nikamuaga kurejea nilipomuacha kigogo niliyemsindikiza aliyekuwa ananisumbua mno kwenye simu kama mtu asiyejiamini.

Wakati natoka viunga vya Makerere,nikamuona Dr.Stephen Ulimboka. Mimi hanijui kama akina Abed na Ighondu. Nikajipendekeza kumsalimu kwa kiswahili fasaha. Akaniitikia.Anasoma pale. Ana siha njema na mwenye furaha. Tukaongea na kufahamiana.

Anawashukuru watanzania wote kwa ujumla wao kwa kila sala,swala na nia njema kwake. Hana mengi zaidi ya shukrani.Amesema tukio lake limemsogeza karibu na Mungu na watanzania. Ilifika wakati alilia kwa furaha kwa stori zangu za huku Bongo na maisha kwa ujumla.

Dr.Ulimboka yu imara na anasonga mbele!

VUTA-NKUVUTE wa Lumumba Dar es Salaam

Inawezekana ulionana naye but kwa 100% hakuweza kuwa muwazi kwako coz hakukuamini kuhusu kuwepo kwake Uganda..kama kweli ulionana naye Ni kweli ana siha safi na imeimarika but hasomi hapo Uganda may be alikudhani ndiyo wale wale. Dr Uli anaendelea na shughuli zake binafsi hapa hapa Bongo usiwaongopee wana jamvi. Nilikuwa naye mwezi wa kwanza na niliongea naye mambo mengi na hakugusia kuhusu kwenda kusoma Uganda
 
Mwishoni mwa juma hili,nilikuwa nchini Uganda kumsindikiza kigogo mmoja wa CCM..

Wakati natoka viunga vya Makerere,nikamuona Dr.Stephen Ulimboka. Nikajipendekeza kumsalimu kwa kiswahili fasaha. Akaniitikia. Ana siha njema na mwenye furaha. Tukaongea na kufahamiana.

Anawashukuru watanzania wote kwa ujumla wao kwa kila sala,swala na nia njema kwake. Hana mengi zaidi ya shukrani.Amesema tukio lake limemsogeza karibu na Mungu na watanzania. Ilifika wakati alilia kwa furaha kwa stori zangu za huku Bongo na maisha kwa ujumla.

VUTA-NKUVUTE wa Lumumba Dar es Salaam
Mimi nilimsindikiza gogo moja la CCM matibabuni India.

Nilikwenda kumtembelea lafiki yangu mmoja , wakati naludi kwa hoteli niliyofikia, nilimuona Dr. Ulimboka. Alisituka lakini alijikaza..tulisalimiana vyema, tulitia stori kwa saa limoja.

Alilia kwa fulaha za stoli za bongo...Anatibu vigogo katika hospitali maalufu huko India..Ile hospitali vigogo ya CCM inapenda.

Anamsalimieni sana.

Ukivuta usivute wa kutunga, Dal es Saraam.
 
tunasubiri akatoe ushahidi wake ICC maana mwendesha mashitaka mkuu wa ICC alipitapita Bongo!
 
Umepotea nija??? Huyo mlugaluga habari zake ziliisha!
 
Back
Top Bottom