Ana kwa ana na Dr.Ulimboka

Ana kwa ana na Dr.Ulimboka

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Mwishoni mwa juma hili,nilikuwa nchini Uganda kumsindikiza kigogo mmoja wa CCM na Serikali aliyekwenda kutoa mkono wa pole kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni ambaye hivi karibuni alifiwa na baba yake mzazi. Baada ya kuhani,tukarejea Kampala na miji ya pembezoni kutembeatembea na kupunga upepo.

Mimi niliamua kwenda kumtembelea 'classmate' wangu wa UDSM ambaye anahadhiri Makerere University. Ni Profesa wa Sheria pale. Tukazungumza vya kutosha na mwenyeji wangu ambaye alikuwa kwenye viunga vya chuo hicho. Baadaye nikamuaga kurejea nilipomuacha kigogo niliyemsindikiza aliyekuwa ananisumbua mno kwenye simu kama mtu asiyejiamini.

Wakati natoka viunga vya Makerere,nikamuona Dr.Stephen Ulimboka. Mimi hanijui kama akina Abed na Ighondu. Nikajipendekeza kumsalimu kwa kiswahili fasaha. Akaniitikia.Anasoma pale. Ana siha njema na mwenye furaha. Tukaongea na kufahamiana.

Anawashukuru watanzania wote kwa ujumla wao kwa kila sala,swala na nia njema kwake. Hana mengi zaidi ya shukrani.Amesema tukio lake limemsogeza karibu na Mungu na watanzania. Ilifika wakati alilia kwa furaha kwa stori zangu za huku Bongo na maisha kwa ujumla.

Dr.Ulimboka yu imara na anasonga mbele!

VUTA-NKUVUTE wa Lumumba Dar es Salaam
 
hadithi hadithi.hadithi njoo.uongo njoo utamu kolea...........
 
Tunashukuru kwa Mungu kumjaalia siha njema ili mwisho wa siku ukweli utabainika tu....
 
Ameridhia habari hizi uje kuzitoa public??
 
Mwishoni mwa juma hili,nilikuwa nchini Uganda kumsindikiza kigogo mmoja wa CCM na Serikali aliyekwenda kutoa mkono wa pole kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni ambaye hivi karibuni alifiwa na mama yake mzazi.
mkuu tugawane basi perdiem maana hali yangu ni mbaya sana ki-uchumi, nimekwama.
 
kidato cha 4 kila watoto100 watoto 60 wame_keep left round about
 
hivi kesi yake imefikia wapi? au ndio ameshazimwa na kontena la midola?
 
Back
Top Bottom