babu M
JF-Expert Member
- Mar 4, 2010
- 5,221
- 3,167
Mama Kilango aliposema atapiga kambi Moshi Mjini hakina tofauti na Mrema alichosema juzi kwamba atapiga kambi Moshi Mjini kuwavurugia Chadema.Chadema walikwenda jimboni kwa AK kufanya Mkutano ndio Mama Kilango akaamua kuwatishia na ndicho A Mrema analichofanya siku za karibuni baada ya kuona John Mrema ana mpush pembeni taratibu akaamua kutishia nae.Jambo JF Members
Leo hii nilifanikiwa kukutana na Mzee mmoja wa CHADEMA huku Moshi tukwa na mazzungumzo ya hapa na pale. Mojawapo ya mambo tuliyoongea ni kuhusu Mama Anna Kilango. Alidokeza tu kuwa atahakikisha anapiga KAMBI Jimbo la Moshi mjini ili ahakikishe kuwa linarudi CCM. Lakini tangu kampeni zimeanza huyu mama hatumsikii na wala hajaja kupiga kambi huku kama alivyoahidi. Juzi kwnye matangazo ya CCM Moshi walitanga wahutubiaji wa mikutano yao kwa siku husika wangekuwa Ole Sendeka na Anna Kilango lakini aliyefika ni Ole peke yake. Nilipomuuliza yeye (mzee wa CHADEMA) anafikiri kulikoni alinaambia kuwa maji yamemfika shingoni na kurudi bungeni ni ngumu kuliko maelezo. Amedai kuwa mama amewalaghai sana wapiga kura wake. hata kiwanda cha kusindika Tangawizi pia ni hewa hakuna kitu. Hali hii imemfanya Mama Kilango kukomaa jimboni kwake ili anusuru kiti chake ingawa matumaini ni hafifu sana.