Ana Kilango Malecela na Jimbo la Moshi Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ana Kilango Malecela na Jimbo la Moshi Mjini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eeka Mangi, Oct 10, 2010.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Jambo JF Members
  Leo hii nilifanikiwa kukutana na Mzee mmoja wa CHADEMA huku Moshi tukwa na mazzungumzo ya hapa na pale. Mojawapo ya mambo tuliyoongea ni kuhusu Mama Anna Kilango. Alidokeza tu kuwa atahakikisha anapiga KAMBI Jimbo la Moshi mjini ili ahakikishe kuwa linarudi CCM. Lakini tangu kampeni zimeanza huyu mama hatumsikii na wala hajaja kupiga kambi huku kama alivyoahidi. Juzi kwnye matangazo ya CCM Moshi walitanga wahutubiaji wa mikutano yao kwa siku husika wangekuwa Ole Sendeka na Anna Kilango lakini aliyefika ni Ole peke yake. Nilipomuuliza yeye (mzee wa CHADEMA) anafikiri kulikoni alinaambia kuwa maji yamemfika shingoni na kurudi bungeni ni ngumu kuliko maelezo. Amedai kuwa mama amewalaghai sana wapiga kura wake. hata kiwanda cha kusindika Tangawizi pia ni hewa hakuna kitu. Hali hii imemfanya Mama Kilango kukomaa jimboni kwake ili anusuru kiti chake ingawa matumaini ni hafifu sana.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kuna Daladala moja miaka hiyo lilikuwa limeandikwa.."Mwisho wa Ubaya ni AIBU"
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kumebakia takribani siku 20 tuingie kwenye chaguzi
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  ni mpiganaji mzuri na alikuwa anahitajika bungeni, lakini namba ya wabunge wa upinzani ni mhimu kuliko Anna Malechela
   
 5. d

  dotto JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  .. She is good but chama chake!!!
   
 6. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Kwa kuwa Mama Kilango anaipenda sana CCM kuliko wananchi,ninaomba wana Same wasimrudishe.Nashangaa sana kwa akina Ole Sendeka kufanya fitina dhidi ya Ndesamburo mtu aliyefanya mambo mengi Moshi Mjini,hivi wanachotaka wao ni idadi ya wabunge wa CCM kuongezeka na sio maendeleo,hawa si watu wazuri.
   
 7. S

  Selungo JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Heshima Mbele!

  Mimi nipo sehemu inaitwa Gonja Same Mashariki. Mambo ni magumu mkuu. Mama hachomoi mwaka huu. Hali inamwendea kombo ile mbaya. Kijibanda cha kuku anachesema ni kiwanda cha tangawizi duh! Watu wamekizira mkuu. Si lolote si chochote. Mama Kaboyoka ni kanyaga twende. Kila kona ni Kaboyoka. Taarifa nilizo nazo, AK ana mpango wa kumleta SM kusaidia kuokoa jahazi. Wapare wamesema sisi bwana ni Wachina wa TZ, hapa SM hapati kitu. Kama alishindwa ugogoni hapa ataipata. Na akifanya mchezo tunampigia LUKUNGA (yowe la kipare) watu wamtoe nduki.
   
 8. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Humjui vizuri, ni mchumia tumbo mzuri sana isipokuwa asipopata gawio kwenye dili za kifisadi basi hujifanya anatetea wanyonge!
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  hivi amepita-pita skuli eeh?
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  .
  Mkuu unazungumza kumleta SM kumsaidia? Aache utani bana. Maana hii ni sawa na magari mawili yameanza safari kutoka Dodoma kuja Dar, moja linapinduka pale kabaigwa jingine linakwama Chalinze. Sasa yule wa la Chalinze anapiga mahesabu ya kupata msaada wa kuvutwa na lililopinduka huko kibaigwa. IT IS DOUBIOUS.
  .
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hivi hii dhana ya upiganaji inaonekana is sooo loose..au ni mimi siielewi?
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Hvi Field Marshall yupo wapi?
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Siasa sazingine ni unafiki tu, Mtu kama ole Sendeka kuwapigia kampeni mafisadi nasikia alienda moduli, Moshi, arusha nilisikia amekuja kwa huyu mama Betilda ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Lowasa na wote tuna jua Ole sendeka alivyo na bifu na Lowasa au ndiyo ule usemi "funika kikombe mwana haramu apite" bado sija msikia Mwakyembe
   
 14. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mama Kilango akiwa Bungeni peke yake bila John Cigyemwisyu Malecela ni sawa na BBA ALL STARS Mwisho bila mchumba wake Merly Bwaaa haaaa haaaa haaaa... Wapi FMes.... Sauti ya Lusinde! Lol...
   
 15. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  na aibu imeshawqanyemelea ccm kutokana na ubaya wao
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Selungo,

  ..siamini kama Naghenjwa Kaboyoka anaweza kumshinda Anna Kilango ktk uchaguzi mkuu.

  ..kumbuka huu utakuwa mchuano wa tatu kati ya kina mama hawa wawili.

  ..mwaka 2005, Kaboyoka alishindwa ktk kura za maoni na Mama Kilango, baada ya hapo akahamia Chadema, na kushindwa kwenye uchaguzi mkuu.

  ..mwaka huu tena, Kaboyoka akarudi CCM akashindwa tena kwenye kura za maoni, sasa yuko Chadema anajaribu kitu kilekile alichoshindwa mwaka 2005.

  ..tatizo lingine ni kwamba Kaboyoka ameshindwa kwa margin kubwa sana ktk kura za maoni za CCM. hiyo ni dalili mbaya sana inayoelekeza kwamba hata ktk uchaguzi mkuu atakuwa na wakati mgumu. mara nyingi wanaoshinda baada ya kujitoa CCM ni wale ambao walishinda ktk kura za maoni lakini wakafanyiwa fitina kama ilivyotokea kwa Dr.Slaa mwaka 95.

  ..Dr.Slaa alikuwa Kilimanjaro, mbona sikusikia kama amekwenda kumpigia kampeni Kaboyoka?
   
 17. S

  Selungo JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  JokaKuu, HESHIMA MBELE!

  Kumbuka kwamba nyakati zote hizi, mama alikuwa anapata support toka kwa SM. Mfano kwenye kura zote za maoni zilizo endeshwa kwa wakati ule zilitumika nguvu za ziada na hasa mlungula wa waziwazi. kura za maoni za hivi karibuni wote tumeshuhudia jinsi rafu za wazi wazi zilivyokuwa zikichezwa na bila kuchukuliwa kwa hatua zozote. Kumbuka mama AK alilia hata pale mjengoni Dom. akitishia kwamba kama sisi em haitachukuwa hatua Same mashariki, basi damu itamwagika. Alikuwa anajua kwamba mwaka huu ngoma ni nzito.
  Same mashariki kuona kwamba mambo hayaendi kama walivyo taka, wakamwambia mama Kaboyoka hama nasi hatukuangushi.

  Kwa taarifa yako mimi nipo huku, hali halisi naiona na mambo yana mwendea AK mrama. Si aliahidi kwenda Moshi kumtoa Ndesapesa, mbona hajatoa mguu? Vaathu wameshtuka ile mbaya. Sasa sana anajivunia pale kwao Uzambara na kwa waMasai. Mamba walishashtuka baada ya kutoa ahadi zisizo tekelezeka.

  Si kila mahali Dr. wa kweli anaweza kwenda kwa kampeni. Ila kwa Kaboyoka tuna uhakika wa kushinda kwa kiwango cha juu.
   
 18. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ole sendeka nampenda sana lakini ni mnafiki MWANZO MWISHO. SHAME ON YOU OLE SENDEKA. umeshapita sasa mbona unapigana na watu wanaotaka kuliokoa taifa kutoka kwa wezi?
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Sasa ndugu yangu unampendaje manafiki?
   
 20. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dr wa Ukweli alifika Mamba Miamba, Ndungu, Same Mjini kwenye Kampeni hizi angalia ratiba au archives alihutubia na Vaathu walijaa sana kumsikiliza akasema wasimchague Vuvuzela Anna Kilango
   
Loading...