Ana Kilango Malecela na Jimbo la Moshi Mjini

Jambo JF Members
Leo hii nilifanikiwa kukutana na Mzee mmoja wa CHADEMA huku Moshi tukwa na mazzungumzo ya hapa na pale. Mojawapo ya mambo tuliyoongea ni kuhusu Mama Anna Kilango. Alidokeza tu kuwa atahakikisha anapiga KAMBI Jimbo la Moshi mjini ili ahakikishe kuwa linarudi CCM. Lakini tangu kampeni zimeanza huyu mama hatumsikii na wala hajaja kupiga kambi huku kama alivyoahidi. Juzi kwnye matangazo ya CCM Moshi walitanga wahutubiaji wa mikutano yao kwa siku husika wangekuwa Ole Sendeka na Anna Kilango lakini aliyefika ni Ole peke yake. Nilipomuuliza yeye (mzee wa CHADEMA) anafikiri kulikoni alinaambia kuwa maji yamemfika shingoni na kurudi bungeni ni ngumu kuliko maelezo. Amedai kuwa mama amewalaghai sana wapiga kura wake. hata kiwanda cha kusindika Tangawizi pia ni hewa hakuna kitu. Hali hii imemfanya Mama Kilango kukomaa jimboni kwake ili anusuru kiti chake ingawa matumaini ni hafifu sana.
Mama Kilango aliposema atapiga kambi Moshi Mjini hakina tofauti na Mrema alichosema juzi kwamba atapiga kambi Moshi Mjini kuwavurugia Chadema.Chadema walikwenda jimboni kwa AK kufanya Mkutano ndio Mama Kilango akaamua kuwatishia na ndicho A Mrema analichofanya siku za karibuni baada ya kuona John Mrema ana mpush pembeni taratibu akaamua kutishia nae.
 
siasa sazingine ni unafiki tu, mtu kama ole sendeka kuwapigia kampeni mafisadi nasikia alienda moduli, moshi, arusha nilisikia amekuja kwa huyu mama betilda ambaye ana uhusiano wa karibu sana na lowasa na wote tuna jua ole sendeka alivyo na bifu na lowasa au ndiyo ule usemi "funika kikombe mwana haramu apite" bado sija msikia mwakyembe

unafiki sio hulka ya "wa-metal"(kyela):a s 13:
 
Humjui vizuri, ni mchumia tumbo mzuri sana isipokuwa asipopata gawio kwenye dili za kifisadi basi hujifanya anatetea wanyonge!
Mkuu, jaribu kuhusisha akili yako unapochangia.Haya tueleze nini amekuwa akichumia tumboni?
 
Humjui vizuri, ni mchumia tumbo mzuri sana isipokuwa asipopata gawio kwenye dili za kifisadi basi hujifanya anatetea wanyonge!

Being vocal bungeni ni muhimu kuleta maendeleo na kusukuma serikali isilale, therefore She fits to became MP for second term. Actually she is better off compared to many opposition Mps who were 'kimya' in the parliament. While Anna who came from the ruling party was able to strongly challenge the government.
We need Anna again in Dodoma as an MP from Same
 
Nina support wapinzani kuwa na wabunge wengi kutoka na mchango wao wa bunge lililopita na vile vile nina support baadhi ya wabunge wa CCM kama AK na Mwakyembe kutoka na mchango wao wa bungeni.
 
.
Mkuu unazungumza kumleta SM kumsaidia? Aache utani bana. Maana hii ni sawa na magari mawili yameanza safari kutoka Dodoma kuja Dar, moja linapinduka pale kabaigwa jingine linakwama Chalinze. Sasa yule wa la Chalinze anapiga mahesabu ya kupata msaada wa kuvutwa na lililopinduka huko kibaigwa. IT IS DOUBIOUS.
.
bwa ha ha ha ha
 
JokaKuu, HESHIMA MBELE!

Kumbuka kwamba nyakati zote hizi, mama alikuwa anapata support toka kwa SM. Mfano kwenye kura zote za maoni zilizo endeshwa kwa wakati ule zilitumika nguvu za ziada na hasa mlungula wa waziwazi. kura za maoni za hivi karibuni wote tumeshuhudia jinsi rafu za wazi wazi zilivyokuwa zikichezwa na bila kuchukuliwa kwa hatua zozote. Kumbuka mama AK alilia hata pale mjengoni Dom. akitishia kwamba kama sisi em haitachukuwa hatua Same mashariki, basi damu itamwagika. Alikuwa anajua kwamba mwaka huu ngoma ni nzito.
Same mashariki kuona kwamba mambo hayaendi kama walivyo taka, wakamwambia mama Kaboyoka hama nasi hatukuangushi.

Kwa taarifa yako mimi nipo huku, hali halisi naiona na mambo yana mwendea AK mrama. Si aliahidi kwenda Moshi kumtoa Ndesapesa, mbona hajatoa mguu? Vaathu wameshtuka ile mbaya. Sasa sana anajivunia pale kwao Uzambara na kwa waMasai. Mamba walishashtuka baada ya kutoa ahadi zisizo tekelezeka.

Si kila mahali Dr. wa kweli anaweza kwenda kwa kampeni. Ila kwa Kaboyoka tuna uhakika wa kushinda kwa kiwango cha juu.

evava
 
Hizi SIASA MUNGU tu atusaidie maana wengi ni wanafiki sana.Katika hali ya kawaida Watanzania tunatakiwa kufikiria sana na kuchambua mambo kiundani.Hivi Mgombea anayewapigia Debe watu walio na kesi mahakamani tena za wizi wa pesa za Umma na kuwaita ni viongozi wazuri huyo ana akili timamu?Tena watu hawa wameshitakiwa na Jamhuri ambayo yeye ndo anaisemea,huyo ni mtu wa ajabu kabisa.Aidha haelewi anachofanya,Biblia inasema ni MPUMBAVU anhitaji kufundishwa au......nisaidieni. Nadhani tufikirie mara mbili mara tatu. Wakati wa kuchagua vyama umepita sasa ni kuchagua KIONGOZI BORA kwisha.

MUNGU Ibariki Tanzania.
 
Hata akishindwa ubunge hana shida sana. Anaweza kurudia tu ile kazi yake ya kuleta madawa ya kulevya lakini this time nafikiri atakua more clever hatakamatwa tena airport kama wakati ule. Anyway atakua former MP kwa hio that might lessen the scrutiny (and scare the security) at airport.
 
Jambo JF Members
Leo hii nilifanikiwa kukutana na Mzee mmoja wa CHADEMA huku Moshi tukwa na mazzungumzo ya hapa na pale. Mojawapo ya mambo tuliyoongea ni kuhusu Mama Anna Kilango. Alidokeza tu kuwa atahakikisha anapiga KAMBI Jimbo la Moshi mjini ili ahakikishe kuwa linarudi CCM. Lakini tangu kampeni zimeanza huyu mama hatumsikii na wala hajaja kupiga kambi huku kama alivyoahidi. Juzi kwnye matangazo ya CCM Moshi walitanga wahutubiaji wa mikutano yao kwa siku husika wangekuwa Ole Sendeka na Anna Kilango lakini aliyefika ni Ole peke yake. Nilipomuuliza yeye (mzee wa CHADEMA) anafikiri kulikoni alinaambia kuwa maji yamemfika shingoni na kurudi bungeni ni ngumu kuliko maelezo. Amedai kuwa mama amewalaghai sana wapiga kura wake. hata kiwanda cha kusindika Tangawizi pia ni hewa hakuna kitu. Hali hii imemfanya Mama Kilango kukomaa jimboni kwake ili anusuru kiti chake ingawa matumaini ni hafifu sana.

"Politics, like theater, is one of those things where you've got to be wise enough to know when to leave."
 
Kilango na wapiganaji wenzake watarudi bungeni kwa kura nyingi saaaana. Hamuendi majimboni kuona watu wanafanyaje.mfano mvomero ktk kura za maoni makalla amemshinda murad watu wakazira hali ikawa mbaya saaana. Jk akenda kama mar 2 hivi, nenda sasa hali shwari.kelele na jazba zinawaletea pressure ndio maana mnakufa fasta na umri mdogo.tar 31 oct tutawauliza wakiristooo mmeona faida za kampeni za makanisani? Ushindi wa kishindo lazima mtabaki na jesus slaa, sorry padre mzinifu slaa.
 
Selungo,

..Dr.Slaa alikuwa Kilimanjaro, mbona sikusikia kama amekwenda kumpigia kampeni Kaboyoka?

kwa kaboyoka ameenda ndesamburo amekaa wiki mbili na helikopta yake, sasa hivi wananchi hawasikii wala hawaoni kwa kaboyoka.
ni kama vile zitto anavyokwenda sehemu zingine badala ya slaa
baada ya anna kilango kupiga kambi mjini moshi, ndesa nae akarudisha majibu kwa kupiga kambi wiki mbili jimboni kwake same

hali ya upepo imebadilika sana na kilango anaogopa kurudi tena mjini moshi, inabidi ajilinde mwenyewe jimboni kwanza.
hata akienda mjini moshi hawezi kubadilisha chcochote. ushindi kwa ndesa ni 90%
 
Kilango na wapiganaji wenzake watarudi bungeni kwa kura nyingi saaaana. Hamuendi majimboni kuona watu wanafanyaje.mfano mvomero ktk kura za maoni makalla amemshinda murad watu wakazira hali ikawa mbaya saaana. Jk akenda kama mar 2 hivi, nenda sasa hali shwari.kelele na jazba zinawaletea pressure ndio maana mnakufa fasta na umri mdogo.tar 31 oct tutawauliza wakiristooo mmeona faida za kampeni za makanisani? Ushindi wa kishindo lazima mtabaki na jesus slaa, sorry padre mzinifu slaa.

hapo nilipoweka red - tafadhali weka maelezo - tuelewe vizuri (elaborate please)
 
ni habari njema kwani amekaa pamoja na mafisadi na hataki kutoka ccm bora tu aangushwe kwani naye ni mdandia hoja tu za upinzani.....angetoka huko aliko angeonekana wa maana
 
Kilango na wapiganaji wenzake watarudi bungeni kwa kura nyingi saaaana. Hamuendi majimboni kuona watu wanafanyaje.mfano mvomero ktk kura za maoni makalla amemshinda murad watu wakazira hali ikawa mbaya saaana. Jk akenda kama mar 2 hivi, nenda sasa hali shwari.kelele na jazba zinawaletea pressure ndio maana mnakufa fasta na umri mdogo.tar 31 oct tutawauliza wakiristooo mmeona faida za kampeni za makanisani? Ushindi wa kishindo lazima mtabaki na jesus slaa, sorry padre mzinifu slaa.

Alama za mtu mnafiki ni tatu
1.akiongea husema uongo
2. akitoa ahadi hatimizi
3. akiaminiwa hutenda hiana(haaminiki

kutokana na hayo point 3 hapo juu Ni nani au chama gani ambacho ni mnafiki/Kinafiki
AK kama analijua hilo ilitakiwa ahame chame huwezi ukawa kinyume na ufisadi halafu bado uko ndani ya mafisadi na ndio maana walinyamazishwa dodoma wakabaki kimya na kuruhusu mijadala ipite kiaina kwa ajili ya masilahi ya chama hivyo binafsi siwezi kumuamini

JK, AK na wote waliopo CCM ni wanafiki na wanahitaji kung'olewa isipokuwa Dr. Mwakyembe Pekee kwani walau anaweza kuusimamia ukweli bila kujali itkadi ya chama
 
Mimi nilikua nawasapoti sana kipindi walipojitangaza kama vinara wa kupambana na ufisadi wakiwemo Selelii,Ole Sendeka,Mwakyembe na wengineo.Walipopigwa biti na CCM wakiambiwa wanataka kukigawa chama,walinywea.
Matokeo yake Mafisadi kama Sofia Simba naye akajitangaza kupambana na ufisadi,wakharibu maana nzima yakupambana na UFISADI.
Mimi nasema twogopekama UKIMWI hawa watu WANAFIKI,waoweka maslahi ya chama mbele.
 
Humjui vizuri, ni mchumia tumbo mzuri sana isipokuwa asipopata gawio kwenye dili za kifisadi basi hujifanya anatetea wanyonge!
Kula tano.... watu wanapotea na sauti yake ya kulalamika....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom