Amuua mke wake kisa tamaa ya mali

Guantanamoh

JF-Expert Member
Jul 18, 2020
1,983
4,170
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 56 Mkazi wa Buzilayombo Wilayani Chato Mkoani Geita anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumuuwa Mkewe aitwaye Kasaka January (48) kwa kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake chanzo kikidaiwa kuwa ni tamaa za mali zilizokuwa zinamilikiwa na Mwanamke huyo Mchapakazi.

Kamanda wa Polisi Geita ACP. Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mpaka sasa Mwanaume huyo amekuwa akiishi nyumbani kwa Mama huyo "kiini cha tukio hili ni tamaa ya mali, nichukue nafasi hii kutoa wito kwa Jamii tutafute kwa jasho letu kila siku naendelea kusema kwamba matukio kama haya ni matukio ya kutokuwa na hofu ya Mungu"

RPC Safia amesema Mwanaume huyu amekuwa akiishi akiishi nyumbani kwa Mama huyo na Watoto ambao sio wa kwake na kwamba Mwanamke huyu alikuwa ni Mchakarikaji aliyemzidi Mume wake kipato ambapo mkasa uliibuka baada ya kupotea kwa betri za Mwanamke huyo ambazo hutumika kwenye shughuli za uvuvi.

"Baada ya betri kupotea Mama huyo alianza kutoa taarifa na kusema ameshamjua Mtu aliyezichukua betri hizo ndipo Mwanaume huyo akajishitukia na kuchukua uamuzi huo"

Source: Millard Ayo
 
Jamii ya Sasa imebadilika sana. Watu wanatamani vitu ambavyo hawajavitolea jasho. Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu mpambanaji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom