Amos Makala ang'aka

Amos Makala ang'aka

Tenga alipika supu nzuri,ila kaitia sukari ! Ndio basi tena. kaiharibu...
 
Sio mbaya tukifungiwa hata miaka 5 mbele,tukifunguliwa hawa wanaong'ang'ania watu wao watakuwa washachoka,na nchi itakuwa ishajipanga kisoka,tutasonga kivingine,wakati huo huo ligi yetu ya ndani inaendelea
mtu akikwambia Ndg. Jenerali Ulimwengu ni mtu mwenye vision usikatae kwa maana wakati akiwa BMT (?) wakati huo akina Ndolanga waligeuza FAT kijiwe chao cha kudumu na serikali ikiogopa kuingilia eti tusifungiwe. Yeye alisema kuwa tulikuwa hatufanyi lolote la maana katika michezo ukilinganisha na nchi zingine na akashauri tujitoe ili tujipange na tukija kuruhusiwa tuwe tumerekebisha mfumo wa uendeshaji hizi taasisi zetu za michezo.
Sasa fikiria, tangia wakati huo hadi leo bado tupo kwenye mdundiko tu na watu wanaiba pesa lakini maendeleo hayaonekani.
Ni bora tukafungiwa tu sasa ili tujifunze kitu

 
Fifa wameiandikia TFF azma yao kuiwekea kifungo Tanzania ikiwa 'amri' za serikali kwa TFF hazitafutwa. Nilishangaa kusikia redioni Amos Makala aking'aka kwamba Tenga ndie aliyewaambia FIFA kuandika barua hiyo wakati fifa wenyewe wanadai wamepata habari kuhusu uingiliaji wa serikali kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini. Nadhani Amos Makala ana mengi ya kujifunza kabla ya kujiamini sana.

eh! kumbe fifa wanafanya kazi kupitia magazet?
 
Dawa ya hawa Fifa ni kuanzisha chama kingine cha soka. Hii monoploy ndiyo inayowapa kiburi.

Kwenye mchezo wa ngumi ilikuwa hivyo hivyo. Kulikuwa na chama kimoja (WBO kama sijakosea). Na kwenyewe kulikuwa na monopoly ya kijinga kama hii tunayoiona sasa.

Lakini baada ya kuanzishwa vyama lukuki vya mchezo wa ngumi sasa kila bondia anachagua apiganie chama gani. Ndio maana leo unaweza ukasikia Francis Cheka ni bingwa wa dunia, Kaseba naye ni bingwa wa dunia na mwingine naye hata hajulikani lakini naye ni bingwa wa dunia. Hao wote unakuta ni mabingwa kwenye vyama vyao.

Sasa na hii monopoly ya Fifa (eti ina sauti kuliko serikali ya nchi husika...WTF) haiwezi kuondoka hadi hapo tutakapokuwa na vyama pinzani vya mchezo wa mpira wa miguu.
 
Wanachofanya tenga na kampani yake ni kupotosha kwa hali na mali hili swala,kwa kifupi kuna madudu yamefanywa na tenga ndio maana anamg'ang'ania Nyamalani amrithi ili aweze kuficha makosa ya tenga,Tenga anajua kabisa akiingia Malinzi au Wambura tff patanuka.
 
Tenga na Genge lake ndio watabeba msalaba kama tukifungiwa na FIFA.
Tenga ONDOKA TFF umeshakula vya kutosha!!!
 
Hivi kumbe FIFA wanasoma magazeti ya mwanaspoti,champion ata lile linaitwa kabumbu...doh magazeti yetu yametishaje.
 
hii ishu kina tenga wanataka kuficha maovu yao na mwakalebela leo kasema kuwa serikali imewaambia waitishe mkutano ili wajadili katiba mpya au wafanye uchaguzi kwa katiba ya zamani sasa kina tenga wao wanataka kuwekana wanajifanya serikali imewaingilia nakuiandikia barua FIFA yaani bongo bwana..

#MauozoYaTFF
Tatizo sio katiba ila Malinzi na watu wake wanaona lazima yeye aingie hata kama kwa taratibu walizojiwekea TFF wanaona hafai.
 
katiba zote za michezo zinasajiliwa na selikal,iweje leo selikal imeona ya tff haifai,kisha ikae kimya?AMOSI safi
Kusajili katiba haitoi fulsa kwa serikali kuingilia uendeshaji wa vyombo vilivyosajiliwa kwa namna serikali inavyoingilia TFF kuamrisha wala sio kushauri
 
Serikali imeeingilia TFF na Tenga kama kiongozi ni lazima awa taarifu FIFA kile kinachotokea kwenye tawi lake. Mpaka hapo sijaona tatizo la Tenga au mtu yeyote aliye ripoti hilo... Kama yeye Makala huwa atoi ripoti kwa aliye mteua basi hilo ni tatizo lake. Serikali yeote ikiingilia chama cha soka adhabu yake iko wazi sasa ana ng'aka nini?

Katiba ya TFF ifuatwe wakati huu wa uchaguzi watakaoingia wanaweza kuibadili...sio kubadili sasa katiba ili kuwaruhusu watu fulani kuapata madaraka. Mfano, Wambura aliacha nini TFF kila wakati anagombea? Mbona haku kabidhi ofisi pale alipo shindwa kwenye uchaguzi na Tenga?
 
FIFA yenewe inaendeshwa kiimla. Blatter amekuwa rais wa chombo hicho kwa miaka mingapi? mbona viongozi wengine hutawala kwa mihula miwili yeye zaidi ya mitatu. Turudi kwa TFF, Tenga ameonyesha udhaifu mkubwa hasa kipindi hiki ambacho alitakiwa kusimamia uchaguzi wa mtu atakayemrithi. Haiingii akilini kwa mtu aliyewahi kuongoza klabu kubwa kama Yanga na amwenyekiti wa chama cha soka cha mkoa na ambaye aliwahi kugombea uenyekiti wa TFF kabla akakosa sifa za kugombea uenyekiti 2013. Nasema haiingii akilini.

Kwa maoni yangu serikali inahaki ya kuingilia kile kinachofanyika ndani ya TFF maana kukitokea vurugu ni serikali hiyohiyo itakayoitwa kutuliza vurugu, pili TFF inatumia viwanja vinavyomilikiwa na serikali kama kile cha Taifa wananchi wakivurugana huko itakayopata hasara ni serikali. TFF haiwezi kuwa serikali kamili ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katiba yao lazima iendane na matakwa ya kikatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Tatizo ni tenga naisi amelewa misifa mingimingi,Serikali aijaingilia uendeshaji wowote pale TFF,ilichosema serikali ni kwamba katiba iliyopo kwa msajili ni ile ya 2006,kwa kawaida unapotunga katiba lazima isajiliwe na msajili wa vyama vya michezo nakila unapofanya mabadiliko yoyote lazima uyapeleke kwa msajili ili ayasajili ndivyo sheria zetu zinavyosema ata hili FIFA wanalifahamu,Tenga wao baada ya 2006 wamefanya mabadiliko kwenye katiba yao ikiwemo na kuiondoa BMT katika katiba yao ila awajawai kupeleka haya mabadiliko kwa msajili ili ayasajili kama sheria inavyosema,mwaka jana tena wakafanya mabadiliko mengine katika katiba yao ambayo ndio yaliunda kamati huru ya rufaa ya TFF na mengineyo,hapa walipeleka kwa msajili ila yalikwama kwa sababu za kisheria.
Sasa waziri mwenye dhamana na michezo kwa niaba ya serikali ametoa maagizo(sio kuingilia utendaji)TFF waitishe mkutano mkuu wajadiliane waipitishe mabadiliko ya katiba alafu uchaguzi mkuu uandaliwe au wafanye uchaguzi kwa katiba ya 2006 baadae viongozi wapya ndio wafanye mchakato huo wa katiba.Hivi vyote vinawezekana tatizo ni tamaa ya madaraka na kubebana katika familia ya mpira wa miguu kuanzia FIFA,CAF na TFF wanataka kuiga.FIFA inatambua kabisa mamlaka ya nchi husika na inaheshimu sheria za nchi,TFF aiwezi kuwa juu ya sheria za nchi zilizotungwa na bunge zinazomtambua msajili wa vyama vya michezo na BMT.
FIFA ina wanachama 209, yaani kila siku wanasoma magazeti ya nchi zote wanachama?jamani tuone mbele kidogo tusidanganyane, juzi nchini morroco kulikuwa na mkutano mkuu wa uchaguzi wa CAF viongozi wa TFF waandamizi walikuwepo na pia viongozi wote waandamizi wa FIFA walikuwepo sasa kwa sisi wabongo wa uchu wa madaraka,kubebana hivi fitna hapa aikupita?kwa nini barua ya FIFA kwa TFF wanasisitiza kuwa wamezipata hazari za tanzania kupitia vyombo vya habari?
Binafsi navyoelewa na jinsi jana mh makala alivyotoa ufafanuzi ni sahihi kuwa serikali aijaingilia uendeshaji wa TFF,TANZANIA sio koloni la FIFA bali ni mwanachama huru kama vilivyo vyama vingine.
 
Naunga na wale wanaosema bora tufungiwe, kuna nchi zilishawahi kufungiwa na ziliporudi zilirudi kwa kishindo, siukatai ukwelu kuwa tff ni taasisi huru na kwa katiba ya fifa, tff inawajika kwa fifa. sasa pamoja na uhuru huo serikali yetu isikubali kudharauliwa na fifa.Nasema afadhari kufungiwa kuliko kuendekeza huu ujinga wa viongozi wa tff kufanya madudu kwa kujiamini kuwa serikali haiwezi kuwaingilia, huu ni upuuzi kabisa, tff inaendeshwa kama familia fulani, leo hatumtaki huyu kwa kuwa si mwenzetu kesho hatumtaki yule kwa kuwa mwazo yake ni tofauti na yetu. ACHA TUFUNGIWE!
 
Mhe,makala piga kazi uyumbishwe na Tenga,wala usiogope FIFA.wenye akili tunatambu dhamira ya Tenga si nzuri hata kidogo,nia yake imekaa kihujumahujuma
 
Hana adabu kabisa huyu tenga niliwaambia watu amejaribu kujiosha kukataa agombei kuona aibu akatafuta means ya kufanya aishi milele mshenzi kabisa kabisa tulimwona wa maanaa kumbe bora ndolanga.....
 
Back
Top Bottom