Amini usiamini, anguko la CCM laja. Ni 2020...

Amini usiamini, anguko la CCM laja. Ni 2020...

CCM na itawale miaka mia nane na ikiwezekana itawale milele maana Tanzania hakuna watu wanaohitaji mabadiliko. Wameamini mabadiliko na maendeleo yanapatikana ndani ya CCM
 
Kamwambie huyo Mganga aliekuambia kuwa arudie kusoma rada zake upya...

CCM bado ina nguvu zaidi uijuavyo mkuu...
 
CCM ni kama maji kwa nyakati hizi na kwa miaka mingi ijayo. Kusema CCM itaanguka ni sawa na kusema...kuanzia sasa mito, maziwa, mvua, visima, chemichemi, mabwawa, bahari n.k. vitapotea, siyo kukauka, vitapotea ! Sasa nini kitabaki hapo hivyo vyanzo vyote vya maji vikipotea? Kwa kifupi, yawezekana haujui nini maana ya CCM yaani haujui msingi wa uwepo wa CCM hapa nchini kama chama cha siasa na kwa sasa kinaongoza awamu ya tano ya serikali yetu ya Watanzania. Nakushauri katafute ufahamu wa msingi wa uwepo wa CCM.
Walikuepo majabali wa siasa leo hii wako wapi? Unapaswa kujiuliza hili.
 
Nicolai Cesse cue wa Romania alikuwa na akili kama za jiwe,aliwatesa wananchi wake kwa miaka mingi sana,kila wakitaka kuandamana anawatisha,binadamu hufikia mwisho wa uvumilivu.
Wananchi wakaamua sasa tunaandamana,liwalo na liwe,ilikuwa ni Dec mwaka 1989,wananchi wakaingia mitaani ,kama kawaida jeshi la police likaingia kazini kuwapiga kuwatawanya na kuwakamata,hiyo haikusaidia.
Kila mshale wa saa ulipokuwa ukigonga ndo idadi ya watu kuingia mitaani ilizidi kuongeza,police walianza kuua,mkuu mimi nilikuwa Romania kipindi hicho haya niliyaona kwa macho yangu,nilikuwa na miaka 14,nilikuwa nimeenda huko nikiambatana na raia wa Australia waliokuwa wamenichukua kunisomesha,waliamua mwezi huo kula Xmas na mwaka mpya Romania, nitakuja kuweka thread maalumu humu kuhusiana na tukio lote nilivyoshuhudia Bucharest.
Police walizidiwa,wanajeshi nao wakaingia kazini,kufumba na kufumbua Romania ikaanza kunuka harufu ya mauti,maiti zilitapakaa kila kona,kila sehemu,risasi zilikuwa zinaua watu zikitoka kila sehemu,snipers,walikuwa wengi juu ya maghorofa,waliuliwa kama sisimizi.
Kilichonishangaza idadi ya watu haikupungua mitaani,ndo ilikuwa inazidi kuongezeka,vifaru vilitapakaa mitaani,mwisho wanajeshi wakaanza kurudisha silaha kambini na kuanza kuungana na wananchi kuandamana.
Nicolai na mkewe Helena wakakimbia kutumia Helicopter, bahati mbaya ilipofika mji wa Targovista ikaharibika,ikabidi walinzi wao wateke Taxi ili kutoroka nayo,walienda kama km 10 tu ikaishiwa mafuta,naam,walikamatwa na jeshi na kuchinjwa kwa risasi,
Natamani raisi john Joseph magufuli apite humu ajifunze kitu kikubwa sana humu
 
Binafsi nilidhani anguko la CCM ni kuhama kwa Mamvi kumbe unachokisoma mitandaon na kukiona kwenye TV kinasanifiwa na pesa zaidi lakini siyo uhalisia wa mambo! Ili kuiangusha taasis kama CCM unahitaji taasis kwa ajili ya kazi hiyo pekee na at least miaka kadhaa siyo eti Membe pekee aangushe CCM.Ni kama ANC tu au ZANU PF.It'll take time.
 
CCM ilikufa tangu 2015 sasahivi limebaki genge la wahuni, watekaji, watesaji na wauaji.
 
Jifunike hapo hapo kwenye blanket la historia, hata kina Gaddafi, Hosni Mubarak pia walijiaminisha hivyo hivyo. Saa hii watu wanaongea mengine. Hao walikuwa na nguvu kuliko hiyo ccm unayoitaja.
=====
tindo, Mkuu, nazungumzia CCM. Sizungumzii mwanachama/ mtu bali nazungumzia chama. Kwa mjadala ulioko mezani nazungumzia CCM. Mifano uliyotoa ya comrade Ghaddaf(R.I.P) na Hosni hawa walikuwa ama ni wanachama. Hawa ni watu na wala hawakuwa vyama. Narudia na zungumzia CCM. Kuijua CCM kuwa ni kama maji jibidiishe kuongeza ufahamu wa msingi wa uwepo wa CCM kama chama cha siasa hapa Tanzania.

Karibu.
 
Kwa taarifa yako ccm ni hicho cheo cha rais. Ccm yoyote iliyopo na zilizopita zilitegemea kofia ya urais kufanya siasa. Siku rais wa nchi hii akitoja nje ya ccm ndio utakuwa mwisho wa ccm. Kama sio madaraka ya rais, ni nadra ccm kupata wabunge halali 50%+. Hili kubali kataa kwamba bila rais kuwa mwanaccm hakuna namna yoyote ccm inaweza kuwepo. Halafu sio ccm tu, vyama vyote vikongwe barani Afrika vilifutika kama sio kuwa mahututi baada ya kupoteza dola (rais)
 
Jifunike hapo hapo kwenye blanket la historia, hata kina Gaddafi, Hosni Mubarak pia walijiaminisha hivyo hivyo. Saa hii watu wanaongea mengine. Hao walikuwa na nguvu kuliko hiyo ccm unayoitaja.
Raia wapi nzan misr na libya sio waoga na wanafiki kama wadanganyika
 
mtoa mada unaonekana ulitoa mada hii ukiwa umelewa ama ndoto. pia unaonekana ni mgeni sana katika siasa za CCM. CCM huimarika kipindi ambacho wapinzani hudhani kuna msuguano ama mgongano.CCM si kufa leo wala kesho , ni ya miaka mingi sana. kidumu chama cha mapinduzi
 
Dunia tunapita Hakuna kitachodumu milele acha kuota ndoto za mchana
 
Back
Top Bottom