DiasporaUSA
JF-Expert Member
- Aug 27, 2016
- 23,291
- 29,485
Marekani hawezi kumpa maagizo mchina au mrusi hata siku mojaKiuchumi ndiye nambari moja, akimuacha mbali mno wa pili-China. Kijeshi, ndiye kinara. Kiintelijensia, hakuna zaidi yake. Kiushawishi (kwakuwa anaongoza na kuwa na nguvu ya kiuchumi, kijeshi na kiintelijensia), hakuna anayemzidi ushawishi Marekani.
Mtu yeyote atakuwa sahihi akisema kuwa Marekani ndiye kiranja Mkuu wa dunia hii. Ndiye ambaye aweza kusema au kuagiza hili au lile na likatekelezwa. Ndiye ambaye anaweza kupeleleza bila kueleza na kufuatilia bila kufuatiliwa na akajua kila alitakalo. Nguvu ya kifedha!
Marekani hana mpinzani humu duniani kwasasa. Kila nchi husema na kufanya lakini inapofikia kuna mvutano na Marekani, nchi husika hujirudi na kusikiliza kwa makini Marekani anataka au hataki nini. Hata kama nchi husika hulifanya jambo kisiasa, haliwi mbali na akitakacho mwenyenguvu Marekani.
Inauma kukiri hili. Lakini, ndiyo ukweli wenyewe. Kiongozi wa Korea Kaskazini kukaa meza ya mazungumzo na Trump si jambo dogo. Hivi sasa anakula shushu. Kimyakimya. Amini nawaambia, pamoja na porojo zote tunazoweza kuambiana, hakuna kama Marekani kwa dunia tuliyonayo hivi sasa.
Pompeo, Jasusi mbobezi na Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Ujazusi la Marekani almaarufu kama CIA, Waziri wa sasa wa Mambo ya Nje wa Marekani ameshasema aliyoyasema kumhusu Makonda na Tanzania kwa ujumla. Tuseme yote lakini tukumbuke Marekeni ndiye mwenye nguvu.
Haitatusaidia barua ya Msando wala kuiweka hoja kando kama simu isiyo na bando. Marekani imefuatilia; imekusanya; imechambua na imetuambia. Ni kazi kwetu kusuka kusuka au kunyoa. Niaminini mimi, hakuna kama Marekani!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.