Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,660
- 46,349
Kwa ufupi ili uwe superpower lazima uwe na nguvu kubwa kiuchumi na uwezo wa "ku project" power/kuipeleka nguvu yako katika eneo kubwa zaidi la dunia kwa njia mbalimbali.
Taifa pekee lenye uwezo huu kwa sasa ni USA. Marekani ndilo taifa lenye vituo vingi zaidi vya kijeshi duniani, zana za kijeshi sehemu kubwa ya dunia, ndilo taifa linaloweza kupeleka majeshi sehemu nyingi zaidi za dunia pamoja na kupigana vita nyingi kwa wakati mmoja.
Katika suala la Uchumi ndilo taifa linaloweza kutumia vikwazo vya kiuchumi na nguvu ya pesa yake kama nyenzo katika kufanikisha maslahi yake katika sehemu kubwa ya dunia.
Pia suala la utamaduni wako kuweza kushawishi na kutawanyika sehemu kubwa ya dunia ni muhimu katika superpower. Utamaduni wa USA umezagaa dunia nzima.
China inakuja juu kwa uchumi kwa kasi ila bado haijafikia nafasi ya kuwa superpower hata hivyo haionekani kutumia sana jeshi katika maslahi yake na pia utamaduni wake haujaweza kuwa na ushawashi nje ya mipaka yake. China na India zinazokua pamoja na Urusi inayodidimia tunaweza kuziita ni great powers au regional powers.