Amezaa na mke wa mtu watoto watatu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amezaa na mke wa mtu watoto watatu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pape, Dec 4, 2009.

 1. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  wana JF,

  Kuna jirani yangu ambaye alikuwa anauhusiano wa kimapenzi na mke wa mtu. Ameniambia kwamba mwanamama huyo ndiye aliye mshawishi wawili hao wawe wapenzi bila kujali mumewe (ndoa yake). Baada ya miezi 5 mwanamama huyo alipata ujauzito na alipojifungua mtoto alifanana kabisa na rafiki yangu. Mume wa mwanamke wala hakuhoji!!

  Baada ya muda wapenzi hao waliendelea na kamchezo! Mama huyo akapata ujauzito tena na mtoto wa pili alifanana na huyu rafiki yangu! Huyu rafiki yangu yeye aliogopa na kuamua kuhama mji kwani alihofia usalama wake kwa mume wa yule mwanamama.

  Alikaa mkoa wa jirani takribani miaka mi tano! Rafiki yangu huyo baada ya muda alirejea tena jijini Arusha na kukuta katika kipindi chote hicho yule mwanamama na mumewe hawajapata mtoto mwingine.

  Yule mwanamama alianza tena tabia yake kwa kumhakikishia kwamba mumewe hana tatizo na hawezi jua kuhusu uhusiano wao! Punde yule mama akashika ujauzito! Alipojifungua mtoto wa tatu alifanana sana na huyu rafiki yangu.

  Ndipo huyu rafiki yangu aliamua kufuatilia kwakaribu ili ajue undani zaidi na ndipo alipogungua kwamba mwanamama huyo na mumewe walikuwa wamepanga mchezo wote kwani jogoo la mumewe 'haliwiki'

  Sasa wana JF, huyu kijana hajaoa lakini anauhakika wa 100% kwamba watoto wale watatu ni wake...

  Je, anayohaki ya kuwadai watoto hao kuwa ni wa kwake?

  Je, afanyeje ili aweze kutendewa haki?
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  JP kwanza tumpongeze huyu kijana kwa ujasiri na risk taking ya maisha yake aliyofanya kwa mambo mawili: 1.Kummega mke wa mtu pekupeku kwa nyakati hizi inahitaji ujasiri wa chizi. 2.Kummega mke wa mtu kwa ufundi mpaka akapata mtoto wa kwanza, ufundi ukaendelea, wa pili na mwisho wa tatu hebu fikiria kama huyo bwana asingekuwa na matatizo haya yanayofikiriwa kwamba siyo productive. Hao watoto anaofikiria kuwa dai leo ndio ingekuwa ticket ya kuzimu.

  Kifupi sana hiyo sehemu niliyoweka rangi nyekundu ni kwamba hakuna mwizi anaestahili hicho anachofikiria kukidai.

  Ni sawa na kumuingilia mtu usiku ukiwa mwizi, halafu kesho kwenda kudai kwamba ulidondosha kitambulisho, nadhani jibu unalo mshauri ipasavyo manake kama unampenda usije ukampoteza. Nina hakika mwenye mali ata revenge kwa style ya nyati aliyejeruhiwa ili kuficha hicho mlichokigundua kama wezi.
   
 3. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huyu kijana anastahili atupiwe mawe mpaka afe...
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mambo haya bwana...sasa alioaje mke wakati kumbe ni joka la kibisa?? kisheria hana haki ya kudai hao watoto...
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hana chake hapo yeye alikuwa anapanda DECI
  hee na kina mama mbona tuna hatari sana jamani ?
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  asithubutu kufanya hivyo.
  Aoe mke azae watoto wake mwenyewe yaishe.
  Hao watoto ni wa huyo jamaa mwenye mke, maana amewatunza na kuwafikisha popote walipo.
  Familia/Ndoa zinatunza vituko na vibweka vya ajabu sana...!
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,486
  Trophy Points: 280
  Mi namwombea kwa Mungu azae mwanamke MGUMBA! Shaitwain Ibilisi huyu!
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nina imani ulimaanisha aoe.
  Lakini xpin weka into consideration ushaitwani na ushawishi wa wanawake, na hasa huyu kwenye tukio. Huoni jamaa alikuwa anakimbia mkoa, na akirudi mwanamama yupo tu mzee, na anamhakikishia usalama!
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  mmh dua zako ni noma
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Huyo kijana ni mpumbavu sana!!!
   
 11. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  mkuu JP mshauri huyu jamaa aachane na hilo wazo la kuwadai hao watoto anaweza kujikuta anajifungulia kesi yeye mwenyewe ya kuiba mke wa mtu,
   
 12. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  yeye asubiri maumivu tuu kwani akioa watu watamsaidia
  ile mbaya. halafu kutokana na historia yake hatomuamini
  mkewe hivyo maumizi ndio yatamzidia.

  kubwa kuliko ndo hivyo kisha maliza mbegu zake za uzazi
  hivyo atakua akitoa povu tuu na akitaka watoto itabidi
  na yeye akubali kusaidiwa tuu lol
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  tena mpumbavu sana,
  unaweza zaa mtoto mmoja na mwanamke wa mtu..
  But sio watatu.....
  Halafu wewe huoi na kuzaa wa kwako,
  eti udai wa watu.very stupid.
   
 14. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nothing personal?
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  nothing at all.
   
 16. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ok, I was curious to know!
   
 17. Brutus

  Brutus Senior Member

  #17
  Dec 6, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ha ha.. eti jamaa alikuwa anapanda DECI... i like it!
  So funny!
   
 18. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkubwa Inawezekana jogoo akawa anawika na unamwaga mbegu lakini mbegu zikawa ni week.., haziwezi kurutubisha yai kwa kitaalamu wanaita oligospermia teh teh
   
 19. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kigogo,

  mshukuru Mungu hayajakukuta! siku yakikukta unaweza hata kuchukua bibi mzaa mama yako ukaishi nae kufunika kombe mwanaharamu aite!

  usalama wa mzee aliyeibiwa unategemea sana usiri wa mkewe waliyekubaliana aibe, vinginevyo akigundua kuwa katoa siri siri yao anaweza kjimaliza uhai wake.

  ni hivi huyo bwana ana matatizo ya kisaiklojia. ana taka watoto wawepo nyumbani afunike aibu anayoamini itampata ulimwengu ukigundua jogoo wake hawiki. inawezekana hata uamuzi wa kuoa aliufikia kwa sababu hii na alikubaliana na mchumba wake (mkewe wa sasa) khusu maisha watakayoishi baada ya ndoa.

  kijamii, hawa ni watu muhimu sana na inatakiwa serikali iangalie uwezekano wa kufanyia marekebisho sheria ya ndoa ili haki zao zilindwe kisheria dhidi ya wale "wapanda mbegu" kwani hawa ni watunzaji wazuri wa watoto na wanachangia maendeleo ya jamii kwani huwapeleka watoto shule na hata kuwarithoisha maadili, tabia njema na hata mali wanapofariki.

  kwa vile siri imeishatoka nashauri huyo mpanda mbegu ashauriane na hawara yake waape kuitunza siri hyo hadi mwisho wa dunia kwa usalama wa maisha a huyo mume na mpanda mbegu asithubutu kuwadai watoto. aoe mke wake azae wengine, huku akumtumaini Mungu.

  hakiuna lisilowezekana
   
 20. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  afadhali kidogo umeonyesha mawazo pevu, si hao wasemao "stupid" hakuna kitu kinachoutwa "stupidy" kwa watu wazima wenye akili zao!
   
Loading...