Amezaa na mke wa mtu watoto watatu!

Nimeona mitazamo tofauti mingine mizuri, mingine 50/50 na mingine inasikitisha. Kuna ambao wamekasirishwa sana na kitendo cha huyu kijana kiasi cha kushindwa kufikiri logically! Kabla ya kumshushia kila aina ya maneno kijana huyu, je ni kweli nyie sio wazinzi? Je ni kweli kati yenu mliomporomeshea maneno makali hamjawahi kuwa na mahusiano na walio katika ndo? Labda sababu kuu ya wengi wenu kuandika mliyoandika ni kutokana na nyinyi wenyewe kuwa katika ndoa na mmejiweka katika nafasi ya nyinyi kuibiwa, sasa kutokana na kutawaliwa na wivu mmehisi kuguswa na kuumizwa! Ningependa kushauri, safari nyingine msichague upande na mjaribu kufikiri logically by looking at the sitution in 3D. Shukrani kwa wale ambao wamejaribu kuangalia pande zote.

Kwa kuwa mimi ni mzinzi au mpumbavu, hainiondolei upumbavu wangu simply kwa kuacha kumuita mpumbavu mwenzangu hivyo... we dare talk openly!!! Manake ni kwamba kama ni upumbavu basi tutauita hivyo hata kama mimi pia naufanya kwani mimi pia ni mpumbavu

Mpumbavu ni mtu aliyepumbaa, soma kamusi utaelewa maana zaidi, mpumbavu ni clueless!!!

Kama na mimi nafanya haya, basi na mimi ni mpumbavu

Lets call a spade a spade and not a big spoon
 
wewe usiongee pumba humu.
Mimi ni mzinzi lakini kumzalisha watoto watatu mke
wa mtu halafu uanze kuwadai ni upumbavu,period,
yaani mtoto wa kwanza hukushtuka,
wapili je?
Mpaka wa tatu??????
Halafu watoto utawaambia nini??????
Kwamba nilikuwa nazini na mama yenu bila baba yenu kujua
ndo mkazaliwa???????

We huoni huu ni upumbavu mtupu.????????

Boss, nakubaliana na wewe, upumbavu ni upumbavu ...nothing personal!!!
 
Anaweza kudai watoto ni wa kwake kwa njia ya DNA na wakapewa jina lake kama baba kwenye birth certificate. Akasema hakujua kama mama aliolewa (Officially married) na kusema alimhadaa. Kwenye sheria atashinda kwa sababu hivi sasa Ulaya unapokwenda kuchukua birth certificate kama hutumii common surname (officially married) au baba hayupo basi mtoto atapewa surname ya jina la mama i.e. maiden name.

Mwambie atafute lawyer mzuri tu achukue watoto wake.
 
wana JF,
Ndipo huyu rafiki yangu aliamua kufuatilia kwakaribu ili ajue undani zaidi na ndipo alipogungua kwamba mwanamama huyo na mumewe walikuwa wamepanga mchezo wote kwani jogoo la mumewe 'haliwiki'

Sasa wana JF, huyu kijana hajaoa lakini anauhakika wa 100% kwamba watoto wale watatu ni wake...

Je, anayohaki ya kuwadai watoto hao kuwa ni wa kwake?

Je, afanyeje ili aweze kutendewa haki?

Sipendi sana kuamini unachokisema lakini inawezekena
ila huyo kijana ana roho ngumu kuliko muuza sumu Arabuni atanyongwa hata huko kuhama ni uongo mtupu sijui hii inaonyesha jinsi alivyojua kosa lake? cha kushangaza amerudia mara nyingi! Nashindwa kuutambua uelewa wa mama huyu kama kweli tatizo ni hilo....! maana sidhan yapo atakayemtuma mkewe akamegwe hadi mimba wakati zipo njia nyingine za upandikizaji?? Najiuliza kijana huyu akimegewa mkewe sijui itakuwaje mhhhh atakua mkali huyoooooo! mwambie wale si watoto wake kwa sasa!
tena asiende kuthubutu kudai ye si kidume apandikize kwa mkewe!
 
hivi hakuna sababu nyingine ya kuoana zaidi ya kuzaa?
kama hakuna uwezekano wa kuzaaa kwanini msifurahie matunda mengine ya ndoa,ambapo watoto ni moja wapo tu?

Teh teh teh! ni kwelei mwana va mutwa,lol nakugongea senks hapo
 
Huyu kijana ni jasiri sana......jasiri wa ujinga! Kama habari inavyosema kwamba mwenye mke ana matatizo, mimi najiridhisha kuwa suala la mke kutafuta watoto kupitia kazi za nje walilipanga ndani ya nyumba yao. Hivyo huyo mume anafahamu fika kuwa watoto sio wake (at least in biological sense).

Kwa hivyo mimi nadhani kwa ujasiri wa kijinga aliounyesha kuzaa watoto watatu kwa moyo mkunjufu, ni mkubwa zaidi kuliko kuwadai watoto hao! Risk ya kuwadai naiona ni ndogo mno........kuliko risk ya kuiba mke wa mtu na kumjaza mimba tatu!
 
Naweza kusema katika ile mimba ya kwanza labda kijana alihadaiwa, hakujua mwenzie alitaka kuzaa. Lakini hizo zilizofuata alifanya upumbavu mtupu. Kwamba huyo mama alitaka kuzaa nae na yeye akakubali kwa mara 2 zilizobaki akijua ni mke wa mtu, ina maana alijua wazi anazaa watoto wa kificho.

Na siri huwa zinatunzwa kwa gharama sana. Siku huyo mwenye mke akipata japo tetesi tu kuwa sperm donor wake aliyepaswa kuwa wa siri anataka kumuumbua hadharani, hataruhusu hilo litokee, na anaweza hata kumvizia amuue au hata amsingizie ujambazi ampige risasi au chochote cha aina hiyo. Usalama wa huyo kijana utapatikana kwa kukaa kimya kabisa na kukata mawasiliano yote na huyo mama, vinginevyo KIFO chamjia.
 
Huyo kijana ni mpumbavu sana!!!

Upumbavu wake ni upi? Mie namwona kama shujaa vile maana kutikisa nyavu (kunasisha mimba) siyo mchezo lazima uende futi za uhakika! Hongera kijana Acha mwanaume mwenzio akutunzie mbegu ya ukoo wako na nina uhakika kabla ya huyo mama kuaga dunia atawaambia ukweli watoto wake kuwa baba yao ni yupi?
 
Ulisoma biology wewe? Basi kama uliingia huko darasani hukuelewa kitu. Kutia mimba hakuhitaji ufundi wowote wala nguvu yoyote ya ziada. Kwa taarifa yako hata yule mwanaume anayemaliza tendo kwa nusu dakika tu anaweza kutia mimba. Manii zikiingia ukeni tu hata kama zimeingizwa na kidole zinaweza kuleta mimba.
 
Biology haisaidii chochote! Mimba zilianza kutungwa enzi na enzi kabla ya vijisomo vyako vya biology! Nenga na vimbegu vyako dhaifu kama utampa mwanamke mimba! Tena muulize mwanamke aliyemjamzito akupe michapo jinsi mshedede alivyopelekewa na kupata ujauzito! Au angalia physical exipirience ya wanyama Ngombe jike akipandwa huenda akapinda kwa masaa kadhaa ndiyo arudie hali ya kawaida! Bata dume huishiwa nguvu hapo hapo na kulala chini dk kadhaa! I'm real worried sijui hata kama una umtoto wa kusingiziwa!
 
Ulisoma biology wewe? Basi kama uliingia huko darasani hukuelewa kitu. Kutia mimba hakuhitaji ufundi wowote wala nguvu yoyote ya ziada. Kwa taarifa yako hata yule mwanaume anayemaliza tendo kwa nusu dakika tu anaweza kutia mimba. Manii zikiingia ukeni tu hata kama zimeingizwa na kidole zinaweza kuleta mimba.
hilo nalo neno!
 
Na siri huwa zinatunzwa kwa gharama sana. Siku huyo mwenye mke akipata japo tetesi tu kuwa sperm donor wake aliyepaswa kuwa wa siri anataka kumuumbua hadharani, hataruhusu hilo litokee, na anaweza hata kumvizia amuue au hata amsingizie ujambazi ampige risasi au chochote cha aina hiyo. Usalama wa huyo kijana utapatikana kwa kukaa kimya kabisa na kukata mawasiliano yote na huyo mama, vinginevyo KIFO chamjia.

Hata hivyo kama mwenye mke anajua bado huyu jamaa yuko hatarini bila hata kudai hao watoto. Ikumbukwe alichotaka jamaa ni watoto na sio mkewe kumegwa hivyo ili zoezi la kumegewa mkewe liishe na siri iendelee kuwepo anaweza kumueliminate kwa njia yoyote ile.

Mshauri rafiki yako akimbilie mkoa wa mbali zaidi na afute kabisa wazo la kudai watoto kwani hata akiwapewa hawawezi kuwa na mapenzi nae.
 
Si umesema kuwa mume na mke walipanga na mtia mimba anajulikana na huyoo mume. Ba mwizi aongee na huyo mama kama kuana uwezekano wa wote watatu kujadili hilo jambo ilakimsinngi watoto na wa muoajimwizi ana hatia
 
Sasa hapo anatafuta kukimbizwa mji kwa lazima kwa kubakwa. Jamaa hatavumilia hilo.
 
wana JF,

Kuna jirani yangu ambaye alikuwa anauhusiano wa kimapenzi na mke wa mtu. Ameniambia kwamba mwanamama huyo ndiye aliye mshawishi wawili hao wawe wapenzi bila kujali mumewe (ndoa yake). Baada ya miezi 5 mwanamama huyo alipata ujauzito na alipojifungua mtoto alifanana kabisa na rafiki yangu. Mume wa mwanamke wala hakuhoji!!

Baada ya muda wapenzi hao waliendelea na kamchezo! Mama huyo akapata ujauzito tena na mtoto wa pili alifanana na huyu rafiki yangu! Huyu rafiki yangu yeye aliogopa na kuamua kuhama mji kwani alihofia usalama wake kwa mume wa yule mwanamama.

Alikaa mkoa wa jirani takribani miaka mi tano! Rafiki yangu huyo baada ya muda alirejea tena jijini Arusha na kukuta katika kipindi chote hicho yule mwanamama na mumewe hawajapata mtoto mwingine.

Yule mwanamama alianza tena tabia yake kwa kumhakikishia kwamba mumewe hana tatizo na hawezi jua kuhusu uhusiano wao! Punde yule mama akashika ujauzito! Alipojifungua mtoto wa tatu alifanana sana na huyu rafiki yangu.

Ndipo huyu rafiki yangu aliamua kufuatilia kwakaribu ili ajue undani zaidi na ndipo alipogungua kwamba mwanamama huyo na mumewe walikuwa wamepanga mchezo wote kwani jogoo la mumewe 'haliwiki'

Sasa wana JF, huyu kijana hajaoa lakini anauhakika wa 100% kwamba watoto wale watatu ni wake...

Je, anayohaki ya kuwadai watoto hao kuwa ni wa kwake?

Je, afanyeje ili aweze kutendewa haki?

Kweli huu ulimwengu una mambo

Huyu kijana anastahili atupiwe mawe mpaka afe...

Mkuu, unakosea. Huyu si mwizi bali ni mtaalam na anapaswa kupewa uwaziri wa kina mama na watoto/jinsia kwa kazi yake ya kujituma na kuonea kina mama huruma mpaka anawazalishia watoto kwa ukarimu.
 
Hili sakata sijui liliishaje yarabi........ila mwanamke jasiri sana huyo.........kumfichia mtu aibu ni moyo wa kipekee sana.......
mkuu Pape........hebu njoo utupe mrejesho.........japo nina muda sijakuona............
 
Last edited by a moderator:
wewe usiongee pumba humu.
Mimi ni mzinzi lakini kumzalisha watoto watatu mke
wa mtu halafu uanze kuwadai ni upumbavu,period,
yaani mtoto wa kwanza hukushtuka,
wapili je?
Mpaka wa tatu??????
Halafu watoto utawaambia nini??????
Kwamba nilikuwa nazini na mama yenu bila baba yenu kujua
ndo mkazaliwa???????

We huoni huu ni upumbavu mtupu.????????

Okay, kama jamaa ni mpumbavu, huyo mwanamke aliye mke wa mtu aitweje?

Au yeye hana kosa kabisa kwa sababu yeye ni mwanamke na ni mke wa mtu na hivyo mwenye kosa hapo ni huyo jamaa aliyezini (na kuzaa na mke wa mtu na si kumzalisha) na mke wa mtu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom