birungi
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 391
- 16
baada ya kimya kingi sasa amerudi
alikua na kazi nyingi,ukweli mda haukuzidi
kama ujuavyo kimya kingi kina mshindo mkuu
birungi tena nimerudi, na habari nzito zilizo kuu.
katika pitapita zangu,mengi nimeyaona
nkafanya tafiti zangu,vidogo na vilivyonona
nkaona moja liwe langu,isije baadae kuibiana
si nkampata wa kwangu,sitaki na watu kushea
si kwamba wa juzijuzi,ni mda nimemtafiti
na haikuwa kubwa ajizi,malengo kufikia tamati
akapeleka pombe na mbuzi,hata vitenge vya bibi
hivo siku twazisubiri,MUNGU na ndugu wawe mashahidi.
nimeona ni jambo la kheri,rafiki zangu na wadau muwe nami
hata kama si kimwili,mawazo yenu na ushauri nauthamini,
naweza sema karibuni,ntafurahi tena kuwa nanyi.
birungi tena nimerudi,na habari nilizo nazo nimewapeni.