Mejja - Landlord (nyimbo na matukio)

Mejja - Landlord (nyimbo na matukio)

josephdeo

Member
Joined
Nov 23, 2015
Posts
96
Reaction score
208
• Mejja - Landlord

Kwenye hili song kutoka 254 hakuna chochote kinacho endana na story..

Ila kwa kuwa nimeisikia kwa dereva bajaji hapa basi imenikumbusha 2015. Experience ya kupanga kwa nyumba ya wenyewe huku Landlord akiwa kichefuchefu. KWANINI?!!

#NYIMBOnaMATUKIO

Around hiyo miaka nilikuwa nimerudi maskani na nilipata job town. Ilikuwa officiall job kabisa ambayo nilikuwa nikipokea salary. Hivyo kujipata huko kukafanya baada ya miezi miwili ya kazi nikashift kutoka kwa blaza ili kuanza maisha ya peke yangu. Gheto la wengi lilikuwa limenipitisha through alot na hivyo nilitaka kuwa mwenyewe!. Pia bro alikuwa na demand ya kutaka kuoa hiyo ni fact nyingine iliyoniondoa kwake.

Baada ya kuangaika huku na huku nikapata nyumba maeneo ya Bugarika, Bendera tatu. Nyumba ilikuwa mpya ila haikuwa na wapangaji yaani nilikuwa mimi peke yangu na maza house. Life langu lilikuwa lile la asbuhi na mapema kung'oa na kurejea mida ya saa tatu mpaka nne usiku. Pia kama kuna mpira wa usiku au wekeend basi nilikuwa silali hapo ghetto.

Sikuwa na mda kabisa wa kushinda ghetto na hata ungekuwepo ulikuwa mfinyu ila nilihama mara baada ya miezi miwili kati ya sita niliyolipia. Inshu ilianza kama maskhara tu bebe alikuja kujua crib linalo nihifadhi. Ila maza house akaniwashia eti ninunue mziki kwa kuwa wakati niko kwenye faragha zilisikika nyumbo ambazo wasanii wake hawafahamu.

Kabla ya round ya pili kuja bebe nilikuwa nimenunua kisabufa fulani cha kuzugia. Kweli mtoto alikuwa na vilio vya kero kwa wasikilizao ila hamasa kwa aliye juu ya kifua chake. Nikadhani tulimaliza kumbe haikuwa hivyo maza house alimindi tena na round hii ati akanitaka niwe nafanyia gest. Inshu ikawa solved kwani nilimpiga ban babe kufika pale.

Ukaibuka ugonvi mwingine na hiyo ni baada ya wana kuibuka wakiwemo ma blaza zangu. Maza house si akaniwashia moto eti kwanini naleta watu asiowajua nyumbani kwake. Alinifungia spika siku hiyo na ilikuwa aibu ki mtindo kwa sababu maza house alikuwa umri wa Bi. Mkubwa. Alafu namna alivyocharaza ni ile ya kutojiheshimu kabisa.

Hilo likaisha japo nilikasirika sana ila nikaliacha lipite na hayo yote yanatokea unaweza kudhani ulikuwa mda mrefu ila ni wiki mbili tu za kukaa pale. Siku moja bro alikuja kunishutua kuhusu mchongo fulani. Sasa ilikuwa asbuhi na maza house alikuwa na tabia ya kuwahi kuamka na kufanya usafi wa uwanja. Si akamzuia blaza kuingia eti hamfahamu. Hata nilipoingilia kuwa yule ni mgeni wangu bado maza house alizingua.

Tukaenda kuongolea nje na ghetto na Hilo swala nililinikwaza vibaya na nilishajaribu kumvumilia na nilikuwa nimechoka. Sasa nilikuwa nimepimika kwenye mizani yake kama alipanga kunipima. Kurudi ndani nikamuamshia plus kumcharazia. Sasa wakati namcharazia si nilimwambia kuwa "utaona na leo utaijua rangi yangu halisi".... We...we, bango likashikiliwa hapo kuwa nimemtishia maisha.

Mi sikujali nikaenda kuoga Kisha nikarudi ndani choo na bafu vilikuwa ndani ila havikuwa chumbani mwangu. Ile nimerudi chumbani mwangu naendelea kujiandaa ili nisepe town. Nisijue kuwa maza house katia lock kwa nje. Ile nimemaliza zangu navuta mlango nao umeng'ang'ania kwa nje ikawa vuta nikuvute mpaka nilipofahamu hilo kuwa nimefungiwa kwa nje.

Hichi kitu kilinifanya nikavimba kama kiboko maza house alikuwa kafikia hatua mbaya ambayo ilinichukiza. Gonga mlango wala hakuna anayefungua Wala aliyekaribu. Nikajua hakuna mtu kwa sababu palikuwa kimya. Ile nimechukua simu nimpigie blaza aje mara nasikia sauti za watu zikija. Kiongozi akiwa maza House huku akitamba na yule maza hakuwa anaweza kuongea kwa taratibu. Yeye alikuwa akipayuka hata kwenye maongezi ya kawaida.

Ila hakuwa mwenyewe kwa kuwa hatua zilikuwa nyingi na namna alivyokuwa akiongea ni kama alishitakia. Mara mlango ukafunguliwa na hapo uso kwa macho na mgambo akitaka kuingia ndani. Huwa sio mnyonge mimi nikashika ukosi wa jezi yake na kurudi naye nje kwa shari. Ikatokea purukushani kidogo ila ikaamuriwa na mwenzie aliyeonekana ni muelewa kidogo.

Taarifa walizokuja nazo Ni kuwa nahitajika kufika kwenye ofisi za mwenyekiti kujibu tuhuma zinazonikabili huko. Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kupata kesi ya mwenyekiti offcoz nilishapata kesi kibao ila nyingi zilikuwa kwa ngazi ya balozi na polisi. Kwa mwenyekiti tena kuja kukamatwa na mgambo kwa shari ilikuwa mara ya kwanza.

Kufika kule naambiwa nataka kumuua maza house kwa kitisho nilichompa. Tukakaa pale kwa namna ya usuluhisi kwa kuwa mjumbe mmoja kati ya wanne aliyekuwepo alikuwa mwanangu. Hapo ndipo nikajua ukubwa wa maneno niliyomwambia maza house. Baada ya mabishano ya masaa kadhaa tukakubaliana na tukasamehana ila jioni yake nilihama nikarudi kwa bro.

Maza house hakuamini yeye alidhani kuwa yameisha na tungeendelea kukaa pamoja na hapo ndipo nikajua kwanini ile nyumba haina wapangaji. Kila nikisia ila punch ya Mejja "landlord bhana!". Naishia kucheka tu na kumkumbuka maza house..
 
Mejja kitambo sana anakamua vema tafuta wimbo wake unaitwa Barua hutojutia
 
Mejja ana ngoma yake inaitwa "amejibamba kimeja".
 
Mejja anajua imba
Beat ilikuwa nzuri
Video very creative
 
Usinialibie siku bana landlord we ni tafashta(okonkwo)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom