Amerudi Kwenye Baraza, Mpiganaji Aliyepigana Hadi Risasi Ya Mwisho!

Kuna wafanyabiashara fulani wakubwa walitaka kuwatumia wanasiasa uchwara kumpaka matope prof. Muhongo ila Mungu kasimama katikati na karudi,kwa speed ya Magufuli jamaa huyu alihitajika kuliko inavyodhaniwa. Ni mweredi,mwadirifu na mchapakazi na ni mja kati ya watu wachache duniani waliobobea kwenye elimi ya miamba,asante Magufuli kwa kumuona tena
 
Dawasco kama hamumfahamu profesa ulizeni wezenu wa sayansi mambo ya njoo kesho muache
 
Previously he was a right choice in the bad era. Kwa sasa is a right choice in the right time/era
 
Wasiyempenda kaja.
Namkubali sana Prof.Muhongo
Kasi yake itaendana na ya Magufuli.
 
Tutampenda zaidi Muhongo wakati huu ambao ana boss (Magufuli) sahihi wanayeendana
 
Maggid Nadhani wewe unatoka jirani na Muhongo ndiyo maana unampamba mwizi mkubwa.
huyu Muhongo si ndiye aliyetuaminisha kuwa pesa hazijaibwa tena Bungeni?
pili huyu si ndiye aliye muamulu Rugemalila auze hisa zake kwa Seth Singh?
sasa usafi wake unatoka Mfukoni?
 
Watanzania mkimpenda mtu amuoni amsikii kisa mmemkubali magufuli bas ata kwa muhongo mshafall... ebu taja achievements za uyoo muhongo kwenye wizara yake usiandike vitu vingi wala uo uproffesor uckuzuzue
 
Zilikuwa ni njama za upinzani kumfifisha, sasa karudi kwa kishindo! Sio wa kuteuliwa tena na anaenda kukalia kile kile kiti chake pale jengo next na makao makuu ya KKKT ya Tz.
Safi sana!
 
Mmoja kati ya wazalendo wachache waliokuwa wanapambana waziwazi na waroho wa rasilimali zetu KWA manufaa ya taifa letu! Kati ya watu niliotamani kuwemo kwenye baraza LA mawaziri LA magufuli HUYU ni mmoja wao!Hakika unastahili Prof. Muhongo!Nakuunga Mkono Majjid!
 
Ndugu zangu,
Ni Sospeter Muhongo. Ni takribani mwaka mmoja uliopita, katika kipindi kama hiki, Profesa Muhongo, akiwa Waziri wa Nishati Na Madini, alijikuta kwenye mapambano makubwa na makali yenye kuhusiana na maslahi ya kiuchumi.

Profesa Muhongo alisimama upande wa watu na taifa. Hakuwa na media ya kumsaidia. Hata hivyo, Muhongo alipambana kijasiri hadi risasi ya mwisho. Ikafika mahali, na kwa maslahi ya taifa, alilazimika kuingia handakini.

Kwenye Baraza Jipya lililotangazwa leo, bila shaka, Sospeter Muhongo ni mmoja wa wateule wenye furaha kubwa ya ' ushindi' . Kwamba ameonyesha kuwa ni mtu asiyekata tamaa. Aliamua kujimbia handakini. Kimyalimya akapigana jimboni kwake kuomba kura za wananchi, maana, alikuwa mbunge wa kuteuliwa tu.

Binafsi nimefurahi kumwona Sospeter amerudi tena. Niseme wazi, nilimkubali Sospeter Muhongo kwa utendaji wake na misimamo yake isiyoyumba. Alisimamia alichoamini ni ukweli na ni kwa maslahi ya umma.

Naaomba hapa nikumbushie nilichoandika Desemba 17, 2014 kwenye ukurasa wangu wa FB;
"Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema ameshajiuzuru. Ni hekima na busara kwa Jaji Werema kuchukua uamuzi huo. Maana, alikiri hata ndani ya Bunge, kuwa ni kweli kuwa alitoa ushauri wa kuidhinisha fedha kutolewa. Hata kama ni kwa kuchelewa, bado ni uungwana, kwa Jaji Werema kuwajibika kwa ushauri aliutoa na hata kuleta mtafaruku wa kisiasa na kijamii katika nchi.

Hata hivyo, kuna hamu, miongoni mwa wanajamii, kuwa na kichwa cha Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, nacho kibiringike kwenye vumbi. Hamu hii inaonekana kupandikizwa pia kwenye jamii ili kutimiza malengo ya wachache wenye kutaka Muhongo ang'oke kwa sababu zao, ama za kisiasa au kiuchumi.

Maana, mtu mzima ukiisoma ripoti ya CAG na kisha PAC, na kisha ukiliangalia jambo hili kwa macho maangavu, na kwa kuyatafakari mazingira , fursa na changamoto tulizonazo, kama taifa, kwenye sekta ya madini na nishati, na kwa kuangalia mwenendo wa harakati za mataifa makubwa kwenye kupigania rasilimali muhimu kama gesi na mafuta, huoni mantiki ya Tanzania yetu, pamoja na mapungufu ya kibinadamu aliyonayo Profesa Muhongo, kufanya maamuzi ya kujitia hasara kama taifa, kwa kumtoa kafara mmoja wa Watanzania wachache wenye weledi wa kupigiwa mfano kimataifa kwenye sekta ya madini kwa kuegemea mapendekezo ya ripoti ya PAC iliyoandaliwa na wanadamu wenye utashi wenye kutofautiana na iliyothibitika, kuwa nayo ina mapungufu. Na tuwe na ujasiri, kwa maslahi ya taifa, kuyapa mgongo hata yale ambayo, kwa matashi yetu ya kisiasa hata kijamii, tungependa yawe ili tunufaike au tufurahi tu, basi.

Ningelikuwa miongoni mwa wenye kutaka Profesa Muhongo ang'oke, kama ripoti ya CAG ingeonyesha uhusika wa moja kwa moja wa Profesa Muhongo kwenye sakata la Escrow. Lakini, ripoti ya CAG haionyeshi hivyo. Na katika kufanya maamuzi, lililo muhimu ni kutompendelea mtu au kumuonea. Hivyo, ndio maana ya kutenda HAKI.

Niliouelezea hapo juu, ni mtazamo wangu unaotokana na kusumwa na mapenzi kwa nchi yangu niliyozaliwa, basi."

Maggid Mjengwa,
Iringa.

attachment.php

we unatafuta mzungu wa kukuoa
 
Huyu mzee ni kati ya wanasiasa wachache waliokutwa na fitna za unafiki wa Zitto & co
 
Back
Top Bottom