Amerudi Kwenye Baraza, Mpiganaji Aliyepigana Hadi Risasi Ya Mwisho!

Ndugu zangu,
Ni Sospeter Muhongo. Ni takribani mwaka mmoja uliopita, katika kipindi kama hiki, Profesa Muhongo, akiwa Waziri wa Nishati Na Madini, alijikuta kwenye mapambano makubwa na makali yenye kuhusiana na maslahi ya kiuchumi.

Profesa Muhongo alisimama upande wa watu na taifa. Hakuwa na media ya kumsaidia. Hata hivyo, Muhongo alipambana kijasiri hadi risasi ya mwisho. Ikafika mahali, na kwa maslahi ya taifa, alilazimika kuingia handakini.

Kwenye Baraza Jipya lililotangazwa leo, bila shaka, Sospeter Muhongo ni mmoja wa wateule wenye furaha kubwa ya ' ushindi' . Kwamba ameonyesha kuwa ni mtu asiyekata tamaa. Aliamua kujimbia handakini. Kimyalimya akapigana jimboni kwake kuomba kura za wananchi, maana, alikuwa mbunge wa kuteuliwa tu.

Binafsi nimefurahi kumwona Sospeter amerudi tena. Niseme wazi, nilimkubali Sospeter Muhongo kwa utendaji wake na misimamo yake isiyoyumba. Alisimamia alichoamini ni ukweli na ni kwa maslahi ya umma.

Naaomba hapa nikumbushie nilichoandika Desemba 17, 2014 kwenye ukurasa wangu wa FB;
"Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema ameshajiuzuru. Ni hekima na busara kwa Jaji Werema kuchukua uamuzi huo. Maana, alikiri hata ndani ya Bunge, kuwa ni kweli kuwa alitoa ushauri wa kuidhinisha fedha kutolewa. Hata kama ni kwa kuchelewa, bado ni uungwana, kwa Jaji Werema kuwajibika kwa ushauri aliutoa na hata kuleta mtafaruku wa kisiasa na kijamii katika nchi.

Hata hivyo, kuna hamu, miongoni mwa wanajamii, kuwa na kichwa cha Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, nacho kibiringike kwenye vumbi. Hamu hii inaonekana kupandikizwa pia kwenye jamii ili kutimiza malengo ya wachache wenye kutaka Muhongo ang'oke kwa sababu zao, ama za kisiasa au kiuchumi.

Maana, mtu mzima ukiisoma ripoti ya CAG na kisha PAC, na kisha ukiliangalia jambo hili kwa macho maangavu, na kwa kuyatafakari mazingira , fursa na changamoto tulizonazo, kama taifa, kwenye sekta ya madini na nishati, na kwa kuangalia mwenendo wa harakati za mataifa makubwa kwenye kupigania rasilimali muhimu kama gesi na mafuta, huoni mantiki ya Tanzania yetu, pamoja na mapungufu ya kibinadamu aliyonayo Profesa Muhongo, kufanya maamuzi ya kujitia hasara kama taifa, kwa kumtoa kafara mmoja wa Watanzania wachache wenye weledi wa kupigiwa mfano kimataifa kwenye sekta ya madini kwa kuegemea mapendekezo ya ripoti ya PAC iliyoandaliwa na wanadamu wenye utashi wenye kutofautiana na iliyothibitika, kuwa nayo ina mapungufu. Na tuwe na ujasiri, kwa maslahi ya taifa, kuyapa mgongo hata yale ambayo, kwa matashi yetu ya kisiasa hata kijamii, tungependa yawe ili tunufaike au tufurahi tu, basi.

Ningelikuwa miongoni mwa wenye kutaka Profesa Muhongo ang'oke, kama ripoti ya CAG ingeonyesha uhusika wa moja kwa moja wa Profesa Muhongo kwenye sakata la Escrow. Lakini, ripoti ya CAG haionyeshi hivyo. Na katika kufanya maamuzi, lililo muhimu ni kutompendelea mtu au kumuonea. Hivyo, ndio maana ya kutenda HAKI.

Niliouelezea hapo juu, ni mtazamo wangu unaotokana na kusumwa na mapenzi kwa nchi yangu niliyozaliwa, basi."

Maggid Mjengwa,
Iringa.

attachment.php

Tanzania's next president Profesa Muhongo
 
Sasa kutoka mkoa wa Mara angemchagua nani,kwani wabunge wa CCM wa huko Lameck Airo ndio usiseme,Mzee Mkono umri umempita kwa hiyo aliyebaki ni Muhongo,imebidi tu mgeni usiyempenda akaribishwe sebuleni na kupewa chumba,baado naona kuna kasoro kubwa kwenye kumchagua Muhongo,hata kama ni mtendaji mzuri lakini anastahili kuwaheshimu wananchi wake ambao ndio wanaomlipa mshahara,hii ya kudai kupigana hadi risai ya mwisho na eti ni shujaa huku ni kujikomba kwa Maggid,kwa mwandishi mbobezi kama Maggid kuandika kwa kujipendekeza namna hii ni kujidharirisha,vinginevyo kama ana maslahi binafsi kutoka kwa Muhongo,pia kudai eti Chadema mbona walimsimamisha Lowasa huo ni umbumbu,kwanini tufanye tena yaleyale tuliyokuwa tunayapinga kwa wana Chadema kuhusiana na Lowasa?huu ni undumila kuwili.
 
Profesa Muhongo alisimama upande wa watu na taifa. Hakuwa na media ya kumsaidia. Hata hivyo, Muhongo alipambana kijasiri hadi risasi ya mwisho. Ikafika mahali, na kwa maslahi ya taifa, alilazimika kuingia handakini.

Maneno mazito hayo Maggid:hand:

Ifike wakati wamiliki wa Media wasomeshwe matumizi yenye mashiko ya hivyo vyombo vyao. Swali la kipima joto jana lilikuwa:

Wanaotumia vyombo vyao vya mawasiliano, kupotosha umma na kwa faida ya maslahi yao hata kama ni kwa gharama za kudumaza maendeleo ya Taifa, wahukumiwe kama wahujumu uchumi?

Matokeo:

95% wamesema Ndiyo; 3% wamesema Hapana na 2% wamesema Sijui kama boss ameliruhusu swali hili!
 
Sospeter ni jembe lilo wekwa makali baada ya kuwa nje ya baraza. Hongera rais kwa uteuzi wa huyu jemadari
 
Nakubaliana na wewe Maggid. Professor Muhongo ni mtu makini na mzalendo halisi. Hongera Prof. Muhongo kwa kuwaumbua wabaya wako na hasa yule anayemiliki vyombo vingi vya habari nchini na ambaye ni kuwadi wa mabeberu.

Hahahahahahah Duhh nimecheka sana mkuu
 
Prof.S.Muhongo ni mchapakazi kwelikweli na mambo yaliyomkuta ni kama ajali tu ya kisiasa. Nampongeza Rais wetu kwa uteuzi huu na nadhani sasa ule umeme ambao ulikuwa unakuja vijijini kazi itaanza; maana mambo yalisimama kabisa baada ya Muhongo kuondoka.
Yaa umenena vyema mkuu nguzo nying zilizokuwa zinaozea chin sasa zitapata ahueni baada ya jamaa kurudi hope ataenda na speed ya escape velocity na asiwasikilize wapiga majung wao sik zote in kupinga tu at a visivyopingika
 
i like Prof. Muhongo. tunarudi kwenye zama za kufungiwa umeme kwa wiki moja.....maana iliishafikia hadi miezi mitatu kwa sasa
Nimeomba kufungiwa umeme ni miezi miwili sasa, ngoja jamaa aspishwe nadhani watanitafuta wenyewe!
 
Sijui kwa nini nikimfikiria Muhongo nawaza tu kupanda kwa bei ya umeme hadi kupata unit 8 kwa 10000 mwanzoni mwa mwezi. Shida yangu ni hiyo kila ninaponunua umeme namuona Muhongo!

Jamaa alitwambia bei ya umeme itashuka baada ya Mitambo ya kinyerezi kufanya kazi
 
Back
Top Bottom