Amepata kazi Bunda mkoani Mara. Vipi wenyeji wa huko?

Kibara ( chibhala) ni sehemu nzuri sana. Ni mji mdogo wa kibara ndio yalipo makao makuu ya wilaya ya Bunda Dc( vijijini). Km kama 45 hivi kutoka Bunda mjini iliko njia panda ya kwenda Tarime, kenya, Musoma na kurudi Mwanza. Kutoka bunda kwenda kibara unatembea kando kando ya ziwa na hata kibara yenyewe ipo ziwani( ziwa victoria), ni sehemu yenye huduma zote mfano hospital ya mission, usafiri wa uhakika muda wote, maji, umeme nk
Barabara ni ya rami. Wenyeji ni wajita na sasa kuna mchanganyiko na makabila mengine na ndio wenye pesa samaki ikiwa ni biashara kubwa. Wajita ni watu wema, hawana makuu. Uchawi inategemea, kama wewe ni mchawi basi nikwambie kuwa upo, kama sio basi hakuna uchawi. Kibara ni maeneo ya nyumbani, kwa sasa niko mojawapo ya mikoa ya pwani, ila nikipata wasaa, ni kheri nirudi nyumbani kuishi na kufanya kazi. Karibu sana Chibhala
Chasubu,waongera mawe
 
Karibu sana, ni pazuri ila kukame sana. Samaki wakutosha wapo. Ukifika fanya yako huku unajua umewakuta watu.
 
Uchawi kila sehemu upo.Ukiugopa ndo unakudhur

Umeelezea vizuri sana mkuu,,sema Apo kwenye Barbara Kuna kipande kidogo Cha kutoka bunda mjini kuja kibara ni Barabara ya vumbi..Wenyeji tupo tunamkarbisha sana kibara nina miaka 2 hapa.
Module a.. Aice ntakutafta nipo nansio huku..kuna uwezekano nikaja pia hapo mkuu mwisho wa mwezi kuna harakat nataka kuja kufanya pia kibara
 
Karibu sana bunda, kibara ni sehemu nzuri hali ya hewa ni nzuri, samaki wapo wa kutosha kwa sasa nipo ya moto bar napata moja moto moja baridi
 
Mapanga shaa ni Tarime,Mara sio Tarime kuna makabila mengi tu waungwana.
Wengi tumekosa chaguo la moyo wetu kisa tunatoka Mara wote tunajumuishwa na washenzi hata ukiwa muungwana
Huyo alikua hakupendi...! Wala sababu sio unatokea Mara, akikupenda haangalii unatokea wapi...! Mrisyaaa umeniuzi sana
 
Pako vizuri mkuu we mwambie akapige kazi tulijenge taifa. Hakuna sehemu isiyokosa changamoto zake hapo wenyeji ni wajita, samaki wa kutosha na barabara safi kabisa muda wowote usafiri wa kurudi Mwanza mjini upo, Wenzake wamepelekwa Bukoba huko vijijini hata mtandao hakuna sembuse yeye Kibara.!
Wasukuma wengi Kibara
 
Huyo alikua hakupendi...! Wala sababu sio unatokea Mara, akikupenda haangalii unatokea wapi...! Mrisyaaa umeniuzi sana
Alisema tabia ngozi ukizingatia nilikuwa kusini,bora kanda za Kati, kaskazini nk wanajua kutenganisha Tarime na Mara
 
Aice bukoba kuna sehemu nilienda piga kazi panaitwa mrusagamba kule nahisi wangepewa tu Burundi maana hata mtandao wanaotumia ni lumitel, kwahyo ukisikia MTU anapakandia kibara lazma uhisi ana kaupungufu sehem frani, Kigoma ndo janga lingne tena
Wahaya ni wanafiki Sana, na kheri kuish na mchawi kuliko mnafiki
 
Ajiandae kupigwa majungu sana. Watoto wa kike hapo wana kawaida ya kuzalia nyumbani (single mothers). Kuna vijana wana vijisenti senti hapo basi ni waharibifu sana kwa watoto wa kike. Kuna soko hapo wanauza samaki, matunda na vyakula vinginevyo. Kama mdogo wako ni mwelewa/amekomaa basi ataishi tu bila matatizo.
Kwa hiyo pia ajiandae kupigwa pipe au?
 
Ni kwao na George masatu tu Kama wewe ni shabiki wa kolofc utajua. Pako poa mkuu ni sehemu imechangamka kiasi chake. Huduma zote ziko karibu na usafiri kwenda popote upo wa kutosha. Atapapenda na anaweza asiludi uko kwenu. Karibu sana dada niko busambala kijiji kinachofuata kutoka kibara kama unaenda ukerewe.
bado gineri ipo?
 
Mapanga shaa ni Tarime,Mara sio Tarime kuna makabila mengi tu waungwana.
Wengi tumekosa chaguo la moyo wetu kisa tunatoka Mara wote tunajumuishwa na washenzi hata ukiwa muungwana
Mwanamke akikupenda kakupenda Tu Mimi mbona nikitongoza dem wowote na mwambia Mimi kwetu Tarime na hani katai, kijana hacha kuwa muoga jiamin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka niliwahi fanya kazi hapo kibara bunda kupeleka mradi wa umeme palikuwa vyema sana pamoja na kwamba ilikuwa zamani sana ila naamini nia yake ni kufanya kazi basi amtumainie Mungu na afanye kazi kwa juhudi na maariofa lazima malengo yake yatatimia bila ya shaka.
 
Back
Top Bottom