Vilio vimekuwa vingi mno hawa viumbe sijui nini kimewatokea yani kugawa utamu kwao sio jambo la aibu tena wala hawaogopi chochote, kuna mmoja alijitamba mbele yangu eti iyo meza hapo wote nishapita nao'nikajua tuko kwenye vita kali na hawa watu na adi sasa ni kama wanaongoza.Its either wanaume tumekuwa weak emotional au hawa watu wamekuwa manunda sana au hali ya maisha umewafanya wapagawe kabisa.NI MAAMUZI YANAYONIUMIZA
Nalazimika kumuacha mpenzi wangu ninayempenda sana, sielewi naenda kuishi maisha gani bila ya ukaribu nae, najaribu kutafuta furaha mpya lakini bado siipati, nikijumlisha na 4g ya Jana ndio naishiwa pozi kabisa.
Ni baada ya kumtembelea bila kumwambia ndipo nikajikuta nimevamia Uhuru wa mwanaume mwezangu kujiachia na nimpendae. Sikuona umuhimu wa kuanzisha vurugu ndani ya kile chumba sababu kwa hasira nilizonazo ningetia hasara wallet yangu, namshukuru Mungu mpaka naondoka ndani ya ile nyumba wapangaji hawakufahamu alichokifanya mpangaji mwenzao labda baada ya mimi kuondoka.
Huyu ni mwanamke pekee ambaye hapo kabla niliona angalau ni wife material na sikuwa na mwanamke mwingine zaidi yake nilimuamini kiasi kwamba akawa yeye ndio muongozo wa maisha yangu kumbe najidanganya mwenyewe, kila alichotaka alikipata kumbe Kuna jamaa anapata anachokitaka kutoka kwa huyu mwanadada.
Kwa sasa msaada pekee nitakaoupata Ni kutoka CHAKO NI CHAKO, sitaki Tena mahusiano.
MAPENZI NI UGONJWA WA AKILI.
Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app