Ameniambia "Hujanijua vizuri eh"

Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
319
500
Wakuu wasalaam!

Bila shaka hamjambo, kwa wenye changamoto poleni!

Wakuu nina miezi 8 kwenye mahusiano ila nimeanza kuishi nae miezi 4 iliyopita, ni binti 26 yrs mimi nina 33 yrs.

Issue kubwa amekuwa na kauli za kibabe sana kiasi zimenifanya kila mwezi na postpone kupeleka mahari kwao kwa sababu hatua za mwanzo nilishafanya.

Kila nikiwaza kupeleka mahari na haya maneno ninayopewa na wife moyo unasita.

Imekuwa ni kawaida yangu kusaidia majukumu ya home kama kuchota maji, kupika hasa akiwa zake kazini maana mimi nawahi kurudi toka job, mimi ni mfanyakazi wa shirika (jina linahifadhiwa) na kazi ndogo ndogo mara moja moja nafanya, ndivyo tulivyolelewa home lakini siku akikuta sijafanya anafoka kana kwamba ni sehemu ya majukumu yangu ya lazima, nampenda na namhudumia kama baba wa nyumba.

Mfano; Leo tumezinguana kwa issue ndogo lakini kanambia nanukuu "hujanijua vizuri kumbe"

Nimeongea nae sana kumsihi abadilike lakini naona bado, nimeshirikisha Dada yake lakini bado, ninachowaza kwa sasa ni kukaa kijeshi tu, nikae kibabe nisimjali kiufupi kila mtu awe kimpango wake!

Na zaidi naona nazidi kupata moto kutopeleka mahari naona kama hatutadumu na huyu bibie, sijajua kinachompa jeuri, historia yake kwa ndugu zake inaonekana ana kiasili cha hii tabia, mimi nina asili ya upole lakini ni mkorofi nikichoka kuvumilia.

Issue ni nyingi naomba kuweka haya ya muhimu zaidi, kama una cha kunishauri mwanaume mwenzangu karibu, na wewe mwanamke toa neno tafadhali.

Naomba radhi kama kuna makwazo kwenye uzi huu!
 

Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
319
500
Sema kweli mkuu nashangaaa sana, halafu kumsaidia sio kumuogopa nafanya kwa kuwa ni moyo wa upendo tu, na yeye anakuwa kwenye majukumu yake naona isiwe tabu nafanya.
Duuh hivi kwa nini Mwanamke ukimsadia majukumu yake ya ndani anaona kama ni wajibu wako kufanya???? Alafu huwa wanajisahau sanaa aisee mimi nishajifunzaaa bora uchelewe kurudi nyumbani kuliko kujidai unamsaidia yanakukuta haya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom